Tumiaga akili basi kujibu, akili yako imejaa utopolo tupu. Nani kakishadadia ? Pamoja na USA kuwa case 60k wewe hiyo inakuhusu ? Watanzania wanahaki ya kupewa taarifa juu ya mwendelezo wa Taarifa za Gonjwa hili.
Majuzi kati nilikuwa nachati na dada yangu mmoja yupo dar, alikuwa akienda kariakoo nikamwambia jitahidi kuwa mwangalifu na uvae barakoa..! Alichonijibu ni kuwa Corona imeisha [emoji15][emoji15][emoji22][emoji22]. Nikamwambia usiseme hivyo, subiri serikali ikisema hakuna corona ndipo useme hivyo, akanielewa akavaa barakoa.
Sasa ishu inakuja, huyu ni mmoja tu ambaye kwa sababu ya ukimya huu anajikuta anaamini kuwa ugonjwa huu haupo. Hebu vyombo husika waache ukimya bali waseme kitu ili tuokoe wenzetu ambao wataangamia kwa sababu ya kutopata taarifa.
Sent using
Jamii Forums mobile app