Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Siku tatu au nne zilizopita niliandika juu ya hulka isiyosawa ya Rais Kenyatta hasa baada ya kutenguliwa kwa uchaguzi wa wiki iliyopita.
Kenyatta si Mwanademokrasia ila Katiba ya Kenya ni ya Kidemokrasia
Mara baada ya IEBC kutangaza matokeo hayo na Raila kuyapinga, wafuasi wa kiongozi huyo wa upinzani waliingia mitaani kuandamana lakini walikumbana na vikwazo na baadhi yao kuuawa.
Haya hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, Rais Kenyatta aliingilia kati na kuruhusu waandamane kwa amani kufikisha ujumbe wa kupinga matokeo hayo bila kuharibu mali za watu wengine.
Kenyatta aliwataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi wakati wa maandamano hayo ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi.
Rais Kenyatta alisema hayo alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo akiwa katika Jengo la Harambee alikokwenda kukutana na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya kuapishwa kwake.
Katika ujumbe huo uliomlenga zaidi Odinga aliyekuwa mgombea urais kupitia muungano wa Nasa, Kenyatta aliwataka wagombea wote ambao hawakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wachukue hatua zilizobainishwa na Katiba ili kupata wanachotaka — mojawapo ni kwenda mahakamani.
Kauli hiyo ya Kenyatta haikushangaza sana, maana kutokana na hulka ya mshindani wake, inaonyesha ni mtu wa kauli na matendo ya kidemokrasia kuliko viongozi wengi wa Afrika.
Katika kipindi chake cha uongozi, Rais Kenyatta ameruhusu wapinzani kufanya siasa bila bugudha, mikutano ya kisiasa na maandamano bila vikwazo na mambo mengi yanakwenda kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo, mara baada ya Odinga kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu ambayo ilitoa hukumu ya kufuta matokeo ya uchaguzi huo, Rais Kenyatta alihutubia Taifa na kutangaza kutokubaliana na uamuzi huo lakini akasema ataheshimu mahakama. Zaidi, alisisitiza amani na utulivu wakati Wakenya wanasubiri uchaguzi wa marudio.
Hatua hiyo ilikuwa tisa na ikapongeza na dunia nzima, lakini muda mfupi baadaye, ndani ya saa 24, Kenyatta ameanza kuonyesha sura yake ya pili; alianza kutoa lugha za vitisho na kashfa kwa majaji waliohusika katika hukumu ya kihistoria iliyofuta ndoto za kuapishwa mapema.
Kenyatta anasema akirudia uchaguzi huo na akashinda tena, majaji hao walioongozwa na Jaji Mkuu David Maraga watamtambua. Anasema haiwezekani uamuzi uliofanywa na mamilioni ya Wakenya ukatenguliwa na watu wanne, na kuwa hapo kuna tatizo ambalo itabidi alishughulikie baada ya kurejea madarakani.