Mwananchi: Tunakatazwa kupakia Samaki kwenye Mwendokasi mpya

Mwananchi: Tunakatazwa kupakia Samaki kwenye Mwendokasi mpya

Ndugu yangu Chalamila angekua humu jf ningempa mbinu ya kulitatua hilo tatizo.
Hivi kwanini wakubwa hawapendi kujiunga social media ukiachia mama mmoja waziri mwenye weledi
Jibu ni moja tu. Weledi hawana. Hawapo kwa ajili ya wananchi
 
Jana Oktoba 2,,2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea vituo vya mabasi ya Mwendokasi vya Kivukoni na Kimara kukagua utoaji wa huduma na kuzungumza na wananchi.

Akiwa Kivukoni, alikutana na changamoto ya wafanyabiashara wa samaki waliodai wamezuiwa kupakia bidhaa zao kwenye mabasi mapya. Walisema hali hiyo inawapa ugumu wa kufikisha samaki sokoni.

Majaliwa alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akae na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhu, ikiwemo kuangalia njia ya kufunga mizigo yao au kutumia utaratibu mwingine. Alisisitiza kuwa changamoto hiyo lazima ipatiwe ufumbuzi mapema.

Ziara hiyo ilihitimishwa Kimara, ambapo Waziri Mkuu alitaka mabasi mapya yaendelee kutoa huduma bora na salama kwa wananchi.

Pia Soma: Mabasi mapya ya Mwendokasi ya MOFAT yaanza kubeba Abiria Gerezani–Mbezi
Mia saba tu ndo uwaachie watu shombo gari zima...
 
kwamba hata ukitumia ndoo zilizofungwa vyema hairuhusiwi!!!!sato zinapanda ndege kwa kutumia ndoo zenye mifuniko,sembuse bus la mwendokasi!!!!!

yaani hao wahudumu wa mwendokasi akili zimelalia kwenye katazo tu bila kutoa suluhisho l katazo lao,ni kama wana visa na wauza samaki.
Hizo ndio kwenye ndege Huwa abiria wanazikumbatia kwenye siti zao ?
 
Ndugu yangu Chalamila angekua humu jf ningempa mbinu ya kulitatua hilo tatizo.
Hivi kwanini wakubwa hawapendi kujiunga social media ukiachia mama mmoja waziri mwenye weledi
Weka mbinu hapa, acha maneno mingi
 
Nauli anayo lipa ni Kwa ajili ya MTU na sio mzigo.
Udart sio usafiri wa mizigo , ili mizigo ipite inabidi ikaguliwe kwa usalama. Na hili jambo sio lengo la udart.
Najua wafanyabishara wanataka mserereko kwa kukwepa matumizi ya usafiri wa mizigo Yao.

Tukisema turuhusu mizigo, watu wataingia na tv , meza, godoro etc , udart ndio itakuwa hovyo kabisa
 
Ndugu yangu Chalamila angekua humu jf ningempa mbinu ya kulitatua hilo tatizo.
Hivi kwanini wakubwa hawapendi kujiunga social media ukiachia mama mmoja waziri mwenye weledi
Kiongozi we andika huwezi jua labda yumo humu
 
Kuna muda watu wawe reasonable. Hayo magari ni ya kupandisha samaki?

Hii ndio shida ya kutokuwa na standards. Kuna mataifa wanaweka sheria kali kudhibiti watu wa hovyo kuingia au kufika maeneo fulani ili kuchuja wastaarabu katika kundi la watu wa hovyo walio wengi.

Najua sote tuna haki ya kutumia vitu public kwa uhuru kama raia huru ila kwa mtu uliyestaarabika unaweza vipi kupanda na ndoo ya samaki wabichi wenye shombo kali kwenye gari ya kisasa ambayo inajaza watu na inategemewa kutoa huduma kistaarabu?

Nadhani ifike wakati watu wasiwe na lawama za kipuuzi bali wajitathimini. Unaweza kujichanga na wenzako mkakodi kirikuu kikawabeba hadi makwenu. Mwendo kasi muwaachie wastaarabu na watu wanaopenda unadhifu na usafi.

Leo wewe unapanda na ndoo ya samaki mwingine atakuja kubeba maiti kwenye hilo hilo basi,mwingine ataingia na mbuzi na kuku. Huo upuuzi pelekeni huko Kijijini mbwinde.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hizo basi tulieni zipo kimkakati, soon baada ya uchaguzi mkuu zitarudishwa zilipotoka
 
Sasa na nyie wananchi hebu oneni aibu basi? Yaani magari mazuri yale mnataka kuyachakaza haraka kwa kuanza kuingia ndani na mizigo yenu hiyo? Kapandeni DCM na samaki zenu huko achaneni na gari hizo bado mpya zinataka usmati tu

Aisee!
 
Maendeleo yasiyo fit mahitaj/ bias kwa jamii sio haki kbs🙄
 
Katazo ni sahihi, ila watafutiwe suluhisho.

Kuna kipindi fulani jamaa alikuwa amebeba ule mchuzi wa pweza.
Kwenye purukshani za kupambania gari, mchuzi ukamwagika ndani ya gari.

Sio nzuri hata kwa abiria wengine.
Japokuwa na hawa samaki tunawaitaji huku mtaani.
 
Jana Oktoba 2,,2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea vituo vya mabasi ya Mwendokasi vya Kivukoni na Kimara kukagua utoaji wa huduma na kuzungumza na wananchi.

Akiwa Kivukoni, alikutana na changamoto ya wafanyabiashara wa samaki waliodai wamezuiwa kupakia bidhaa zao kwenye mabasi mapya. Walisema hali hiyo inawapa ugumu wa kufikisha samaki sokoni.

Majaliwa alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akae na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhu, ikiwemo kuangalia njia ya kufunga mizigo yao au kutumia utaratibu mwingine. Alisisitiza kuwa changamoto hiyo lazima ipatiwe ufumbuzi mapema.

Ziara hiyo ilihitimishwa Kimara, ambapo Waziri Mkuu alitaka mabasi mapya yaendelee kutoa huduma bora na salama kwa wananchi.

Pia Soma: Mabasi mapya ya Mwendokasi ya MOFAT yaanza kubeba Abiria Gerezani–Mbezi
Watanzania walio wengi ni wajinga!
 
Mkiharibu magari na matenga yenu ya samaki baadaye mnaanza kuilaumu serikali. Halafu hiyo shombo ya samaki kwenye vipedo vyetu haifai, tafuteni maguta kama wafanyabishara wenzenu wa ndizi mbebee hao samaki.
Tanzania nchi yangu....
 
Ndugu yangu Chalamila angekua humu jf ningempa mbinu ya kulitatua hilo tatizo.
Hivi kwanini wakubwa hawapendi kujiunga social media ukiachia mama mmoja waziri mwenye weledi
Wapo humu sema kwa majin banfia, hawana ujasiri wa kuwa live humu.
Natamani Nyerere angekuwepo kipindi kama hiki cha mitandao, yule mzee angekuwa anasepa na kijiji.
 
Mkuu hao wahudumu wameajiriwa na wana wategemezi wakileta za kujua kibarua hawana
Acha wakaze hadi abiria waisome namba
shida ya kazi nyingi has za kutoa huduma,mhudumu hatakiwi kutoa maoni hasa ya kile anachokiona eneo la kazi,ni kutekeleza anachosema boss hata kama boss hajui kitu.
 
Back
Top Bottom