Mwanangu akilia anakauka mpaka anazimia, jamani hii ni hali ya kawaida?

Mwanangu akilia anakauka mpaka anazimia, jamani hii ni hali ya kawaida?

Wana jukwaa, naomba ushauri.

Mwanangu wa mwaka 1 na nusu kila akilia anakauka mpaka anazimia, na hali hii imekuwa ikijirudia kila anapolia kabla ya kurudi katika hali ya kawaida. Kwa kifupi, inanitisha sana kwani sijui shida ni nini.

Je, hii ni hali ya kawaida kwa watoto au inahitaji matibabu ya haraka?
Mchinjie mbuzi, na uwape wazee chakula
 
Jichunguze kwenu au Kwa mwenza wako kuna mtu anakisirani? Hiyo ni ishara tosha atakuwa na hasira Kali. Mpeni Upendo na muache kumuuzi.

Pia zingatia ushauri wa mdau wa kubadiri jina, kama mwenye jina alikuwa na tabia hiyo ya hasira.
 
Wana jukwaa, naomba ushauri.

Mwanangu wa mwaka 1 na nusu kila akilia anakauka mpaka anazimia, na hali hii imekuwa ikijirudia kila anapolia kabla ya kurudi katika hali ya kawaida. Kwa kifupi, inanitisha sana kwani sijui shida ni nini.

Je, hii ni hali ya kawaida kwa watoto au inahitaji matibabu ya haraka?
Sidhani kama inakutisha kwani siku ya kwanza tu ungeshaenda hospitalini. Kweli kuna watu mna roho ngumu. Mtoto analia leo mpaka anazimia, kesho tena na tena, na bado umekalisha makalio nyumbani unakimbilia kwenye keyboard kuulizia?
 
Niliwah sikia hii Kwa mama mmoja anasema alivokuwa mdogo alikuwa na hali siziso za kawaida had walipombadilisha jina hiv ni kweli?
Ni kweli, ila sio kukauka na kuzimia? Ni kuwa huwa muda wote analia tyuuh,
Ndo anabadilishwa jina.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom