DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
ila huyu mzazi ana moyo sana hakika mimi nisinge ondoka hapo ni lazima ningekula sahani moja na huyo Mwl nisinge kubali hiyo elfu ishirini ….yani hiyo mbwa ingejuta! Lakini bado nafasi ipo huyu mtu anapaswa kusakwa!
 
Mwalimu wa field? Huyo ni mwalimu wa aina gani. Mwalimu mkuu bado yuko madarakani?
 
Kama imefikia hatua Waziri anarusha mpira kwa mtu aliye chini yake kwa tukio la kikatili na kupelekea mauaji kwa namna hii basi nchi haina uongozi.

Inaumiza sana kuuliwa mwanao alafu walioshika mpini wanalindana, haki mzazi achana na hiyo maiti hadi haki ipatikane vinginevyo ukiibeba umeruhusu jinai kuwa haki.
 
Kuna walimu ni vichaa, miaka 7 unampiga ngumi....hata kama angekua na 30 viboko si vipo kama kuna ulazima wa viboko.

Pumzika kwa amani toto, pole sana mzazi 😢
Huyo sio mwalimu ni mbwa tuuu! Yani huyu ni kula nae sahani moja…..hapa ndio naoma umuhimu wa kuroga huyu anatakiwa kufanywa awe ana jikojolea tuu muda wote….
 
Poleni wafiwa.
Mungu awape faraja.
 
Kimsingi siwezi kutoa lawama sana kwa waziri kwa sababu kimsingi awezi fanya kila kazi mwenyewe anapaswa kusaidiwa lakini anachotakiwa kuhakikisha wanao msaidia wawe active na wawe ni wenye uelewa na utu sio wajinga wajinga,jeuri ,kibri na dharau …dawati linapaswa liwe na watu wenye utu!

Kimsingi hao watu watamuharibia sana Dkt. Gwajima D sifa zake na juhudi zake maana kila mwana jf anajua anavyo jitahidi kujibu na kutolea ufafanuzi na kushughuliakia matatizo ya watu na ni kati ya mawaziri walio active sana hapa na hawaogopi mijadala…
Bila shaka atakuja kulijibu hili swala maana watu kama hawa wanao puuza watu hawapaswi kumzunguka wana muharibia sana sana!
 
Pole mama.

Umasikini ni aghari, mama kitu cha kwanza haukutakiwa kuipokea hiyo shs. 20,000/=, kwa kifupi shule ilitumia udhaifu huo kukusukumia mzigo wewe mzazi, mzazi ulitakiwa ukaripoti polisi kwa hatua za kisheria badala ya kujadiliana na shule, pia shule ilitakiwa ichukue jukumu la matibabu ya mwanao wewe ukiwa msindikizaji tu.

Udhaifu wa kupokea ile pesa ili umpeleke hospitali ndiko kulikoifanya shule ikuambie gharamis upasuaji watakurudishia pesa zako, kwa kifupi walijitoa kwenye tatizo hilo.

Mama hapo Moshi ipo mamlaka ya wizara ya elimu inayosimamia shule zote, pia yupo mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ambao ulitakiwa uende ofisini kwao kuwajulisha kuhusu tatizo hilo.

Mwisho ulitakiwa upate ripoti ya kina mobiTuki yaani postmortem ya maiti. Hii postmortem inakuwezesha kufungua kesi ya jinai dhidi ya shule na mwalimu.

Mwisho, kabla ya kupeleka tatizo lako kwa Waziri anza na viongozi wa mkoani mwako, vinginevyo utadhani unakosa msaada kumbe ni njia ambazo si sahihi unazotumia.
 
Shida ni umaskini jamani huyu mtu alicho jali mwanzo ni uhai na afya ya mtoto hakujua kama yange pelea haya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…