DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nyumba ikiharibika lawama ni kwa kiongozi wa nyumba haijalishi upo low or high mental.
 
Poleni sana Kwa Msiba huo...

Hivi inaingia akilini kabisa wewe Mwalimu mtu mzima uanze kumchapa mtoto hadi kumpiga na ngumi kabisa?

Angekuwa mtoto wako ungemfanyia hivyo?

Tuweni na kiasi jamani, it's unfair kumfanyia mtoto mdogo ukatili Mkubwa hivyo hadi kupelekea apoteze maisha🥲

Kuna wakati nilisoma mahali kwamba Viboko vimepigwa marufuku mashuleni hadi Kwa Kibali maalumu cha Mkuu wa Shule n.k na mwisho ilikuwa Viboko kama sikosei 2 ama 3, Je huyo Mwalimu alipewa kibali cha kumchapa huyo mtoto.
 
ushauri wa bure hata akienda mahakamani hatapata haki huyo mama dr gwajima hatamsaidia nchi hii , kila mtu anajua hadi yaliyoshindikana mahakamani makonda anaweza kuyatatua amvizie makonda kila anakoenda amweleze shida yake ndio ukweli wa nchi yetu akishindwa makonda amwachie Mungu au achukue mwili na kwenda kuroga mwisho.
 
Makonda ndo mahakama anatoa haki? Mkuu jitafakari
 

Pole sana Mkuu
Dkt. Gwajima D kuna kazi huku
 
Makonda ndo mahakama anatoa haki? Mkuu jitafakari
labda hujanielewa mleta mada amesema waziri muhusika na maswala hayo dr gwajima ameshindwa zipo kesi nyingi watu wanapata dhulma na watendaji wa mahakama, kwanini kwa makonda ni rahisi kusaidiwa serikali inatumia mfumo huo kwa maslahi ya chama ccm, lakini nani alikwambia mahakamani wanatoa haki, pata shida ya kisheria ndo utajua hakuna haki kule haki yako unaipigania utatoa pesa kumpata wakili na mengineyo, ukiwa huna pesa mahakama haikupi haki wewe, sio mahakamani tu hata ukienda polisi baadhi ya maeneo ukawaambie mda huu kuna majambazi yanaiba nyumbani kwangu na kubaka usipotoa hela ya mafuta hawaji yani utarudi nyumbani majambazi wamepika na ugali wamechinja kuku wamekula wameondoka zao.
 
Nimesisimka Kwa uchungu
 
Kwanini Dr D kamrudisha mara 2 kwa yule yule aliekataa kunsaidia?
Najiuliza hili swali sana
Msipopiga marufuku kuchapa watakufa wengi kwa upumbavu wenu
Ipo siku mwalimu atachinjwa pia ndio mtajua hamjui
Unampiga mtoto kama una uadui nae
Ngumi kweli mtoto mdogo why?
Mmezidi unyonge
 
Nchi inalaaniwa kwa mambo kama haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…