Pole sana mkuu kwa hiyo changamoto na nikutie moyo tu kwamba mtihani humfika auwezaye,
Mwaka juzi binti yangu mwenye miaka minne sasa alithibitika ana tatizo la sickle Cell anemia, Nililazimika kufanya kipimo hicho baada ya kuona anasumbuliwa na homa za mara kwa mara na mbaya zaidi ni maumivu ya viungo hili lilinistaajabisha inawezekanaje mtoto wa miaka miwili alalamike mguu ama mkono unamuuma? Katika hali ya kawaida baada ya kupata majibu nilipanic sana lakini baada ya muda niliamini MUNGU amenipa mtihani ninaouweza. Nilipata wakati wa kuutafiti na kuuelewa huu ugonjwa kupitia kwa wataalamu wa afya na wahanga wa sickle cell hakika nilijifunza mambo mengi ambayo ningependa ku-share na wewe.
Chanzo cha Ugonjwa wa Sickle Cell.
Kama baadhi ya wataalamu na wachangiaji hapo juu walivyoeleza, Sickle Cell ni ugonjwa wa kurithi ambao mtoto anazaliwa nao, mtoto anarithi huu ugonjwa kutoka kwa wazazi wote wawili (Mama na Baba), hapa naomba unielewe vizuri kwani kuna upotoshaji mkubwa ambapo unaweza kutengeneza tatizo kubwa sana juu ya tatizo kwani kuna baadhi watakwambia kama hakuna historia ya huo ugonjwa kwenye ukoo wenu basi mtoto umepigwa, sawa linaweza kuwa jibu lakini sio sahihi, uelewe kwamba kuna sickle Cell carrier na sickle Cell severe. Kwa historia jamii nyingi sana za kiafrika tuna changamoto ya sickle Cell carrier lakini kadri miaka inavyosogea tuanenda kwenye severe. Ok tuachane na mambo ya takwimu ila nilitaka kumaanisha kwamba sickle Cell carrier sio mgonjwa ila tu ndani yake ana vinasaba vya sickle Cell ila haishauriwi kuitumia damu yake kumuongezea mtu mwingine hii ilinitokea nikiwa kidato cha sita nilichangia Damu coz mimi ni group O+ positive lakini siku alivyorudi doctor kutoa majibu alinishauri nisitoe damu tena japo namlaumu hakuwa muwazi labda ingenisaidia sana. Sasa ikitokea mama na Baba wote mkawa carrier kuna high chance ya kuzalisha severe pale wakataki wa kuchangia gene wote mkatoa vinasaba vya sickle Cell, hivyo achana na hayo mambo ya DNA sio jawabu la hilo tatizo kwa sasa.
Tiba
Sickle Cell anemia haina tiba ya moja kwa moja, isipokuwa kwa sasa kuna njia ambazo hutumika kama tiba:
(i)kupandikiza uroto (bone marrow) gharama zake kiukweli ni around 60million roughly ila kuna unafuu coz serikali sasa imetenga budget kabisa kwa ajili ya kusupport matibabu hivyo inaweza kuwa chini kidogo ya hapo lakini pia kama unatumia bima kwa kiasi wanasaidia nakumbuka bima yangu walisema wanaweza kunichangia kama 20million. Haishauriwi kufanyiwa mtoto aliye chini ya 10 years coz kuna complications sana.
(ii) Kufanya vipimo vya damu kwa wanandoa watarajiwa kabla ya kuchukua maamuzi ya kufunga pingu za maisha, unaweza kuona kama ukatili fulani hivi eeh? Brothers and Sisters huu ugonjwa ni wa mateso makali sana just imagine mtoto anaejifunza kuongea analia kwa uchungu anasema "Baba/Mama mimi naumia sana" hakika kuna wakati unaweza kujuta kwa mateso ambayo mtoto anayapitia, nashauri tena fanyeni vipimo kabla coz sickle Cell is real.
Jinsi ya kuishi na mgonjwa wa sickle cell
●Hakikisha anakula mboga za majani kwa wingi, beetroots juice, rosella, watermelon.
●Anywe maji mengi sana ila kusukuma zile cells zilizokufa na kuifanya damu kuwa nyepesi.
●azingatie dozi ya folic acid
●Hakikisha anakaa mazingira amabayo hatashambuliwa na magonjwa kama malaria na mafua huwa yanapelekea kupata crisis.
● Pia hakikisha hapati stress wala usiwe unamfokea ama kumtishia mara kwa mara coz pia inaweza kuwa sababu akareact.
●Baridi ama joto kupindukia pia ni changamoto sa kwako anaweza kupata pneumonia
●Hakikisha anahudhuria monthly clinic and monthly check up.
Ni hayo machache nadhani wataalmu wapo hapa wataendelea kutufundisha na kutuongoza zaidi.🙏