Rozela
JF-Expert Member
- Jan 5, 2024
- 845
- 2,235
Yuko primary, ameniambia zaidi ya mara 5 kuwa anatamani sana kuwa askari polisi, ikifika jioni jioni anaanza kupiga kwata kuzunguka nyumba na kupiga saluti.
Akikutana na wenzake anataka wacheze kipolisi yeye awe askari polisi, siku nyingine anaigiza kuongoza magari na kuongoza wanafunzi kuvuka barabara.
Leo ndio funga kazi, baada ya kufunga shule kapitia kituo jirani cha polisi kaja na majarida kadhaa kuhusu mambo ya usalama wa raia inaonesha alienda kuwahoji maswali kadhaa wakampa zawadi.
AKienda shule anarudi akiwa msafi vilevile anasema polisi sio wachafu.
NAMTOAJE KWENYE HILI JANGA WAKUU BILA KUM-ATHIRI KISAIKOLOJIA?