Mwanangu anasumbuliwa na mafua yasiyotoka njia za puani (ana mwezi mmoja tu)

Mwanangu anasumbuliwa na mafua yasiyotoka njia za puani (ana mwezi mmoja tu)

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
971
Reaction score
1,165
Habari ndugu wapendwa katika imani! natumai mmeamka salama na mpo kwenye majukumu ya kila siku.

naomba nielekee kwanye hoja au maombi ya kimawazo, ushauri au tiba kwa aliyekutwa na hili tatizo na kufanikiwa kulimaliza kwa namna yoyote.

Mtoto wangu tatizo la kufura kwa mafua yasiyoka puani lilianza wiki moja mbele tangu alipozaliwa ili hali yalikuwa mafua ya kawaida kutokana na hali baridi ya usku unapongia kwa eneo tulipo, wiki ya pili mtoto alianza kupata shida ya mafua ya kufura kila ilipoanza kuingia jioni! ikautlazimu kumpeleka hospital ya karibuni na dk akatunandikia nasal drop.

Lakini matumizi ya dawa hiyo yalitupa ahueni kwa sku tatu tuu..! lakini mbaka sasa hamna nafuu ya kuridhisha bado usku anapata sana tabu kulala!

Natanguliza shukrani za dhati kwenu, na mungu awaongoze nipate majibu mema yenye msaada kwa mwanangu. AMEEN.🙏
 
Umri wake ni kiasi gani. If umri unaruhusu Jaribu dawa inaitwa Pediatric hiyo ndo imemuokoa sana mwanangu. Ni bit expensive but majibu yake ni ya haraka.

Pia epuka kutumia sabuni zenye manukato kufulia Nguo za mtoto au za mama, na kuhakikisha mnafanya usafi mara kwa mara kuondoa vumbi...ikishindikana muone specialist

Screenshot_2021-09-25-09-04-39-889_org.mozilla.firefox.jpg
 
Nilipokuwa nasoma nyuzi hii nikatabiri huyu mtoto atakuwa ndo kazaliwa, kwa sababu nina uzoefu na tatizo la mtoto mchanga.

Usichoke na kujiskia vibaya sana ukaona umezaa mtoto mbovu, kwa sababu kila mtoto mchanga huwa ana changamoto zake.

Kuhusu hiyo changamoto, wewe endelea kutumia hizo dawa unazoshauriwa na dokta, na kadri anavyokuwa basi ugonjwa hupungua.

Nakumbuka mtoto wangu yeye alianza kuugua mafua na kikohoo akiwa na miezi 3, na alikuwa anapewa hizo hizo dawa za kikohoo na mafua za maji. Dokta alianiambia kama hakuna ugonjwa wa kurithi basi atabadilika kadri anavyokua. Sasa ana miaka 3 ameacha kukohoa na mafua.
 
Umri wake ni kiasi gani. If umri unaruhusu Jaribu dawa inaitwa Pediatric hiyo ndo imemuokoa sana mwanangu. Ni bit expensive but majibu yake ni ya haraka..pia epuka kutumia sabuni zenye manukato kufulia Nguo za mtoto au za mama, na kuhakikisha mnafanya usafi mara kwa mara kuondoa vumbi...ikishindikana muone specialist

View attachment 1951827
ana mwezi mmoja tu mkuu
 
Uwe unamnyonya makamasi mtoto.achana na dawa za kizungu
sio makamasi ya kutoka mkuu! nilishauriwa kama ni ya kuchuruzika niyanyonye kidogo kidogo! lakini yake yanafoekea ndani
 
ana mwezi mmoja tu mkuu
Kama hapandishi homa endelea na hiyo nasal ndop na kupunguza hayo manukato...na pia kama Kuna Nguo, mashuka amerithi achana nayo coz wakati mwingine huwa zimekaa muda mrefu sana kiasi ambacho ukija mvalisha mtoto mchanga mpya zinakua zinamletea shida.

Tatizo likiendelea nenda kwa specialist wa watoto anaweza kuwa msaada Zaidi.
 
sjaelewa maanake
Ni ugonjwa yaani unaweza kuwa na mafua ata mwaka hayakati watu hawa wanakuwaga na allergy ya nyama akila tu yakimpata yanachukua mda baadhi ya dawa zake nilizion za asili wamechanganya miti sijui wadudu inanuka then mgonjwa ananusa.

wengine wengi wanazaliwa na kambaku ni ugonjwa kama pumu tu na unarithishwa kama kawaida.
 
Umri wake ni kiasi gani. If umri unaruhusu Jaribu dawa inaitwa Pediatric hiyo ndo imemuokoa sana mwanangu. Ni bit expensive but majibu yake ni ya haraka..pia epuka kutumia sabuni zenye manukato kufulia Nguo za mtoto au za mama, na kuhakikisha mnafanya usafi mara kwa mara kuondoa vumbi...ikishindikana muone specialist

View attachment 1951827
Mi mwanangu ana miaka mitatu net.
lakini ana makamasi yanamtoka tu tena yale mazito mazito

nishatumia sana dawa za.maji lakini wapi

vipi nikiongeza na hii itaweza kukata?
 
Mi mwanangu ana miaka mitatu net.
lakini ana makamasi yanamtoka tu tena yale mazito mazito

nishatumia sana dawa za.maji lakini wapi

vipi nikiongeza na hii itaweza kukata?
Makamasi yanamtoka au ana mafua
 
Back
Top Bottom