Mwanangu hawezi kukaa naomba ushauri wa matibabu

Kusamburo

Member
Joined
Jan 9, 2020
Posts
48
Reaction score
48
Nina mwanangu ana umri wa miaka 2 sasa. Hawezi kukaza kichwa wala hajaweza kukaa. Nimeenda hospitali hadi leo ni mazoezi tu tatizo hasa sijalijua.

Naombeni mwenye kuelewa anieleweshe nitashukuru.

Nipo Zanzibar.

MAONI YA WADAU:
===
===
 
Unapoishi namini wapo watu wazima hususani wamama wenye umri kuanzia miaka hamsin nakuendelea ambao wana wajukuu na watoto jaribu kuwafuata waelezee unaitaji msaada watakusaidia funguka wazi wazi hata kama upo ofisini share tatizo lako kwa wenzako sema tu jamani naitaji msaada mwanangu ana moja mbili naimani atapatikana wakukusaidia

Wengi huona matatizo ya mtu ila hukaa kimya kwani wanasubilia mhusika aseme
 
Huyo mtoto alivyozaliwa alilia hapo hapo au ilichukua muda kidogo? Alipata njano ya macho? Leba ilichukua muda gani?
Alipata shida ya kupumua alivyozaliwa? Alikuwa analia kwa nguvu na miguu na mikono inacheza au ilikuwa kivivu vivu?
Nina mwanangu anaumri wa miaka 2 sasa.hawezi kichwa wala hajaweza kukaa
Nimeenda hospital hadi leo ni mazoezi tu tatizo hasa sijalijuwa
Naombeni mwenye kuelewa anieleweshe nitashukuru
Nipo znz
 
Huyo mtoto alivyozaliwa alilia hapo hapo au ilichukua muda kidogo? Alipata njano ya macho? Leba ilichukua muda gani?
Alipata shida ya kupumua alivyozaliwa? Alikuwa analia kwa nguvu na miguu na mikono inacheza au ilikuwa kivivu vivu?
Alipozaliwa alipiga umanjano ikabidi kumrudisha hospitali kwa sababu alikuwa hata kunyonya hawezi
Na alipotoka alifanyiwa vipimo ikaonekana kilakitu yuko sawa na ubongo wake unafanya kazi vizuri tu
 
Alipozaliwa alipiga umanjano ikabidi kumrudisha hospitali kwa sababu alikuwa hata kunyonya hawezi
Na alipotoka alifanyiwa vipimo ikaonekana kilakitu yuko sawa na ubongo wake unafanya kazi vizuri tu
Alipozaliwa alilia lkn umanjano alifanya mwili mzima hadi macho
 
Alipozaliwa alipiga umanjano ikabidi kumrudisha hospitali kwa sababu alikuwa hata kunyonya hawezi
Na alipotoka alifanyiwa vipimo ikaonekana kilakitu yuko sawa na ubongo wake unafanya kazi vizuri tu
Huenda hiyo njano ndio imesababisha hiyo hitilafu. Hii kitu inaitwa "Kernicterus" au "Bilirubin encephalopathy". Njano ikiachwa mpaka ikazidi viwango Fulani, huleta shida kwenye sehemu ya ubongo inaitwa basal ganglia na ndio maana mtoto amechelewa kufikia milestones zake kulingana na umri, maana hiyo sehemu ya ubongo ndio inacontrol movement.

Naomba kujua vidole gumba vyake vya mikono anaviwekaje. Huwa wanakuwa na namna Fulani wanakunja kidole gumba kinagusana na kiganja halafu wanafanya kama ngumi Fulani hivi muda wote. "Cortical thumbing"

Cha kufanya kazana na mazoezi kwa bidiii sana ili aweze kuwakamata wenzake wa umri huo. Mtoto ni kama udongo, though amepata shida hiyo lakini unaweza ukamfinyanga akawa sawa ukiweka bidii.
 
Shida ipo kwenye uti wa mgongo !! Sema ni mdogo angekuwa mkubwa angefanyiwa upasuaji kuziweka vizuri pigili za uti wa mgogo

Sent using i phone x
 
Jaribu kusoma hii link hapo chini kama inafanana na dalili za mtoto wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yap na hiyo anaweza hata kupata cerebral palsy so mazoezi ni muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliyoeleza yote yako sahihi kwa mtoto wangu
Asante sana nitazidisha juhudi ya mazoezi
Kwa hiyo unataka kunambia hakuna njia nyengine ispokuwa mazoezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…