Mwanangu kanifundisha somo la Uraia kuhusu uhuru wa kisiasa

Mwanangu kanifundisha somo la Uraia kuhusu uhuru wa kisiasa

Woga mwingi huondoa maarifa,hivi kwanini CCM inatumia nguvu za ziada kumsambaratisha Chadema hata kabla ya ballot box?
Huyu huyu Chadema anayeshinda mahakamani kila siku akishtakiwa kwa mdomo mbovu?
Huyu huyuChadema anaesimama jukwaani akishuka tu anapelekwa Segerea?
Ccm intumia nguvu kupambana na cdema sababu wanajua kwenye kampain hawana cha kuwaeleza watz. Watazungumzia miradi ambayo haijakamilika na miradi hewa. Hawana kiwanda hata kimoja cha kuonesha. Yani sera ya viwanda ndyo imekufa. Najiuliza watakuja na sera gani mpya.
 
Umeelewa maswali aliyouliza kijana au umechagua tu maadhi ya maswali ili yakutengenezee comment?

Moja ya sifa iliyomfanya bashiru kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa ccm, ni kuongoza vizuri japo la kuchunguza mali za ccm, hii ni kwamujibu wa mamlaka ya uteuzi.

Mbona hamkutuma takukuru pindi mlipopata mashaka?
Na baada ya kugundua ufujaji wa fedha za ccm, mbona hamkutumia hata polisi kuwachukulia hatua wabadhirifu?

Acheni upimbi bhana
Kwani hukusikia baada ya kamati ya Dk Bashiru kugundua huo ubadhirifu kuwa watu walishugulikiwa na kunyag'anywa mali walizokuwa wamepora.
Au mnajifanya kuwa hamjui? Pimbi ni wewe ambae unafikiri kwa kutumia makalio,huku ukijamba mawese.
 
Jana nilienda Shinyanga Mjini baada ya siku kama nane hivi tangu nitoke Dar kwenye msiba wa Ndugu yangu aliyefariki na corona - hata kama vipimo havikuonesha lakini dalili zote zilijitokeza.​

Jioni wakati naelekea stendi nipande gari za Maganzo nikaona ninunue magazeti. Magazeti yanayowahi Shinyanga yanaingia kabla ya saa 2 asubuhi - yale yanayotekea kwa Mwanza. Sasabasi nilinunua tu magazeti kama matatu hivi mojawapo likiwa Mwananchi na sikulisoma kichwa chake cha habari.​
​
Kwa kuwa kwenye daladala tulibanana (hatujali corona) sikuweza kuyasoma hayo magazeti mpaka nilipofika maskani. Baada ya kufika mwananngu ambaye jumapili anatakiwa aende shuleni Mara akaniambia anaomba gazeti la Mwananchi alipitie (akanikumbusha pia wkt nafanya kazi kil siku nilikuwa narudi nyumbani na magazeti - nikajichekesha tu).​

Baada ya kumpa lile gazeti aksoma kichwa cha habari ambacho kilionesha kuwa CHADEMA wanafuatiliwa kwa matumizi ya fedha ambazo walikusanya kutoka kwa wabunge wao. Basi akaniuliza maswali kadhaa kama vile je hao wabunge walilazimishwa kukusanya, je fedha hizo alipewa tu Mbowe?​
​
Je, kama zilikuwa ni za wabunge wametoa kwenye chama chao inakuwaje Serikali hasa TAKUKURU waingilie kufanya uchunguzi, basi akaniuliza maswali mengi tu na mwishowe akaniambia - kama yeye anaona vile Serikali haikitaki kabisa CHADEMA. Hapo nikaguna - nikamwambia inawezekana lkn nikamwuliza kwani yeye kaona nini cha ajabu?​

Akaniambia hivi hata CCM nao wanaweza wakahojiwa kwa ajili ya matumizi ya fedha zao? Kwa mfano akajitolea mfano mwenyewe kwamba mwaka jana alinunua kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM na anaamini inaweza ikawa haijatumika vizuri sababu hata risiti hakupewa.​

Je, anaweza kumwajibishaje yule aliyemwuuzia kadi ile kama atakuwa katumia fedha za kadi vibaya? Akaendelea kuniambia mfano Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA anahusishwa sana na fedha za CHADEMA, je hiyo inaweza pia ikafanyika kwa Mwenyekiti wa CCM iwapo CCM inakuwa na matumizi mabaya ya fedha?​

Kuonesha ana ufahamu mzuri kuhusu siasa akasema Dr JPM alipoingia madarakani aliunda timu ambayo ilibaini ubadhirifu wa mali za CCM wkt wa JK, je kwa kuwa JK alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM wakati huo kwa nini hata haikuwahi kusemwa kuwa TAKUKURU wamhoji JK kuhusu matumizi ya fedha hizo?​

Kwa kweli mwanangu Fadhili aliniuliza na kujadili nami mambo mengi sana kuhusu habari ya Mwanachi jana na mambo ya TAKUKURU inavyofanya kazi kwenye ulingo wa siasa hadi nikajiuliza kuhusu Mwl anayemfundisha General Studies huko shuleni kwake (siitaji shule isije ikaleta tatizo). Inawezekana Mwl huyo anawafundisha watoto siasa ngumu sana.​

Zaidi ya yote mwanangu alinionesha ni namna gani vijana wadogo wa umri kama wake wa miaka 19 wanaanza kuelewa dhana ya uhuru wa kufanya siasa kwa haki na kwa uhuru. Anaonesha kwa mifano halisi namna uhuru wa kufanya siasa unavyobinywa.​

Mpaka mwaka jana alikuwa anaisema vizuri CCM kutokana labda ni kunifariji mimi niliyekuwa MwanaCCM. Kwa sasa naona anabadilika na hata rafiki zake nafikiri watakuwa wanafikiri kama yeye. Ninavyotabiri kwa matendo haya CCM inaweza ikawa sio salama sana!​
Mhamishe mwanao hiyo shule anaposoma kisha MTIE DOLE. Mtoto wako anauliza maswali ya kipuuzi na wewe mzazi kwakua ni mpuuzi unakuja kuanzisha uzi wa kipuuzi kutokana na upuuzi uliojadiliana na mwanao!

Nitakujuza upuuzi wako na wake pia (mwanao)

1. TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria inayo mamlaka ya kukagua taasisi yoyote iwe ya umma au isiyo ya Serikali ni hivi majuzi tu walianzisha uchunguzi dhidi ya TFF aidha walifanya vivo hivyo katika kampuni ya Katani kule jijini Tanga.

2. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi TRA unatakiwa kudai risiti na kupewa risiti kwa malipo yoyote yanye thamani ya kuanzia Tzs 100. Hivyo mwanao amemsaidia huyo aliyemuuzia gani ya umoja wa vijana kukwepa Kodi.

3. Mhe. Freeman Aikael Mbowe kuhojiwa na TAKUKURU ni sawa kwakua yeye ni miongoni mwa SIGNATURES watatu katika akaunti inayodaiwa kuchotwa fedha hizo.

Usisahau kumtag mwanao

AHSANTE
 
Kwn majibu ya waliofuja hela za ccm c yalitoka?? Nani aliitwa na Takukuru kuhojiwa baada ya kamati kusema kuna ubadhifu mkubwa wa mali za chama?? au baada ya CAG kutoa hati chafu kwa ccm wa upotevu wa milion 830 nani aliitwa na Takukuru kuhojiwa?? kama kweli chama chenu kina watu safi ni nani kati ya magufuri au Katibu mkuu alikemea huo upotevu na kusababisha ccm ipate hati chafu??? M'kiti wenu anajinasibu eti anapambana na rushwa , mbona ni miaka minne sasa ccm inapata hati chafu mfurulizo na amekuwa bubu?? hii tunaita zilongwa mbali na zitendwa mbali...msitake kuipaka chadema matope kwa mgongo wa Takukuru...Takukuru pia ni wezi na wala rushwa kama serikali yao....sisi tutasimama na ripoti ya CAG hata kama watakuja na matokeo ya kumfurahisha jiwe na wasiotutakia mema sisi chadema..mbona Tr 1.5 hadi leo hazijulikani ziliko na mmeufyata???
Siku ambayo wanachama wa vyama vya upinzania nchini watakapojua kwamba KOSA HALIFUTWI KWA KOSA watakua tayari kupewa nchi hii na kuiongoza.
 
Siku ambayo wanachama wa vyama vya upinzania nchini watakapojua kwamba KOSA HALIFUTWI KWA KOSA watakua tayari kupewa nchi hii na kuiongoza.
Usitake kujificha kwenye shamba la maharagwe...kati ya chadema na ccm nani amefanya vibaya kwenye huu utawala wa awamu ya tano kwenye matumizi ya fedha??? CAG ni shahidi kwa hilo...acha kujipoteza kwa kivuli cha upinzani
 
Tatizo la mitoto ya mtaani ndio hii hainaga jema
 
Ccm intumia nguvu kupambana na cdema sababu wanajua kwenye kampain hawana cha kuwaeleza watz. Watazungumzia miradi ambayo haijakamilika na miradi hewa. Hawana kiwanda hata kimoja cha kuonesha. Yani sera ya viwanda ndyo imekufa. Najiuliza watakuja na sera gani mpya.
Sera ya kukausha mifuko ya wananchi.Hakuna mzunguko wa pesa.
 
Mhamishe mwanao hiyo shule anaposoma kisha MTIE DOLE. Mtoto wako anauliza maswali ya kipuuzi na wewe mzazi kwakua ni mpuuzi unakuja kuanzisha uzi wa kipuuzi kutokana na upuuzi uliojadiliana na mwanao!

Nitakujuza upuuzi wako na wake pia (mwanao)

1. TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria inayo mamlaka ya kukagua taasisi yoyote iwe ya umma au isiyo ya Serikali ni hivi majuzi tu walianzisha uchunguzi dhidi ya TFF aidha walifanya vivo hivyo katika kampuni ya Katani kule jijini Tanga.

2. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi TRA unatakiwa kudai risiti na kupewa risiti kwa malipo yoyote yanye thamani ya kuanzia Tzs 100. Hivyo mwanao amemsaidia huyo aliyemuuzia gani ya umoja wa vijana kukwepa Kodi.

3. Mhe. Freeman Aikael Mbowe kuhojiwa na TAKUKURU ni sawa kwakua yeye ni miongoni mwa SIGNATURES watatu katika akaunti inayodaiwa kuchotwa fedha hizo.

Usisahau kumtag mwanao

AHSANTE
Mpuuzi kajibiwa na Mpuuzi mwenzake. Wapuuzi wanajuana!
 
Back
Top Bottom