Mwanangu kaniuliza baba mbona mama kajaa tumbo (mjamzito) nimepatwa na kigugumizi. Wewe ungejibuje?

Mwanangu kaniuliza baba mbona mama kajaa tumbo (mjamzito) nimepatwa na kigugumizi. Wewe ungejibuje?

Mjibu anamimba akiuliza mengine ya ndani zaidi mwambie ukikua utajua.
 
Very good answer

Mungu ndiye kamuweka humo, je akiuliza huyo Mungu yuko wapi na saa ngapi alimuweka huyo mtoto tumboni kwa mama?? Au akimfuata na kumuuliza mama jinsi gani Mungu alimuingiza huyo mtoto tumboni mwake???.

Ujue kuna learning and acquiring, kuna baadhi ya vitu mtoto ana acquire hii ni pamoja na kujua jinsi mimba inavyopatikana.
 
Pole Sana sijui utamdanganya nini na wakati siku unakula mzigo yeye alijidai amelala akawa anawaangalia
 
Naona wazazi, walezi, ndugu na jamaa ndio mnaolea taifa la waongo. Mnaua curiosity!

Kuna shida gani kumwambia mama ana mtoto tumboni, ambae ni mdogo wake.

Akiendelea kuuliza mjibu ukweli kwa lugha nyepesi.
 
Hebu toa ukweli huo kwa lugha nyepesi tuuone. Tupe mfano if it were you...!
 
Swali hili nililoulizwa na mwanangu Justine wa miaka 4 limeniacha mdomo wazi na nimeshikwa na kigugumizi.

BABA MBONA MAMA KAJAA TUMBO?

Wewe ungejibuje hebu tusaidiane wakulungwa.
Ungemwambia tu 'mama tumbo linamuuma'
 
Swali hili nililoulizwa na mwanangu Justine wa miaka 4 limeniacha mdomo wazi na nimeshikwa na kigugumizi.

BABA MBONA MAMA KAJAA TUMBO?

Wewe ungejibuje hebu tusaidiane wakulungwa.
Si ungemwelekeza kwa aliyejaa tumbo ili amwelezee/ ampe jibu?
 
Halafu ngoja...

Sie wa pande hizi enzi hizo tulikuwa tunadanganywa mtoto anapatikana baharini... wazee wetu Mungu anawaona!!

Hivi wale ambako bahari hamna watoto wao walikuwa wanawadanganya mtoto anapatikana wapi?!

Mizee ya enzi za Nyerere bure kabisa!!!

Halafu tukishindwa kufanya uvumbuzi mtuambie vijana wa siku hata ubunifu hatuna wakati mmeanza kutulisha ujinga tangu tukiwa makinda!! Hivi walikuwa wanafikiria nini hawa?! Mtoto na bahari wapi na wapi?! Aaarrrgh!!

Btw, hivi sasa watoto wakiwauliza mtoto anapatikana wapi huwa mnawajibu nini?!
 
Chakwangu kina miaka minnne hakikuniuliza ila kilinitaarifu baba ticha jackline anatumbo kubwa kuna mtoto tumboni ,nikamzuga ili aone kawaida nikamwambia nikweli hata humu kuna mtoto nikamshikisha kitambi changu kakaniambia humu kuna mavi wababa hawamezi watoto nilicheka kwa woga moral of the story ni bora ukaambie mwenyewe kuliko kaambiwe na mtaa
 
Kwa nini hapana?
Mwambie humo kuna mtoto. Akikuuliza kainhiaje anatokaje mwambie Mungu kamweka na atamtoa kama alivyokutoa wewe. Je Mungu ni nano? Mwambie ndiye ameba kila kitu mengine endelea. Usidanganye maana atauliza na wengine watamwambia na atakurudia kukusuta kuwa ulimdangnya. Sasa hapo pa Mungu hata akiuliza mwisho ni kweli Mungunndiye muumbaji
 
Halafu ngoja...

Sie wa pande hizi enzi hizo tulikuwa tunadanganywa mtoto anapatikana baharini... wazee wetu Mungu anawaona!!

Hivi wale ambako bahari hamna watoto wao walikuwa wanawadanganya mtoto anapatikana wapi?!

Mizee ya enzi za Nyerere bure kabisa!!!

Halafu tukishindwa kufanya uvumbuzi mtuambie vijana wa siku hata ubunifu hatuna wakati mmeanza kutulisha ujinga tangu tukiwa makinda!! Hivi walikuwa wanafikiria nini hawa?! Mtoto na bahari wapi na wapi?! Aaarrrgh!!

Btw, hivi sasa watoto wakiwauliza mtoto anapatikana wapi huwa mnawajibu nini?!

Nakumbuka kuna dogo mmoja wazazi wake
Walisema huyu hasikii.. ukimwambia kitu analeta ujeuri..tumrudishe baharini tukachukue mtoto mwingine..
Dogo alilia siku nzima akawa mpole
Anaogopa kurudishwa baharini..

Baadae tulivyokuwa kidogo
Tulijua Mke na mume wanaomba ndo Mungu
Anawapa mtoto ..na tumbo ndo mimba
Ila inapatikana Kwa kuomba
Na kuzaliwa kuna bunduki maalum anapigwa
Mwenye mimba ndo mtoto anatoka..
Hizo bunduki ni maalum haziui ..zinatumika
Hospital tu...

Siku hizi ukimpa mtoto hizo story
Anakwambia Bora Ngombe wanazaa wenyewe
 
Naona wazazi, walezi, ndugu na jamaa ndio mnaolea taifa la waongo. Mnaua curiosity!

Kuna shida gani kumwambia mama ana mtoto tumboni, ambae ni mdogo wake.

Akiendelea kuuliza mjibu ukweli kwa lugha nyepesi.

Shida ni curiosity
Baadhi ya watoto wakijua mtoto anapatikana
Baada ya sex huenda kujaribu Ku sex ili wapate na wao watoto...

Kumbuka watoto huona mtoto mdogo ni kama mdoli...

Kingine ukiwaambia kuna Mtoto ndani ya tumbo huwezi jua curiosity Yao itaishia wapi?
Wanaweza hata kujipasua tumbo ili waone Kama na wao kuna Mtoto..
Some informations ni dangerous Kwa watoto
Wakipewa jumla jumla
 
Hebu toa ukweli huo kwa lugha nyepesi tuuone. Tupe mfano if it were you...!

Tumbo la mama kubwa kwa sababu kuna mtoto. Akizaliwa atakua mdogo wako. Hata wewe umetoka kwenye hilo tumbo la mama. Na mama katoka kwenye tumbo la mama yake, na baba katoka kwenye tumbo la bibi ambaye ni mama yake baba. Umeelewa mtoto mzuri?
 
Swali hili nililoulizwa na mwanangu Justine wa miaka 4 limeniacha mdomo wazi na nimeshikwa na kigugumizi.

BABA MBONA MAMA KAJAA TUMBO?

Wewe ungejibuje hebu tusaidiane wakulungwa.
Mwambie Kuna mdogo Mungu amemweka huko,ajiandae kupata mtu wa kuchezea naye
 
Shida ni curiosity
Baadhi ya watoto wakijua mtoto anapatikana
Baada ya sex huenda kujaribu Ku sex ili wapate na wao watoto...

Kumbuka watoto huona mtoto mdogo ni kama mdoli...

Kingine ukiwaambia kuna Mtoto ndani ya tumbo huwezi jua curiosity Yao itaishia wapi?
Wanaweza hata kujipasua tumbo ili waone Kama na wao kuna Mtoto..
Some informations ni dangerous Kwa watoto
Wakipewa jumla jumla

There is no dangerous information than misleading information. Fyi huyo mtoto pengine ana idea au anajua mchezo mzima anataka confirmation toka kwa mtu anayemwamini.

Kwa hiyo mtoto akikua utamwambia ulimdanganya kuua curiosity yake?

Tunaweka negativity hata kwenye malezi tukitegema tuwe na kizazi positive?

What if kumwambia kuna mtoto tumboni kukazidisha udadisi kupelekea mtoto ampende mamake zaidi au kutaka kuwa daktari wa kina mama au wa.watoto?
 
Back
Top Bottom