Swali hili nililoulizwa na mwanangu Justine wa miaka 4 limeniacha mdomo wazi na nimeshikwa na kigugumizi.
BABA MBONA MAMA KAJAA TUMBO?
Wewe ungejibuje hebu tusaidiane wakulungwa.
Majibu utakayompa yalingane na upeo wake na uwezo wa kupambanua mambo, usimpe majibu makubwa kuliko uelewa wake na usimpe majibu mepesi chini ya kiwango cha uelewa wake maana kila jibu utakalompa litazaa swali, pia majobu yalingane na jinsia yake, watoto wa kiume hulka zao ni tofauti na wa kike
Wakati niko na mimba ya last born wangu, my first born alikua around 6 yrs na alijua grade one, ilifika wakati tukaanza kuwajenga watoto wetu kwamba we are expecting a baby na mtakua na mdogo wenu na tukawaambia mpaka jinsia, sababu ilikua ni kuwajenga kisaikolojia ili mtoto atakapozaliwa wasiwe na mapokeo tofauti,
Siku moja nikaenda shuleni kwa mwanangu kupeleka risiti za ada, kumbe aliniona na akawaonyesha wenzake kwamba yule ni mama yangu
Jioni aliporusi nyumbani akaniambia mamy Makayla told me that you ara having a baby in your stomach thats why your stomach is too big, ilibidi tu nimwambie ni kweli na ndio maana tuliwaambia kwamba we are expecting a baby, mwanangu wa kiume yeye hakuhangaika na maswali mengi aliridhika na jibu na akaendelea kuendesha magari yake, shida ni huyu wa kike
maswali yaliyozuka hapo yalikua ni mengi na inabidi akili kuyajibu maana kila unachomjibu kinaweza kuzaa swali na asiporidhika atawauliza wenzie shuleni au hata mwalimu, akija anakuja na jibu la mwalimu na jibu la marafiki basi ni vurugu tupu
Swali kubwa hapo aliuliza huyo baby ameingiaje kwenye stomach yako na atatokaje, hapa ndio ilibidi nimdanganye tu kwamba kuna sindano ukichoma baby anaingia kwenye stomach na dokta anapasua stomach anamtoa then you be back to noramal akili yake ikatulia lakini kila tukiona mjamzito ananiambia mama yule ana baby kwenye tumbo
Kids are so curious sometimes ni kutafuta namna ya kuwaeleza isiwe uongo sana maana watoto wa karne hii wanajua vitu vingi na wana intereact na wenzao in unexpected ways