Mwanangu Makonda, hakika, hautapata unachokitaka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nitahakikisha hilo. Nami nipo hapa Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya chama changu CCM kama mmoja wa mwalikwa. Uridhike na ulichopewa chamani.

Ulipoteuliwa tu kuwa Mwenezi wa CCM, hima ukaanza tamaa ya Ukatibu Mkuu. Ukaratibu bila utaratibu wala kutubu mipango ya kuifanya nafasi ya Katibu Mkuu iwe wazi.

Kisa nakijua. Ni Chongolo kukukwepa katika ziara zako mikoani. Ulitamani, ukasema na kuomba kuwa unataka ijirudie mikutano kama ile ya Kinana na Nape. Ukajiapiza kuharibu bila kutibu.

Umekuwa ukiwaambia wana-Sekretarieti kuwa muda si mrefu utawaongoza kwa ujumla wao (yaani utakuwa Katibu Mkuu). Hautaweza. Niko hapa Dar kuzuia hilo kwakuwa nilishajua na kuipata barua ya Chongolo ya kujiuzulu.

Katibu Mkuu atapendekezwa na Mama Samia na atapitishwa na chama, ila huwezi kuwa. Mama Samia, Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, hawezi kuichora picha ya kuogofya kirahisi kwa kukupendekeza. Ukae kwa kutulia.

Gekul, Chongolo mambo ni moto CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Naona umetoka pangoni baada ya mambo kuwa moto moto. Mambo ni fayaaa. Utadhani tupo Mei 2015 au 2025.
 
Utamzuia wewe kama nani ndani ya CCM!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 

Mpira kwako



Majibu yako tafadhali.
 
Duh...!.
P
 
Endeleeni kuparurana, ili watu wenye mapenzi mema na nchi hii wapate nafuu.
 
Makonda anafaa sana
 

Mzee wa kuleee! Nimeshajua kitu hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…