Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

99% ya ulivosema ndo yanatokea kwa mwanangu 4yrs.

Ila ana moja la ziada. Usiku akilala anasaga saana meno.
Hyo ndy mbaya watu hao siku ukikosana nao wana kuweka watch later list lazma waseme na wewe hat ipite miak mingapi yani atakupata tu.
 
Ulimpeleka mtoto kwa waganga,are you mentally fit?
 
Dah!
Pole sana.
Huyo mtoto anaonekana ana dalili za Usonji (Autism). Kuna mtaalamu fulani kwenye runinga aliwahi kutuchambulia hiyo hali.

Msaada hapo ni kumpeleka kwa madaktari bingwa wa watoto na wataalamu wa afya ya akili.

Note:
Usipoteze muda wala pesa zako kwa watu watakaojitokeza na kujifanya wanaweza kuondoa hiyo hali, kiuhalisia hiyo hali huwa ni ulemavu ubongo na mwili wa kudumu lakini kupitia msaada wa kidaktari inaweza kuboreshwa kwa kupunguza madhara ikiwemo mtoto kuweza kutulia, kukua, kuwasiliana na kuishi na jamii. Zaidi ya hapo usitegemee makubwa sana labla msaada wa imani ya miujiza.
 
Pole sana Kaka kwa Mwanao. Lakini sikiliza Madaktari wataalam.

Shida ya Mwanao sio Ndogo ni Kubwa.

Swala la kuongea sio issue sana lakini hizo tabia zingine alizo nazo zinafanya lionekane kubwa.

Nakushauri kwa sisi Madaktari wa Miti Shamba( bush doktas) usimleta tutakulia pesa zako bure.

Mpeleke kwa Paediatrician na Medical Psychologist angalau utapata unafuu wa namna ya ku cope naye.

Hiyo ni Autism haina Dawa.
 
😭
 
Mtoto inabidi aanze kukaa na kusimama akiwa na miezi mingapi maana wangu ana miezi mitatu ila hapendi kulala lala ana taka kusimama simama
Katika hali ya kawaida, mtoto
Miezi
0-1 analala tu bila kugeuka
1-2 anageuza kichwa/shingo
3-4 anakaza shingo
4-5 anakaa kwa kuegemea kitu
6-7 anakaa bila kuegemea kitu
7-8 anabilingita (rolling) akilala
9-10 anatambaa
11-12 anasimama
Kuanzia mwaka mmoja anaweza kutembea.

Nocte:
Wapo watoto wanaoweza kuwahi hatua fulani (hiyo haina maana kila hatua itawahi, kuna hatua atasimama zaidi bila kusonga mbele) au kuchelewa hatua fulani (hiyo haina maana hatua zote zitakazofuata atachelewa) kuna kitu wanaita growth compansation mechanism, mtoto mwenyewe anaweza kuifanya automatically au jamii ikaifanya kwa mtoto kwa kujua au kutokujua.

Lakini ikiwa mtoto atachelewa zaidi ya miezi mitatu kuvuka hatua inayotakiwa (kwa mfano ikiwa mtoto anatakiwa mpaka kufikia miezi 12 awe anaweza kusimama) halafu akafika mpaka mwaka mmoja na miezi mitatu hajaweza kusimama, hapo inabidi juhudi za haraka zifanyike, na ikiwa juhudi hizo zitafanyika bila kuzaa matunda basi inatoa picha mtoto atakuwa na tatizo kubwa ambalo litahitaji muda mrefu zaidi kutatuliwa kitaalamu.

Mwisho wapo watoto ambao wanawahi kusimama (kwa kushika kitu) wakiruka hatua ya kutambaa, hiyo haina maana kuwa mtoto atatembea bila kutambaa, kadri atakavyotaka kutembea mtoto atarudia kwanza kutambaa. Zoezi la kutambaa ndio zoezi muhimu na bora zaidi kumuandaa mtoto kuja kutembea vizuri siku akianza kusimama. Mpe mtoto muda na nafasi ya kutambaa kadri atakavyo, usimharakishe, siku akichoka kutambaa mwenyewe atatamani kusimama na kutembea.
 
Wewe...sio Doctor hizo Dalili za polio .....?

Rubish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…