Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Dawa zitapatikana as long as Watu bado wanafanya Studies nyingi ili kutuokoa kwenye hilo..
Inaitwa ASD (Autism spectrum disorder)
🤣🤣🤣🤣

Tumaini zuri kweli.

Ndio maana watu wepesi kiakili wanakimbilia kwa mwamposa, because the medical system is a CRAP.

Nyie madokta mnaishi kwenye boksi dogo sana.
 
Habari za majukumu ndugu zangu,Nina mtoto wa kiume miaka 4 Sasa lakini haongei ni kupiga makelele tu ana dalili hizi hapa chini
1. Ukimuita jina lake hageuki
2. Anapiga makelele tu
3.kuna wakati Anakuwa anaziba masikio
4. Anatamka sauti zinazojirudiarudia lkn hazieleweki
5. Anapenda kuning'iniza vitu mfano chaja za simu,waya,funguo,ama kitu chochote akishika yeye n kuning'iniza anaweza kutoka chumban na nguo ya ndani ya mamake akaja nayo sebuleni ananing'iniza ( anapenda sana hicho kitu)
6. Mikono yake kama imelegea hata kuanza kula mwenyewe alichelewa na saiv anakula mwenyewe Ila anasambaza chakula ukimpa wali maharage atakula 10% asilimia 90 utakuwa kasambaza chini
7. Anapigapiga kidevu chake
8. Anapenda vitu vyake tu ,
9. Hapendi kucheza na watoto wenzake anajitenga nao hata wakiwa 200 yeye atakaa pekeake anafanya vitu vyake
10. Ukimtuma kitu hawez kuleta maana hakuna kitu anaelewa
11. Kuna nywele zilinyolewa akiwa mchanga Hadi hazijaota. Sehem zingine znaota lakini hiyo sehem hazioto

Nilishampeleka Kwa waganga wanasema mizimu,kurogwa, hospital Wanasema usonji(Autism),maji ya mwamposa alishatumia ,Niko naendelea kutafuta tiba naomba mnisaidie Niko TAYARI kutoa MILION 5 CASH Kwa atakayenisaidia mtoto huyu kuongea. Naumia Kwa sababu ni mwanaume siwezi kuweka emoji za kulia. Naumia sana. Namba zangu ni 0689590080.
Pole sana mkuu Mwenyezi Mungu akupe Wepesi Kwa mitihani huu, Naamini Mwanetu atakaa sawa Inshallah
 
Pole sana mkuu.Mimi kijana wangu wa kiume yeye alichelewa kuongea pia mpaka.3 or 4yrs alikuwa hata kusema mama hasemi.Tukagundua tatizo ,pia akawa yeye ni kula na.kulala tu cha kushangaza aliyembea akiwa na miezi 9 na pia miezi 10 hivi hajikojolei na haja kubwa anatoa ngua anajisaidia chini.Mimi nakupa experience yangu mwenyewe.Nilipogundua hicho kitu ,mimi nilivyoona hospital hainisaidii nilimlilia Mungu usiku na mchana na kusoma Matayo 18:18 nafunga hayo.maroho ya stagnation
Uwezi amini kijana aliimprove darasani na kila kitu kwenye maisha yake .Na ni one of the best students in Tanzania ,mpaka nyumbani ananisaidia sana.Ushauri wangu ,mpeleke kwanza hospital mwone Dr akushauri.Pili fuata masharti yote ya kitabibu utakayoambiwa then ongea na Mungu wewe peke yako kuhusu huyo.mtotto.Shida huwa tunafikiri Mungu yuko mbali sana au yuko kwa wachungaji au mashehe tuko naye.Chunguza maisha yako ,mfano kama ulisha mtelekeza mtoto au kukataa mtoto au minba .Check maisha yenu kwa ujumla mtubu na kama ulikataa mtoto au unakitu ulimfanyia mtu kaombe msamaha ,tubu mwangukie Mungu ni mwaminifu.
Asante sana, sijawahi kukataa mimba Wala mtoto labda nifikirie dhambi zingine Niko tayari kutubu,sisi n binadamu tunawaza tofauti na mawazo ya Mungu
 
Usimkalishe kwanza mpaka miezi 5-6
Muda ukifika hua wanakaa wenyewe pamoja na kuanza kutambaa km yupo kwenye kitanda chake huanza hata kusimama mwenyewe mule mule ukifika muda wa kutembea huanza utundu wa kutaka kutoka utaona anaanza kupanda atoke kwenye kitanda kile usipokua makini atatoka ataanguka ataumia uangalizi unahitaji muda wote, kulea kulea kulea daah maisha haya
 
Hatoi udenda ,ila dalili zingine ni hizi
1. Hata baba Wala mama hawajui
2. Anachekacheka baadhi ya miezi
3. Hata ukimpungia mkono wa byebye kama watoto wengine hawez ku reply
4. Yuko busy muda wote hatulii sehem Moja
5. Jina lake halijui
 
Kwa Africa usonji ni ugonjwa ila ulaya wanajua namna ya kujua interest ya wasonji,
Ni watu ambao akili yao iko focused kwenye kitu kimoja tu,hivyo wanakuwa bora sana kwenye eneo lao,kazi ya mzazi ni kujua mtoto focus yake nini,kisha uweke nguvu zote hapo,
Usipojua basi itakuwa changamoto

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Yaan shida ni kama ana tatzo la ubongo,hafundishiki kitu.
 
Muwahishe hospital kama bado hajaanza matibabu,nakumbuka hii ni moja wapo wa dalili za mwanzo kabisa nilizokuwa naziona kwa mwanangu.

Hiyo ni degedege na wataalamu wanasema ndiyo huzidi kuuvuruga ubongo wa mtoto muwahishe kuna dawa atapewa zitamsaidia though umechelewa kidogo,kijana wangu nilimuanzishia matibabu pale MNH akiwa na miaka 2 yalimsaidia sana kwa kumuangalia mtu hawezi kumjua mpaka amuulize kitu ndiyo atagundua.
Hospital na kwa waganga kashaenda sana! Mungu atamsaidia
 
Hatoi udenda ,ila dalili zingine ni hizi
1. Hata baba Wala mama hawajui
2. Anachekacheka baadhi ya miezi
3. Hata ukimpungia mkono wa byebye kama watoto wengine hawez ku reply
4. Yuko busy muda wote hatulii sehem Moja
5. Jina lake halijui
Autism hiyo. Maombi na uwe na imani kweli kweli
 
Nahitaji msaada mtoto aongee
Keshaanza shule,ndio mtoto WA kwanza pekee hapo home.
Watoto uwahi kuongea wakiwa na wenzao mpeleke shule,wangu aliongea akiwa shule na miaka mitano sababu alikuwa pekee home hakuna watoto wengine
 
Naamini lkn pia Kuna nywele kichwani zlinyolewa isivyokawaida na huwa hazioti hiyo sehemu. Nisaidie namba ya huyo Dr pia,asante
Hapo ni ishu za kiimani inategemea mambo za Imani huwa unaegemea upande upi ndio msaada kwako.
 
Tafuta waonaji wenye uwezo wa kuona ya sirini watakiambia kama ana tatizo au ni utoto TU.
Wengine uchelewa kuongea tegemea na mazingira.
Mfano watoto wa uswahilini uwahi sana kuongea na kuwa wajanja mapema kuliko watoto wa geti Kali sababu ya zile vurugu za uswazi.
 
Back
Top Bottom