Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Pole sana kwa mitihani unayopitia. kujaribu tu, kuna maalim yupo Mkulanga kwa mwarabu (kituo kwa Mwarabu) wanamwita Malamba. Kabla kwenda na mtoto nenda mwenyewe Kwanza ukajue siku hizi utaratibu wake ukoje. huduma zake ni bure kabisa labda siku hizi iwe tofauti
Mitaani tuna watoto wengi wenye shida hii ambao kama wazazi wao wangekutana na watu sahihi kwa wakati sahihi leo wasingekuwa walivyo ila kwa sababu watu tumekuwa tukipeana shauri kama hizi za kufurahishana wanazidi kuengezeka.

Bro,malezi ya mtoto siyo kama gari kwamba utamwelekeza mmiliki kwa fundi fulani aliyewahi kukutengenezea gari lako,hilo ni tatizo na hii ni wide forum wote tumo humu tuliowahi kukutana na shida hiyo huyu mtoto ana tatizo hahitaji maalimu shehe wala pasta mtoto anatakiwa kukutana na Dr wa watoto that's it.

Japo wazo lako limesomwa.
 
Sema na Mungu kuhusu mtoto wako atakujibu tu,na kama unaishi uswahilini kuna mambo mengi sana ya hovyo inawezekana ni kweli wamemchezea,mtoto ni kitu very special kwa binadamu,pata ushauri wa kitabibu lakini katika kila jambo mshirikishe Mungu.Ukishaamua kuzaa maisha mengine ya hovyo hovyo achana nayo,hicho ndio kizazi chako, you have to be very serious at this moment,kuwa karibu na Mungu,kila kitu kitakaa sawa na utafurahia maisha yako...
 
Mleta mada umeweka tangazo pale juu kutoa Tsh 5mill cash kwa atakayemfanya mtoto awe na makuzi ya kawaida,hili jambo halihitaji muujiza hata kidogo.

Epuka matapeli,mtoto ana shida ambazo wengine tumeshazipitia na hela zetu kama ulizo nazo wewe hazikuwahi kusaidia chochote zaidi ya kugombana na watu hizo hela zako mfungulie mtoto Jr account zitamsaidia baadae wewe mchukue mpeleke hospital kwa wataalamu utakuwa umefanya kitu sahihi uje hapa kushukuru.

Makuzi ya mtoto hayana short cut chochote kwa mtoto ni hatua kwa hatua akiwa na shida nayo ni hatua kwa hatua ukitaka ku-solve chochote kwa mtoto hizi kanuni zizingatiwe.
 
Amekwambia kashampeleka kwa Mwamposa kamnywesha na kummwagia maji na mafuta sana Ila wapi Ngoma ngumu mpaka kanyoosha mikono juu Mwamposa kashindwa sasa unataka kusemaje apuyange kila sehemu za wachungaji manabii na mitume kupigwa Hela za maji na mafuta?

Mimi nimshauri tu, ampeleke kwa sheikh akasomewe, kwa uwezo wake Allah mtoto atakua sawa, kwa kina mwamposa atapoteza muda wake na pesa zitamtoka
 
Asante,Niko TAYARI kufanya lolote mwanangu aongee Jana nmetoka Kwa mganga nikamwambia hata akitaka mkono wangu Nampa ili tu mwanangu aongee hata akitaka nilete chochote including uhai wangu Niko tyr
Mmh. Uko serious kweli Mkuu?

Huu ni muda wa wewe kusimama kama baba ili mtoto akae sawa ukisema hadi ikibidi kutoa uhai wako inashangaza.
 
Haongei hata umuongeleshe ataishia kukuangalia km kitu TU yaan km wewe unavyoiangalia smartphone hapo ukiiongelesha inaongea?
Kuna mtu kasema ubongo wake una kuwa taratibu, so wewe ukisema hawezi ni kwamba anaweza ukilinganisha na kuelewa wako.
Ukiwa unaongea naye mtazamane usoni na uongee NENO Hilo Hilo kwa same posi. Na Hilo NENO tamka taratibu, mfano unaweza ukasema NENO mma akiwa anakunywa maji. Kila unapompa maji unatamka mma. Liajengaka slow slow kwa brain.

Fanya mfano wa wewe kusikia na kuongea kingereza. Zile changamoto unazopitia Nia na matokea ya kile unachoongea vinakuwa tofauti.

Amini tu ataongea. Usimkatie tamaa. Na usimtangulie hela kwa watu unapotaka msaada. Mwamini Mungu kweli kweli
 
Duuh mpaka kwa wagangaa ushampelekaaa..pole sana mambo ya watoto magumu sanaa.
Yaani nakwambia Jana nmetoka Kwa mganga nikamwambia Niko hata akitaka mkono wangu Nampa hapohapo,hata akitaka kichwa au damu ya mtu namletea maana nmechanganyikiwa. Mtoto anacheka mwenyewe na ana nguvu kuliko kawaida. Hili la KUCHEKACHEKA mwenyewe ndio linanifanya mwanaume nalia bila kupigwa. Nashukuru wanaonifuata DM na wasapu
 
Habari za majukumu ndugu zangu,Nina mtoto wa kiume miaka 4 Sasa lakini haongei ni kupiga makelele tu ana dalili hizi hapa chini
1. Ukimuita jina lake hageuki
2. Anapiga makelele tu
3.kuna wakati Anakuwa anaziba masikio
4. Anatamka sauti zinazojirudiarudia lkn hazieleweki
5. Anapenda kuning'iniza vitu mfano chaja za simu,waya,funguo,ama kitu chochote akishika yeye n kuning'iniza anaweza kutoka chumban na nguo ya ndani ya mamake akaja nayo sebuleni ananing'iniza ( anapenda sana hicho kitu)
6. Mikono yake kama imelegea hata kuanza kula mwenyewe alichelewa na saiv anakula mwenyewe Ila anasambaza chakula ukimpa wali maharage atakula 10% asilimia 90 utakuwa kasambaza chini
7. Anapigapiga kidevu chake
8. Anapenda vitu vyake tu ,
9. Hapendi kucheza na watoto wenzake anajitenga nao hata wakiwa 200 yeye atakaa pekeake anafanya vitu vyake
10. Ukimtuma kitu hawez kuleta maana hakuna kitu anaelewa
11. Kuna nywele zilinyolewa akiwa mchanga Hadi hazijaota. Sehem zingine znaota lakini hiyo sehem hazioto

Nilishampeleka Kwa waganga wanasema mizimu,kurogwa, hospital Wanasema usonji(Autism),maji ya mwamposa alishatumia ,Niko naendelea kutafuta tiba naomba mnisaidie Niko TAYARI kutoa MILION 5 CASH Kwa atakayenisaidia mtoto huyu kuongea. Naumia Kwa sababu ni mwanaume siwezi kuweka emoji za kulia. Naumia sana. Namba zangu ni 0689590080.

Acha kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Mpeleke kwa Sheikh akamsomewe, kwa uwezo wake Allah atakua sawa, na achana na hao waganga mara sijui kina mwamposa utapoteza pesa
 
Kuna mtu kasema ubongo wake una kuwa taratibu, so wewe ukisema hawezi ni kwamba anaweza ukilinganisha na kuelewa wako.
Ukiwa unaongea naye mtazamane usoni na uongee NENO Hilo Hilo kwa same posi. Na Hilo NENO tamka taratibu, mfano unaweza ukasema NENO mma akiwa anakunywa maji. Kila unapompa maji unatamka mma. Liajengaka slow slow kwa brain.

Fanya mfano wa wewe kusikia na kuongea kingereza. Zile changamoto unazopitia Nia na matokea ya kile unachoongea vinakuwa tofauti.

Amini tu ataongea. Usimkatie tamaa. Na usimtangulie hela kwa watu unapotaka msaada. Mwamini Mungu kweli kweli
Asante sana Kwa ushauri ndugu yangu Mungu akubariki, nmechanganyikiwa
 
Ana dalili zote za USONJI...Ila kuna mambo ya giza pia yanamwandama mtoto...mbane mama yake muulize ameshapita wapi na wapi...wamama wanafanya mambo mengi kuliko sisi wabaca.
 
Back
Top Bottom