Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

doz ya mayai, vichwa vya samak wabichi, maziwa mabichi, mboga za majani, karanga na maharage. Yani kifupi apate protein ya kutosha
Hapo kwenye vichwa vya samaki wabichi ataambulia minyoo na parasites.

Hizo zingine ni sawa.
 
Anadalili za ububu

Ana dalili za polio

Ana dalili za mental retardation

Ana dalili za teratogenic conditions (fatilia kipindi cha mimba mama yake alikuwa anapenda kutumia vilevi au vyakula gan)

Wakat anazaliwa alilia? Na kama alilia alitumia muda gan Toka azaliwe mpka kulia?

Muanzishie doz ya mayai, vichwa vya samak wabichi, maziwa mabichi, mboga za majani, karanga na maharage. Yani kifupi apate protein ya kutosha
Hii unaweza kuwa huduma ya kwanza. Huduma ya pili wawe wanamwongelesha
 
Mpeleke hospitali aonane na daktari wa watoto (utapata specialist anayefaa kumsaidia), sio tabia bali ana tatizo. mkiwahi mtamsaidia kupona mengi, kuwa tayari itakuwa kitu na matibabu na mengi kwa muda mrefu. Labda ana autism etc hivyo wahi akiwaangali mdogo, na pia mmechelewa kumpatia huduma. All the best
 
Acheni ujinga aisee. Yan eti anapenda hicho kitu cha kuning’iniza nguo ya mama ake ya ndani anakuja nayo sebuleni? 😂😂😂

Mkuu uko serious? Kwamba huyo mke hajui kutunza vitu? Kyupi mnawekaje sehemu zinapoonekana na mtoto?
Depal kwani chupi ina siri gani mpaka ifichwefichwe?
 
Usonji huo
Habari za majukumu ndugu zangu,Nina mtoto wa kiume miaka 4 Sasa lakini haongei ni kupiga makelele tu ana dalili hizi hapa chini
1. Ukimuita jina lake hageuki
2. Anapiga makelele tu
3.kuna wakati Anakuwa anaziba masikio
4. Anatamka sauti zinazojirudiarudia lkn hazieleweki
5. Anapenda kuning'iniza vitu mfano chaja za simu,waya,funguo,ama kitu chochote akishika yeye n kuning'iniza anaweza kutoka chumban na nguo ya ndani ya mamake akaja nayo sebuleni ananing'iniza ( anapenda sana hicho kitu)
6. Mikono yake kama imelegea hata kuanza kula mwenyewe alichelewa na saiv anakula mwenyewe Ila anasambaza chakula ukimpa wali maharage atakula 10% asilimia 90 utakuwa kasambaza chini
7. Anapigapiga kidevu chake
8. Anapenda vitu vyake tu ,
9. Hapendi kucheza na watoto wenzake anajitenga nao hata wakiwa 200 yeye atakaa pekeake anafanya vitu vyake
10. Ukimtuma kitu hawez kuleta maana hakuna kitu anaelewa
11. Kuna nywele zilinyolewa akiwa mchanga Hadi hazijaota. Sehem zingine znaota lakini hiyo sehem hazioto

Nilishampeleka Kwa waganga wanasema mizimu,kurogwa, hospital Wanasema usonji(Autism),maji ya mwamposa alishatumia ,Niko naendelea kutafuta tiba naomba mnisaidie Niko TAYARI kutoa MILION 5 CASH Kwa atakayenisaidia mtoto huyu kuongea. Naumia Kwa sababu ni mwanaume siwezi kuweka emoji za kulia. Naumia sana. Namba zangu ni 0689590080.
 
Kwa umri wa miaka 4 bado ni mapema mno kumkatia tamaa! Sema amechelewa tu.
Ushauri wa kwanza nenda kwa specialist wa watoto ajue ni tatizo gani kitaalamu linamsumbua!
Mwisho usiende kwa Waganga wa kienyeji au wapunga pepo watakula pesa yako bure!
 
Pole sana mkuu. Nayajua hayo maumivu maana hata mimi nilishaleta uzi humu kwa hali ya mwanangu inayoelekeana na ya mwanao. Mwenyeji Mungu akakufanyieni wepesi.
Poleni sana
 
Daaah pole sana hata Mimi Kuna wakati anasaga meno na anachelewa kulala sana anaweza kulala saa tisa na Kuna wakati anacheka pekeake
Hilo linaitwa 'Degedege' (au tuseme 'Kifafa' ambayo husabanishwa na Degedege) mkuu na hio ni hali yao hua wanakua nayo mpaka ukubwani Ila kadri wanavyokua na msaada wa Dawa za matibabu hua hali inapungua Ila atakua nayo mpaka ukubwani

Visababishi:

Kuwa na joto la kiwango cha juu (zaidi ya selsiasi 38)

Pengine kama mtoto aliumia ubongo wakati akiwa bado tumboni

Au kama alikosa oksijeni wakati mama anajifungua. Na hali hii inaweza baadaye kugeuka na kuwa 'kifafa'

Alipata maambukizi yakaingia kwenye ubongo, mfano, kupata ajali.
 
Hilo nitatizo la usonji. Atakuwa hapendi makelele kwasababu anasikia kwa kiwango kikibwa kuliko kawaida. Anaweza kuwa mahiri kwenye Jambo Fulani Ila kuongea na kutulia Hilo nijambo gumu
 
Back
Top Bottom