Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Pole sana nazani Shuleni katika kucheza na wenzie au mtaani kuna kitu cha ncha kali alichangia na mtoto ambaye ameathirika na VVU. Hawa watoto tunaawaacha wqcheze na wenzao lakini hatujui afya za marafiki wanacheza nao
 
sijaongelea mke wake, nmeongelea DNA ya Baba na huyo mtoto...kwani mke hawezi shiriki na dume gonjwa akapata ujauzito? alafu mama akabaki kuwa mzima...mtoto akaathiriwa?. Afanye hilo km ataweza maana kuishi na mwanamke kunahitaji akili ya ziada
Mkuu ww hujui sayansi kabisa. Mtoto hawezi zaliwa na HIV kamwe kama mama hana HIV.
 
Hivi vitu vyenye ncha kali vikitumika Na mtu ambae ni + alafu kikakaa labda hata masaa mawili je mtu ambae sio + akitumia anaweza pata maambukizi?

Napata mashaka sana na hizi vifaa vya masaloon jamani tutapona kweli?
 
Pole sana mkuu,
 
Umeeleza vyema sana mkuu. Umeeleweka. Watoto kwasasa wapo ktk mazingira hatarishi sana kuliko enzi zetu tulivokuwa watoto.
 
Mkuu hili la route yake inaweza kuwa sababu.

Sasahivi watoto wengi wanaishi na VVU.
pole sana mkuu,samahani kwa swali hili au maoni haya nitakayo yatoa

huyo mtoto ni wa miaka 9 kama kafanya ngono ndio kwanza atakua ameanza muda mfupi uliopita,je kuna uwezekano ukampeleka kwa daktari kujua kama ana bikra?kwani si mtoto wa kike huyo au nimesoma vibaya?

ukijua hana bikra unaweza pata pakunzia atakuambia tu nani kamtoa,hapo utaanza ku deal na huyo mtu,ikiwepo kumfunga kabisa maana mtoto lazima atataja tu,na kwa umri huo hawezi kua katembea na watu wengi kama kaanza ngono

pole sana mkuu kwa huo mkasa,kama bikra ipo basi itakua kwenye michezo ya watoto,saloon,vitu vyenye ncha kali wanavyozea

hata hivyo mpaka ukimwi umeanza kuonekana inaashiria aliambukizwa si chini ya miezi sita iliyopita japo inategemea na kinga yake ipoje

kaa nae chini akuelezee vizuri ni mwanao tena mdogo hawezi kukushinda,kama hana bk utapata pazuri pakuanzia
 
Kingine HIV ni mdudu, je walimuona, uliza swali hili kwa hao walimpima, na sio kufanya kukisia maana mpaka sasa hakuna vipimo vya kumuonesha huyo mdudu kama ilivyo typhoid au malaria.
We ukipimwa mafua/influenza wanayaona?
 
Mkuu hili la route yake inaweza kuwa sababu.

Sasahivi watoto wengi wanaishi na VVU.
Mkuu nimewahi kufanya kazi ya kuhudumia nyumba za hawa watu. Maambukizi yana njia za ajabu nyingi. Labda shule alikuwa na kucha ndefu wakati wa ukaguzi akachukua wembe wa rafiki yake akakatia kucha.
 
Pole sana ndugu.aanze matibabu mapema ata survive tu
 
Jamani wenye watoto wa kike tuwafuatilie kwa karibu nyendo zao
 
Mkuu una uhakika?hebu ongezea maneno hapo
 
daaah kuna vitu vinaumiza jamani, lakin ukimtunza vizuri ataishi maisha marefu na tiba zipo jirani, Mungu aibariki familia yako.
 
Mkuu uwe unajitahidi kusoma mada na kuelewa. Ulichoongelea kipo kwenye mada tayari, unaharakia nini??
 
nasemea kule hospital watoto kubadilishiwa wazazi au kuibiwa kabisa hizi kesi zipo hujawahi sikia hizoa....kwakuwa unasema mmefanana isivyokawaida basi sawa tupo pamoja.

itabidi uwekeze muda ktk kuchunguza hili swala la route zake

pole sana ndugu
 
This is very sad brother.

Issue zinazohusu watoto huwa very very sad.

Mungu akujaalie wepesi na familia yako.

The best you can do is stay strong for her. If you are weak, she will lose strength... and without strength and faith her perspective towards life and aurvival will be full of negative energy which is the last thing she needs.

She is still a child. She needs to enjoy her childhood without stigma, without having fingers pointed at her or being alienated and to achieve this you need to keep it secret, not out of shame but to protect her from all that.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…