Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Umenikumbusha jambo baya sana, Siku ka binti kangu nilikakuta kanachezea surgical/examination gloves! Nilijisikia vibaya sana tena alikuwa anapuliza kama puto!
Duh! Mungu atulindie tu hawa watoto wetu maana bila yeye ni ngumu sana kulifanikisha hili.
 
Pole mno mkuu, hakika niko katika viatu vyako naona jinsi unachomeka. Kwa kuwa mtoto ameanza kuugua jua kabisa hakapata virusi siku za karibuni. Atakuwa amepata nyuma kidogo kama immune yake ni nzuri. Kwa misingi hii ni ngumu sana kuweza ku trace chanzo ila kwa harakaharaka unaweza suspect yafuatayo:

i. Shuleni anakosoma kama kuna mtoto mwathirika na akawa say kuna contamination yoyote mtoto anaweza kuambukizwa.

ii. Watoto wa siku hizi kwa miaka tisa pia kuna utundu shuleni, imagine kama kuna uwezekano huo kuwa anaweza say kufanya kissing na mwenzie kumbe ana michubuko na kuambukizwa.

iii. Kuna incidence za ndugu au watumishi wa ndani ambao kama mkikosana na akiwa ni victim basi huwa anaweza kutumia miswaki ya watoto na kuacha traces za virusi hivyo ni rahisi mtoto kuambukizwa.

Cha msingi ni ngumu kupata chanzo sasa focus namna ya kumpatia tiba na matunzo mtoto wako. Jipe moyo ataendelea vizuri na ninaamini itapatikana dawa. Mungu akupe nguvu ya kustahimili yote haya.

Pole nyingi mno. Nimeumia sana
 
Ukiona jambo lolote limetokea ambalo sio la kawaida sana kwa binadamu, aidha liwe jema au baya, ujue Mwenyezi Mungu keshasaini...
 
Pole sana mkuu. Inawezekana ni katika michezo ya watoto maana huwa wanapenda kuokota vitu vyenye ncha kali na kuvichezea. Kwa upande wangu binti yangu alishawahi kufanya kitu cha hatari sana akiwa shule alitoa heleni na kuitumia kutobolea masikio ya wenzie pia na yeye kujitoboa tena. Kiukweli nilikosa amani mwezi mzima nilikosa ujasili wa kwenda kumpima. Lakini kikubwa kwa sasa fanya yale unayotakiwa kufanya kwa mgonjwa
 
Anaweza kuwa aliambukizwa wakati wa kujifungua na ma dr. Ama mtotk huyo sio wako walikubadilishia wakati amezaliwa
 
Dooh, pole sana Mkuu, dunia ina mengi, mtoto hana mipaka ya kutengamana na wenzake,kwa hiyo possibility ni ametoa kwa watoto wenzake, hususan kushea vitu
 
Pole, watoto wanachangia vitu vingi sana wawapo nje ya mazingira ya nyumbani
 
hii itakuwa biashara kama zingine tuu
 
Pole sana! Maambukizi yanaweza tokea hata kwa vitu vyenye incha Kali!
 
Hakika watoto wapo hatarini! Umenikumbusha jambo kubwa sana! Watoto hata kushirikiana heleni haifai kabisa. Kwa bahati mbaya katika kucheza watoto wanaweza badilishana hata heleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…