Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Siku hizi watoto wadogo wengi sana wapo HIV positive. Na baahati mbaya katika michezo kuna vitu vyenye ncha kali watoto wamekuwa wakichezea na kushirikiana hususani nyembe za kuchongea penseli na nail cutter. Pia ktk kucheza pamoja endapo wana vidonda ni rahisi sana kuambukizana kama mmoja ni HIV+. Kuna mtoto wa shemeji yangu wife alimkuta anashika shika vidonda vya mwenzake ambaye inasemekana ni HIV+. Kwa mazingira kama haya watoto ni rahisi sana kuambukizwa HIV. Hili ni fundisho kuwa tusipende kuwadhania vibaya wenye HIV, wapo wengi wana HIV na hawakupata kwa njia ya uzinzi.

Nakupa scenario ya nyingine; Dada yangu ana ugonjwa wa sukari, kwa hiyo hujipima sukari kila siku na kujichoma sindano. Siku moja katoto kangu kakasema nako kanataka kupima, akakachoma na kukapima. Binafsi hadi leo huwa sielewi dada alitumia sindano mpya kumchoma mwanangu au alitumia aliyotumia yeye kujichoma? Kwa mfano huu nadhani unaweza kuona ni kiasi gani watoto wetu wapo katika mazingira ya hatari wawapo nyumbani na hata shuleni.

Pole sana mkuu, mwenyezi MUNGU awape nguvu. HIV kaipata shule au hapo hapo nyumbani kwa watoto anaoshinda nao na most likely ni vitu vye ncha kali. Kama unatabia ya kuwapeleka wanao kwa kinyozi kunyoa, tafadhali hakikisha hawachongwi. Ktk kuchonga mara nyingi mashine zile huwa zinakata au kukwangua, imagine mashine imetoka kumnyoa mtu mwenye vidonda halafu ije imkwangue mwanao?
Mkuu hapo kwenywe mashine za kunyolea wengi hatuchukui tahadhari. Tena hapo kuna hatari ya maambukizi ya homa ya ini (herpatitis).
Ni vema umekumbushia hili suala.
Mimi nina mashine za kunyolea home sipeleki watoto salon.
 
Ndugu pole sana, lakini kwa sasa hali inaweza ikawa mbaya kwa sababu kuna watoto wanazaliwa wakiwa positive+, transmission from mother to child. Hawa watoto wanaenda kusoma shuleni na watoto wengine, ni vigumu sana kuwatambua na hakuna shule yao peke yao so lazima wewe mixed na watoto wengine. Watoto Hawa wanacheza na kufanya shughuli mbalimbali shuleni pamoja. So possibly inaweza kuwa mtaani au shuleni huko.
kweli chief ""
 
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Lord have Mercy!

Binti ana umri gani mkuu?

Jipe moyo, mpe lishe nzuri, aanze dawa za kupunguza makali.... Naamini muda si mrefu dawa itapatikana na binti yetu atapona.
 
Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.
Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?
Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Pole sana kwa tatizo lililokupata!..
Lakini nimewaza hao wanafamilia walipima kwa hiari specialy msichana wa kazi. Unajua kupima kwa shurti ukimwi sizani hata mahakama inaweza toa amri hiyo!.
 
Aisee, mbali na njia ya kujamiiana, UKIMWI unapatikana kwa blood contact na damu yenye virus.
Pengine saluni au huko shuleni ama mtaani ktk michezo na watoto wenzake aliumia ndio ikawa chanzo cha kuambukizwa na mwenzie ambaye ni +.

Inasikitisha [emoji17] [emoji17]
Most likely... Mungu awanusuru wanetu kwakweli...

Dah!
 
Dah[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]

Pole kaka inaumiza mno
 
Pole sana mkuu ila nina wasi wasi kwenye majibu kama aliwai kufanya mapenzi au lah...
Watoto wa siku hizi wana ingia kwenye ngono mapema sana.....
Huyo ni wazi aliupata kwa ngono.....
Mpeleke aka anzishiwe dawa mapema japo kama alichelewa....

Siyo lazima ngono. Watoto wanaweza kuwa wamecheza na viwembe au sindano. Siku hizi kuna watoto wengi waliozaliwa na virusi vya ukimwi mashuleni na mitaani ambao huwezi kuwafahamu... katika michezo yao wanaweza kuumia na kuambukizana bila kujua.

Tumwombe Mungu apitishe mbali haya majanga.
 
Dah..pole sana Mkuu..ndio mitihani ya kidunia..
 
Mpeleke maombi pia afanyiwe caseli atasema tu wale ni watalam watamshawi atasema tu
 
Pole sana mkuu,muwahishe hospitali kubwa ili uweze kuona kama cd4 zake zimeshuka kiasi kikubwa ili aanze kutumia ARVs...
 
pole sana....nenda jukwaa la jf doctor "" katafute Uzi unaoitwa "" je unaweza kutembea na mtu aliyeathirika lakini usipate maambukizi.....utapata majibu yote huko """tena nivizuri zaidi kama mods wakiuhamishia huu Uzi wako huko
Mtoto kapimwa hajawahi kuingiliwa kimwili... bado fumbo,
KAUPATA WAPI???
 
Back
Top Bottom