Leo aubuhi nimefuatilia shindano la Olympic kule Paris la mbio ndefu ya kilomita 42 na mwanariadha Ndugu Simbu akiwa mshiriki toka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kweli matokeo yake hayakuwa mazuri kwa kushika nambari 17 akitumia saa 2:10: 03
katika mbio hizo. Pole sana. Rudi nyumbani ukaendelee na mazoezi tena.
Matumaini ya Tanzania kuambulia chochote yapo kwa kinadada Jackline Sakilu na Magdalena Shauri ambao watatupa karata za mwisho za Tanzania katika mbio za Marathon kwa Wanawake ambazo ndio zitakuwa zinahitimisha rasmi Paris 2024.
Soma Pia: Wanariadha wa 4 kutuwakilisha kwenye mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa Mwezi Julai, Kambi kuwekwa Arusha
Katika matokeo mengine.
Tola Tamirat wa Ethiopia ndiye mshindi wa kwanza akinyakua medali ya dhahabu akiwa na rekodi mpya ya Olimpiki ya saa 2:06:26 huku nguli wa Kenya Eliud Kipchoge akishindwa kutetea taji lake.
Tola aliingia katika mbio za marathon za Olimpiki kama mchezaji wa akiba wiki mbili zilizopita, akijaza nafasi ya mchezaji mwenzake aliyejeruhiwa.
Bashir Abdi wa Ubelgiji alinyakua medali ya shaba kwa saa 2:06:47, huku Mkenya Benson Kipruto akitwaa shaba (2:07:00).