Mwanariadha Alphonce Simbu amaliza nafasi ya 17 Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa

Mwanariadha Alphonce Simbu amaliza nafasi ya 17 Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa

d36c0fea-3c69-479b-8551-f1ee4d67f262.jpeg


Tanzania imeshindwa vibaya kwenye mashindano ya mbio za Marathon za Olimpiki Paris 2024 baada ya tegemeo lake kuu Alphonce Simbu kumaliza nafasi ya 17 akitumia saa 2:10: 03

Geay, akiwa katika nafasi ya 74, ni mmoja wa wakimbiaji 11 ambao hawakumaliza hadi Mwisho.

Matumaini ya Tanzania kuambulia chochote sasa yamebaki kwa kinadada Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri ambao kesho watatupa karata zao mwisho katika mbio za Marathon kwa Wanawake ambazo ndio zitakuwa zinahitimisha rasmi michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Sakilu na Shauri wataingia barabarani kuanzia saa 3 za asubuhi kwa saa za Tanzania.

Katika mchuano wa Marathon kwa wanaume leo, mshindi alikuwa Tola Tamirat wa Ethiopia akinyakua medali ya dhahabu akiweka pia rekodi mpya ya Olimpiki ya saa 2:06:26 huku nguli wa Kenya Eliud Kipchoge akishindwa kutetea taji lake, baada ya kushindwa kumaliza mbio hizo.

Tola aliingia katika mbio za marathon za Olimpiki kama mchezaji wa akiba wiki mbili zilizopita, akijaza nafasi ya mchezaji mwenzake wa Ethiopia aliyejeruhiwa.

Bashir Abdi wa Ubelgiji alimaliza wa pili na kunyakua medali ya fedha kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:06:47, huku Mkenya Benson Kipruto akiwa wa tatu na kutwaa medali ya shaba kwa kutumia saa 2:07:00.
 
Serikali ipi, upo usingizini ?
Hii iliyowekeza kwenye Vx LX 200 series?
Maana yangu ilikuwa..aliyesema mbio ndefu na fupi ni kwa watu kutoka US, Kenya, Ethiopia..au cushites na nilotic si kweli sababu Tebogo Letsilie ameshinda fainali Olympic mita 200 wanaume anatoka Botswana..hivyo cha muhimu ni serikali kuwa na malengo na kuwekeza kwenye riadha..watapatikana wakimbiaji wengi na watashinda.
 
Simbu angeenda zile mbio za mule uwanjani labda angepata kitu speed yake sio mbaya ila mi naona walienda ushahidi tena wote Saba walienda ushahidi ila zile mambo hawawezi
 
Waandae mashindano yanayoanza na kwanza kabisa napenda kumshukuru... Hapo tutaongoza
 
Si mnasemaga wakimbiaji wazuri wanatoka Arusha na Manyara? Sisi HUKU mbeya tunaendelea KULA maparachichi huku tunacheka kwa chini chini yaani Hadi kurusha tufe mlitutenga kamati ya Olimpiki mmevuna ubaguzi wenu.

VIONGOZI WALIKUWA wengi KULIKO wachezaji kkkkkkkk!
 
Kumbe ulikuwa na matumaini kabisa? Ili hali washindani hata hawaiwazii Tz. Kwa sikitiko lako, yawezekana ni mnufaika na Olympic, na sasa upo Paris
 
Kumbe ulikuwa na matumaini kabisa? Ili hali washindani hata hawaiwazii Tz. Kwa sikitiko lako, yawezekana ni mnufaika na Olympic, na sasa upo Paris
Maandalizi hafifu, pesa zinazotolewa kwa maandalizi vimeliwa na Henry Tandau na Filbert Bayi na TOC kwa ujumla
 
Walienda huko wakiamini watashindwa!
Maadamu wanalipwa per diem haina shida!
Angalau wameliona jiji la Paris!
 
Hao kila siku wao wanajiandaa
Sisi olympic kesho kutwa leo tunaanza mazoezi

Ova
Mimi naona ni hivyo wabongo hatuna discipline kwenye mazoezi na hatuna consistency.

Mimi nahisi mtu akijitolea kwenye mbio akajidedicate kabisa kwamba do or die basi anatusua.

Kinchotakiwa ni nidhamu ya lishe,mapumziko,na training za kimkakati zitakazmsaidia mwanariadha kukimbia vyema na kwa ustadi.

MBali na hapo kibongobongo tunakosa usimamizi wa mtu binafsi mwenyewe ama wafundishaji hawawazi nj ya box na kuzingatia miiko.

MTu anakimbia mazoezi siku annavyojisikia alafu anataka kwenda kushindana
 
Back
Top Bottom