Mwanariadha Alphonce Simbu amaliza nafasi ya 17 Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa

Mwanariadha Alphonce Simbu amaliza nafasi ya 17 Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa

Alphonce Simbu amefunguka baada ya kumaliza nafasi ya 17 mbio za Marathoni Jijini Paris, Ufaransa akitumia saa 2:10: 03.

Matumaini ya Tanzania kuambulia chochote yapo kwa kinadada Jackline Sakilu na Magdalena Shauri ambao watatupa karata za mwisho za Tanzania katika mbio za Marathon kwa Wanawake ambazo ndio zitakuwa zinahitimisha rasmi Paris 2024.

Tola Tamirat wa Ethiopia ndiye mshindi wa kwanza akinyakua medali ya dhahabu akiwa na rekodi mpya ya Olimpiki ya saa 2:06:26 huku nguli wa Kenya Eliud Kipchoge akishindwa kutetea taji lake.

Tola aliingia katika mbio za marathon za Olimpiki kama mchezaji wa akiba wiki mbili zilizopita, akijaza nafasi ya mchezaji mwenzake aliyejeruhiwa.

Bashir Abdi wa Ubelgiji alinyakua medali ya shaba kwa saa 2:06:47, huku Mkenya Benson Kipruto akitwaa shaba (2:07:00).
 
Wale vijana wa harakati sijui wanaitwa nani nani brothers si huku nako ndiko wangezoa medali? Au wao hawaruhusiwi?
 
Nashukuru ameshindwa mana pongezi zingeenda kwa mtu ambaye sio sahihi na mikelele kibao
 
Tanzania kutokuwa na uwakilishi unaolingana na umri wa nchi toka kupata uhuru, idadi na ukubwa wa nchi kwenye michezo mikubwa km Olympics ni kielelezo kuwa tuna taifa Mfu! na serikali yenye dhamana ya uongozi kwenye mambo yote yanayolipatia taifa sifa, kuheshimiwa, mapato, marafiki haijui ilifanyalo na haijui inakoelekea! Mpira wenyewe hakuna popote umelifikisha taifa! Mpira wa mdomoni..kila mtu ni mchambuzi na afisa habari wa kujitakia kwa timu anayopenda..Eti nchi tunapeleka waogeleaji Olympics..r we serious? tumeshindwa kujua potential yetu iko kwenye michezo gani..? Nchi km Botswana ina watu million 3 tu tunawazidi mara 20, wmefanya homework yao vzr wamejipata, leo wanashiriki Olympics na kushinda medali! Michezo siyo futbal peke yake, na watu wa dar es salaam wanapaswa wafahamu jambo hili! Miaka ya 70, 80 na 90 nchi hii ilikuwa bora sana kimataifa kwenye riadha na netball..sijui ni wapumbavu gani waliingia na kuhamisha attention kwenye netball na riadha ikaenda kwenye uigizaji na u-miss! It's terrible! Tumekuwa km taifa lote tuna asili ya Pwani..maneno meeengi..na ushabiki wa kijinga! Leo tunashindwa na Burundi..kweli?? Nini tumebaki nacho sasa..ignorance na usimba na uyanga..???nini taifa linapata?? nguvu nyingi kwenye mambo nonsense kabisa km simba au yanga day..na media yetu ndio inaua mambo mazuri na kupandikiza ujinga kwa wananchi..!
TUJIREKEBISHE!
 
Jamaicans, US, Ethiopians and Kenyans ni undisputed runners mbio ndefu kwa fupi. Nilotics na Cushites ni long distance-runners.
 
USA wamejipanga sana kwenye hayo mambio mbio... Kenya na Ethiopia wanafuata
mbio fupi USA masafa marefu mashariki mwa afrika Ethiopia na kenya tanzania bado usimba na uyanga mwanga atuweki vipaumbele kwenye michezo mingine ambayo labda ingeweza kutuweka kwenye raman
 
Jamaicans, US, Ethiopians and Kenyans ni undisputed runners mbio ndefu kwa fupi. Nilotics na Cushites ni long distance-runners.
lakini Letsile Tebogo si mmoja wa hao uliowataja na ameshinda mita 200.. ni focus, committment ya serikali zinatengeneza watu km hawa!
 
Back
Top Bottom