Kweli kabisaMimi naona ni hivyo wabongo hatuna discipline kwenye mazoezi na hatuna consistency.
Mimi nahisi mtu akijitolea kwenye mbio akajidedicate kabisa kwamba do or die basi anatusua.
Kinchotakiwa ni nidhamu ya lishe,mapumziko,na training za kimkakati zitakazmsaidia mwanariadha kukimbia vyema na kwa ustadi.
MBali na hapo kibongobongo tunakosa usimamizi wa mtu binafsi mwenyewe ama wafundishaji hawawazi nj ya box na kuzingatia miiko.
MTu anakimbia mazoezi siku annavyojisikia alafu anataka kwenda kushindana
Uko sahihi kabisa.Sisi tunaongoza kwenye mbio za uchawa.
Hao wengine je wanawaandaHuyu kila siku n wa kushindwa tu hiv hamnaga wengine
Bashir Abdi ndio wa pili ni msomaliWa kwanza toka Ethiopia na wa pili toka Kenya.
Mkuu unadhani kwa mwanariadha anatakiwa afanye nini yeye binafsi ili awe mkimbiaji bora wa mbio ndefu tukiachia juhudi za mamlaka ?Tanzania kutokuwa na uwakilishi unaolingana na umri wa nchi toka kupata uhuru, idadi na ukubwa wa nchi kwenye michezo mikubwa km Olympics ni kielelezo kuwa tuna taifa Mfu! na serikali yenye dhamana ya uongozi kwenye mambo yote yanayolipatia taifa sifa, kuheshimiwa, mapato, marafiki haijui ilifanyalo na haijui inakoelekea! Mpira wenyewe hakuna popote umelifikisha taifa! Mpira wa mdomoni..kila mtu ni mchambuzi na afisa habari wa kujitakia kwa timu anayopenda..Eti nchi tunapeleka waogeleaji Olympics..r we serious? tumeshindwa kujua potential yetu iko kwenye michezo gani..? Nchi km Botswana ina watu million 3 tu tunawazidi mara 20, wmefanya homework yao vzr wamejipata, leo wanashiriki Olympics na kushinda medali! Michezo siyo futbal peke yake, na watu wa dar es salaam wanapaswa wafahamu jambo hili! Miaka ya 70, 80 na 90 nchi hii ilikuwa bora sana kimataifa kwenye riadha na netball..sijui ni wapumbavu gani waliingia na kuhamisha attention kwenye netball na riadha ikaenda kwenye uigizaji na u-miss! It's terrible! Tumekuwa km taifa lote tuna asili ya Pwani..maneno meeengi..na ushabiki wa kijinga! Leo tunashindwa na Burundi..kweli?? Nini tumebaki nacho sasa..ignorance na usimba na uyanga..???nini taifa linapata?? nguvu nyingi kwenye mambo nonsense kabisa km simba au yanga day..na media yetu ndio inaua mambo mazuri na kupandikiza ujinga kwa wananchi..!
TUJIREKEBISHE!
Yeye binafsi atambue kipaji chake na akionyeshe kijulikane mapema..Mkuu unadhani kwa mwanariadha anatakiwa afanye nini yeye binafsi ili awe mkimbiaji bora wa mbio ndefu tukiachia juhudi za mamlaka ?
Watu wa kuwahamasisha hawapo mkuu,wewe ungekuwa na nafasi ungetumia hiyo opportunity na tungeona matokeo.Kuna vitu huwa sivielewi...Wamasai wanakimbiza digi digi hadi wanamkamata mkia wakiwa wanawinda huko maporini sasa unawaza vipi wakipewa training ya kukimbia tena kwenye lami..Kuna wasandawe Wanarusha mishale hao n hatari lkn eti hadi warusha mishale hatuna huko Olympic.
😁😂Hapo Husikii WakiesemaMama anaupiga mwingi! Kazi iendelee
PAMBAF kabisaLeo aubuhi nimefuatilia shindano la Olympic kule Paris la mbio ndefu ya kilomita 42 na mwanariadha Ndugu Simbu akiwa mshiriki toka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kweli matokeo yake hayakuwa mazuri kwa kushika nambari 17 akitumia saa 2:10: 03
katika mbio hizo. Pole sana. Rudi nyumbani ukaendelee na mazoezi tena.
Matumaini ya Tanzania kuambulia chochote yapo kwa kinadada Jackline Sakilu na Magdalena Shauri ambao watatupa karata za mwisho za Tanzania katika mbio za Marathon kwa Wanawake ambazo ndio zitakuwa zinahitimisha rasmi Paris 2024.
Soma Pia: Wanariadha wa 4 kutuwakilisha kwenye mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa Mwezi Julai, Kambi kuwekwa Arusha
Katika matokeo mengine.
Tola Tamirat wa Ethiopia ndiye mshindi wa kwanza akinyakua medali ya dhahabu akiwa na rekodi mpya ya Olimpiki ya saa 2:06:26 huku nguli wa Kenya Eliud Kipchoge akishindwa kutetea taji lake.
Tola aliingia katika mbio za marathon za Olimpiki kama mchezaji wa akiba wiki mbili zilizopita, akijaza nafasi ya mchezaji mwenzake aliyejeruhiwa.
Bashir Abdi wa Ubelgiji alinyakua medali ya shaba kwa saa 2:06:47, huku Mkenya Benson Kipruto akitwaa shaba (2:07:00).