Mwanariadha Gabriel Gerald Geay aweka muda wake Bora Marekani

Mwanariadha Gabriel Gerald Geay aweka muda wake Bora Marekani

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Mwanariadha wa Kimataifa Gabriel Gerald Geay ashinda mbio za Boston 10K (B.A.A 10K) na kuweka muda wake bora wa 27:49 huko Boston, nchini Marekani Jumapili, tarehe 25 Juni 2023.

The B.A.A. 10K 2023 Results:

Men’s 10k results:

Gabriel Geay (Tanzania) – 00:27:49
Edwin Kurgat (Kenya) – 00:28:01
Alex Masai (Kenya) – 00:28:09
Tsegay Kidanu (Ethiopia) – 00:28:18
Diego Estrada (Mexico) – 00:28:19
Geoffrey Koech (Kenya) – 00:28:32
Benson Kipruto (Kenya) – 00:28:39
Wesley Kiptoo (Kenya) – 00:28:54
Abel Kipchumba (Kenya) – 00:29:05
Reed Fischer (United States) – 00:29:15
Zouhair Talbi (Morocco) – 00:29:28
Marcelo Rocha (Brazil) – 00:29:33
Reid Buchanan (United States) – 00:29:40
Leonard Korir (United States) – 00:29:45
Eric Hamer (United States) – 00:29:58
Richard Ringer (Germany) – 00:30:02
Tai Dinger (United States) – 00:30:12
Johannes Motschmann (Germany) – 00:30:15
 
Hongera zake sana.

Inaonekana wakenya kwa kukimbia wameshashindikana. Yaani Kenya ndiyo ilikuwa na wakimbiaji wengi kuliko nchi zote zilizoshiriki. Kwa nini wasiwe wanawachujana nyumbani na kubakisha watatu tu kuliko kupeleka wote hao ilihali inajulikana washindi ni watatu tu?

Kenya= 6
USA (wenyeji) =5
Germany =2
Brazil=1
Morocco 1
Ethiopia =1
Mexico=1
Tanzania=1
 
Hongera Sana kwake nafarijika Sana napooona kumbe kuna watanzania wanapenda riadha

Usiache kuleta habari za riadha tupo tunaokufuatilia mkuu

Swali; watanzania wengine walioshiriki mbio hizo majina yao tunaomba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawakushiriki, alishiriki yeye peke yake na ameshiriki mbio hizo mara nyingi…
 
Hongera zake sana.

Inaonekana wakenya kwa kukimbia wameshashindikana. Yaani Kenya ndiyo ilikuwa na wakimbiaji wengi kuliko nchi zote zilizoshiriki. Kwa nini wasiwe wanawachujana nyumbani na kubakisha watatu tu kuliko kupeleka wote hao ilihali inajulikana washindi ni watatu tu?

Kenya= 6
USA (wenyeji) =5
Germany =2
Brazil=1
Morocco 1
Ethiopia =1
Mexico=1
Tanzania=1
Tanzani bado tunajikongoja kwenye maandalizi,
 
Sijui kama ni kweli, ila nimesoma mahali kuwa Gabriel anaishi Tampa, Florida. Kwa hiyo hakushiriki mashindano hayo akitokea Tanzania moja kwa moja; yaani Tanzania haikutuma mtu kwenye mashindano hayo.
HAPANA; amesafiri wiki iliyopita, ila ataendelea kusubiri mashindano mengine ya Tarehe 4 Julai 2023…huko huko marekani.
 
Ameondoka wiki iliyopita, atakuwa na Mbio zingine zitakazofanyika, Atlanta , PeachTree Road Race, AJC , 10K
 
HAPANA; amesafiri wiki iliyopita, ila ataendelea kusubiri mashindano mengine ya Tarehe 4 Julai 2023…huko huko marekani.
Record za waandaaji wa mashindano hayo wameandika kuwa anatoka Tampa !!

1687854451664.png
 
Safi sana, hongera kwake kijana wetu, analeta heshima na motisha kwa wengine.
Nafikiri uwekezaji kwenye riadha hasa kwa maeneo yenye uhitaji sana unapaswa kupewa kipaumbele na serikali/wadau.
 
Safi sana, hongera kwake kijana wetu, analeta heshima na motisha kwa wengine.
Nafikiri uwekezaji kwenye riadha hasa kwa maeneo yenye uhitaji sana unapaswa kupewa kipaumbele na serikali/wadau.
Tunaendelea kuhimiza kupitia mitandao mbalimbali
 
Back
Top Bottom