Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais


kwa ujumla maelezo ya mtaalam huyu yamenitoa machozi Magufuli nitaingia vitani na wewe na wengineo mpaka hapo utakapo muajibisha mkapa, chenge and the rest otherwise taendelea kulia kama samaki machozi majini
 
Kabla hujaenda mbali; hiyo fraud unayoiita nani kathibitisha? Kwa ile tume ya raisi tutashindwa mapema asubuhi. Itahitajika independent committee ili ndio iwe base yetu mahakamani. So far yale matokeo ya tume hayana impact yeyote mahakamani
 
Wale ukileak watajua alieleak ni nani so utaadhibiwa tu hata huko kwa Trump wameambiwa leakers wote wanaapproach treason and they must be jailed to dry up the leaks!
 
Watanzania, raia yangu kwa wote, akiwemo Mh. Rais, matamanio yasifunike hekima na ukweli. Tungependa sana kufanya mambo fulani kwenye madini lakini lazima tutambue kabla ya kufanya tunahitaji uelewa wa kutosha, tahadhari ya kutosha na hekima ya kutosha.

Tanzania siyo kisiwa, kama nchi tuna mamlaka na uhuru wetu, lakini uhuru na mamlaka yetu siyo infinite, yana ukomo. Na ukomo huo tuliamua wenyewe kwa hiari yetu pale tulipoamua kuwa sehemu ya Dunia, na kisha tukasaini mikataba kadhaa ya Dunia inayopunguza mamlaka yetu.

Ukweli ni kuwa hatuna uwezo hata wa kugoma kusaini mikataba hiyo ya kibiashara ya Dunia. Usiposaini hupati wawekezaji maana nao wanaogopa risk ya kuwekeza katika nchi ambayo maamuzi yote yapo kwa nchi wanayowekeza.

Hili la mchanga, tunaweza kushangilia sana lakini ukweli ni kuwa tumechagua njia ambayo toka mwanzo tunajua haitatufikisha tunakotaka kwenda. Kabla hatujaenda mbali sana, turudi na kuichunguza zaidi njiΓ  hii ambayo inatutoa kwenye mfereje na kutupeleka korongoni.
 
Huyu ni mwanasheria UCHWARA. Hana uzalendo na nchi hii.
 
Dr. Kilangi amesema ukweli na ameitendea vema taaluma yake. Hajatuanagusha wasomi na ninamtakia kila la heri katika uandishi wa kitabu chake.

NB: Kumbikeni huyu ni mteule wa Rais. Ni mwenyekiti wa Bodi ya Petroli.
Huyo ni mwanasheria bogus.Anatetea ACACIA KWA VITISHO. Amesahau state sovereignity principle.Hata kesi tukishindwa watatufanya nini? Mwanasheria huyu anawajengea watanzania HOFU. Fake lawayers.
 

fanya tafiti vizuri usikurupuke.

huyo kanifundisha kabla hata hajawa Dr.

Pia kati ya uzee na ujana wewe unaupenda upi??
actually mimi naupenda sana ujana.
 
Pande zote mbili zinalalamika kupitia vyombo vya habari, malalamiko rasmi yanatakiwa yafikishwe mahakamani;
1. Serikali ya Tanzania idai fidia ya kuibiwa kwa kudanganywa kiwango cha madini kwenye mchanga.

2. Acacia wadai fidia inayosababishwa na kuzuiwa usafirishaji wa mchanga.

Mahakama itatoa maamuzi kufuatana na ushahidi utakaotolewa kuthibitisha kuthibitisha.
 
fanya tafiti vizuri usikurupuke.

huyo kanifundisha kabla hata hajawa Dr.

Pia kati ya uzee na ujana wewe unaupenda upi??
actually mimi naupenda sana ujana.
Si ndio maana uko bavichaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
 
Kabla hujaenda mbali; hiyo fraud unayoiita nani kathibitisha? Kwa ile tume ya raisi tutashindwa mapema asubuhi. Itahitajika independent committee ili ndio iwe base yetu mahakamani. So far yale matokeo ya tume hayana impact yeyote mahakamani
Bado tunakusanya ushahidi. Hao mashaidi wengine wa kimataifa muda mwafaka wataitwa ili nao washuhudie / verify hizo findings za tume yetu hususani lumbesa za kontena za mchanga (23 tons instead of 20 tons) na kadhalika.Tutakusanya ushahidi wa rushwa zilizokuwa zinatolewa na watu hawa, na tayari zipo zilizonaswa na kamera. Baada ya hapo ndipo tutaenda kuwashitaki kwa kosa la fraud.
 

Hivi hiyo TANU si ndiyo iliyoleta hii CCM ya majizi iliyouza nchi yetu kwa wazungu
 
Kabla hujatoa povu ungekaa na kujiuliza nani alikuwa anasign hizi contract na ni wakati gani. Wewe Yehodaya miaka yote ni CCM na viongozi wake sasa unaposema tumeibiwa wakati wewe ndo ulikuwa ukiimba CCM mbele kwa mbele tukueleweje? Huyu unayemkashifu huwezi funga hata gidamu za viatu vyake achilia mbali kukaa kuonge naye meza moja. You have nothing to contribute in this poor nation more than talking shite. Nyinyi ndo mlikuwa mnakaa kwenye magofu mnasubiri kengere mwende kwenye gwaride la chipukizi. Argue with points not with matapishi.
Thanks Dr. Kilangi You made my day.
 
Mbona tulipigwa kesi ya DOWANS tulipokwenda kule mahakama ya arbitration? tatizo watu tunapenda kuongea kishabiki mno
 
Na hata hili la kuyakamata haya makontena, kwani ACACIA wana uhakika gani kwamba hayajanajisiwa, na kwamba yako katika hali ile ile yaliyokuwa kabla? maana hata sasa hivi ikiletwa independent team kuyakagua, je "hayajaingiliwa"? Hii ni kwa upande wa ACACIA. mimi napenda sana nchi yangu iwashinde hawa jamaa wezi wa mali zetu, lakini tatizo hapa napambana na wezi wawili: CCM na hao wawekezaji. CCM ndio aliwapa hawa jamaa, leo anajifanya ameshitukia dili, wakati aliwapa mchana kweupeeee
 
Nashangaa sana watu wanaposema tumuibiwa miaka yote hiyo wakati makontena yote tulikuwa tunapima wenyewe (TMAA) kabla ya kutoka nje, na vipimo hivyo kwa mda wote vimekubaliana na vipimo vya kampuni ya vipimo ya SGS, sasa leo tutawadai vipi kuwa wametuibia?

http://www.acaciamining.com/~/media...n-gold-copper-concentrate-exports-english.pdf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…