Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Agent of imperialist at work. Ahadi mojawapo Ya mwana Tanu ilikuwa ikisema nitajiellimisha kwa kadri Ya uwezo wangu kwa faida Ya watanzania walio wengi .mleta maada kajielimisha sana kwa faida ya imperialists. Very sad.Yeye na tundu lisu wamejielimisha sana kwa faida ya imperialists
Kwa sasa kila anayewa-criticise mnamwona ndiye mchawi anayewawangia mambo yenu ya kukurupuka yasiwanyookee!!! Mlikurupuka kusaini mkataba, mmekurupuka tena kuuvuruga mkataba!!!!! .........oooooohhh ni ile ileeeeee ni ile ileeee.....
 
Dr. Kilangi amesema ukweli na ameitendea vema taaluma yake. Hajatuanagusha wasomi na ninamtakia kila la heri katika uandishi wa kitabu chake.

NB: Kumbikeni huyu ni mteule wa Rais. Ni mwenyekiti wa Bodi ya Petroli.
 
Hili ni andiko la Dr Adelardus Kilangi,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha,mwanasheria kitaaluma aliyebobea kwenye sheria za madini,na mwenyekiti wa bodi ya Petrol Tanzania!

............................................
Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.
Mkuu kama kuna vingine lete ,tunataka hoja za kisomi
 
Hakuna kitu kizuri kama kumjua mchawi wako hata kama anaweza kukudhuru, maana tunajua kuwa mchawi ameumbuka hadharani hilo ni pigo kubwa ambapo heshima yake imevunjika mbele ya jamii tunangojea tume iliyobaki ya kisheria ili tumvue nguo zote.Media ni silaha kubwa sana baada ya hapo waswahili husema penye nia pana njia tuendelee na nia yetu nzuri na tutapata njia na kamati ya kisheria itatushauri pa kuanzia.
 
Nilitegemea labda baada ya kusoma hizo background ntakuta maelezo ya aina ya mikataba na clauses zake nchi inayoweza ingia, sababu za kuchagua frameworks, sheria Ina compliment vipi contractual framework nchi inayopendelea, etc with nitty gritty za mikataba.

Mweh
 
Tujiondoe MIGA kwanza, na kwenye treaties zote then tuwatetemesha hawa jamaa...this time ni MAUMAU tu. Overconfidence ya Magu ni changamoto au wenda jopo lake limekamilika ili wengine tubaki ktk sala tu!
 
Agent of imperialist at work. Ahadi mojawapo Ya mwana Tanu ilikuwa ikisema nitajiellimisha kwa kadri Ya uwezo wangu kwa faida Ya watanzania walio wengi .mleta maada kajielimisha sana kwa faida ya imperialists. Very sad.Yeye na tundu lisu wamejielimisha sana kwa faida ya imperialists
Idiot. Mchango wako uko wapi?
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria
Hili ndilo tatizo tulilonalo. Watu wenye elimu zao wakijaribu kutoa mchango wao kwenye mijadala, wanaibuka vichwa-panzi na kutaka kugeuza mjadala wa kitaaluma kuwa wa mipasho.
 
YEHODAYA mbona unaleta matusi ndugu yangu?Lete hoja ili mjadala upambe moto sio kumtukana mtu.
Mpuuze. Ukitaka kumuua mbu, mnyime access ya damu. Ukitaka kumdhibiti attention seeker, mnyime attention
 
Sio kwa faida ya imperialist mkuu bali ameelezea vipengele vya namna mikataba yetu ilivyo ngumu kuwakaba hawa wazungu ambao wao wenyewe ndio wana influence utungwaji wa hizo sheria.

Kiufupi hawa majamaa wanakaba potepote, ndio washika vibendera na marefa wa huu mchezo wa wa uwekezaji katika sekta ya madini.
Jiulize tutapenyea wapi sisi ngozi nyeusi? yaani ni mwendo wa "ukimumunya nchale, ukimeza nchale, ukitema nchale" sarareee Watanganyika mwafwaa!
Haiingii akilini kwamba kampuni inaingia gharama ya kusafirisha makontena hadi 300 ya mchanga kama hayana faida yoyote. Ninajiuliza jee miaka ishirini iliyopita katukuwa na viongozi au walikuwa wapi? Au tuseme kwamba tulikuwa na wanyapara tu. Jamani yuache siasa uchwara tupiganie rasilimali zetu zinazopotea. Kipindi cha ukoloni walituibia almasi pale mwadui sasa na leo pia? Imetosha
 
Tujiondoe MIGA kwanza, na kwenye treaties zote then tuwatetemesha hawa jamaa...this time ni MAUMAU tu. Overconfidence ya Magu ni changamoto au wenda jopo lake limekamilika ili wengine tubaki ktk sala tu!
What about the stabilization clause ndani ya mkataba wenyewe auwezi kukupeleka kwenye arbitration ata ukijitoa huko.
 
Agent of imperialist at work. Ahadi mojawapo Ya mwana Tanu ilikuwa ikisema nitajiellimisha kwa kadri Ya uwezo wangu kwa faida Ya watanzania walio wengi .mleta maada kajielimisha sana kwa faida ya imperialists. Very sad.Yeye na tundu lisu wamejielimisha sana kwa faida ya imperialists

You're very liar and hypocrite!
Just an agent of CCM Hooligans and corrupt rulers!
Trying to condemn Tundu Lissu and author of this thread instead of people like Ben Mkapa,Andrew Chenge,Jakaya Kikuete and all ministers in and out of CCM current leadership is a bright day cheating!!!!
T.Lissu has been on the forefront to speak loud n' clear opposing the Tanzania Mining Law& Contracts!

Tatizo la mi-CCM mnataka kuishi maisha ya mnyama 'KINYONGA'! Kila kukicha mnataka kubadilika rangi like unto a chameleon ili KUKIDHI TAMAA ZENU ZA KISIASA!

Kitu mnachosahau ni kwamba huyu mtawala wenu wa sasa Magufuli anafanya kazi za WAPINZANI aidha kwa maksudi au kwa bakhti mbaya bila kujua kuwa anasafishia njia upinzani 2020!!!
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria
Kwani ukikiri kuwa hujaelewa kitu kuna ubaya gani kiliko kutuletea ubishi wa kishabiki yanga na simba we mswahili?
 
Mwandishi hajapendelea upande wowote, ila ame elezea Nguvu tuliyonayo kama nchi na Mapungufu tuliyonayo kama nchi juu ya mikataba.
Kilichonipa nguvu mwandishi amemalizia kwa kusema hii ni vita. Kwamaana hawezi kuweka hadharani (jukwaani)kitugani tunatakiwa kufanya kama nchi. Ila atakapo takiwa kutoa mchango wake wa kitaaluma ili kupambana na wizi huu atawashauri serikali nini chakufanya, kuwabana Hawa wawekezaji.
 
Pamoja na umuhimu wa kujua background ya migogoro ya miaka 50 na 60 maana hiyo ndio premise ya contractual frameworks zaleo. Ukitaka kuelewa mambo ya mikataba lazima uzijue frameworks zenyewe, main clauses zake, faida na hasara zake, sheria tulizonazo zina support framework zipi.

Aina ya frameworks:
Production sharing agreement
Concessions agreement
Joint venture agreement
Risk/Services contracts

Utaona sheria za nchi zinalenga hapo kutona na prefered contractual framework sio utumbo ulioandikwa na huyo msomi wenu just nonsense.
 
Maelezo ya Dr. Kilangi ni namna nyingine yenye ufasaha zaidi ya maelezo ya Mhe. Tundu Lissu. They have the same position. Na kwa maelezo ya Dr. Kilangi kweli hii ni vita, na mshindi wa vita anajulikana wazi kwa mujibu wa maelezo hayo ya Dr. Kilangi.

Kwa mtazamo wangu kabla ya kuanza vita, maelezo ya namna ya Dr. Kilangi yalitakiwa kutumika kwenye kupanga vita hii ili kuona kama kuna faida kubwa hasara kidogo au hasara kubwa faida kidogo. Pia ingesaidia kutoa options nyingi na kuchagua favourable option kama ingekuwepo kati ya hizo options.

Mimi ni mmoja wa watu tutakaopenda tusome 'kitabu' ili kupata mwanga zaidi. Kwani ili chapisho liitwe kitabu linakuwa na features zipi? Tena kitabu ndio kizuri zaidi kwani tutaona na references au bibliographies zaidi ambazo zitatusaidia tuone hoja zao kamili.
Tatizo bunge letu ni la ndiyooooooo! Huwa wanatengeneza hadidu za rejea nzuri sana
 
Suluhisho LA mgogoro huu ni kuamua kununua smelter kwa gharama yoyote! Mchanga huu tuufanyie smelting wenyewe! Hayo matani ya dhahabu yawe halisi na si ndoto!
Huo utakuwa ni ushahidi tosha kuwa "wawekezaji" wamekuwa wakituibia! Tutadai madini yote waliyokwisha kuiba toka waanze kusafirisha mchanga! Na itakuwa ni sababu tosha ya kuvunja mikataba yote na wawekezaji wa kwenye madini na tuwekeane mikataba yenye manufaa! na lazima iwe wazi!
 
Pamoja na umuhimu wa kujua background ya migogoro ya miaka 50 na 60 maana hiyo ndio premise ya contractual frameworks zaleo. Ukitaka kuelewa mambo ya mikataba lazima uzijue frameworks zenyewe, main clauses zake, faida na hasara zake, sheria tulizonazo zina support framework zipi.

Aina ya frameworks:
Production sharing agreement
Concessions agreement
Joint venture agreement
Risk/Services contracts

Utaona sheria za nchi zinalenga hapo kutona na prefered contractual framework sio utumbo ulioandikwa na huyo msomi wenu just nonsense.
Dr.Kalemani atakuwa anafahamu mengi amekuwapo wizarani kwa muda mrefu
 

Attachments

Back
Top Bottom