Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Kwahiyo hili ni suala la kisanyansi au la kisheria zaidi? Kuapa sio tatizo hata wanaotumbuliwa wanakuwa wameapa! Nilitaka tu kujua kama ripoti ya "maprofesa" ni "duniani na mbinguni"-kwamba sasa imethibitishwa, with no reasonable doubt kwamba ACACIA ni wezi?
Ndo maana ile report Mruma alikuwa anatoa Maximum and Minimum Tonnes za Ounces maana yake ni posibility ya kiasi kilichopo kwa hiyo michanga, hizo ni hesabu lakini kama ulisoma HGL ukaenda hapo UD darasani mnajazana 700 mtabaki kutusumbua tu humu na visheria vyenu
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria

Mkuu,

Weka chanzo cha taarifa yako ili na akina siye tupate maarifa na tuwaumbue "wezi" hawa.

Kaka ...
 
Hili ni andiko la Dr Adelardus Kilangi,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha,mwanasheria kitaaluma aliyebobea kwenye sheria za madini,na mwenyekiti wa bodi ya Petrol Tanzania!

............................................
Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.

Dr. Adelatus Kilangi

[emoji767]copy and paste

Mwanshinga msafwa.
 
Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.
Daktari amesema sawa kwa mambo mengi ila hapa amekosea. TEITA Act iliandaliwa kwa pamoja baina ya Makampuni, serikali na CSOs, kisha kufikia consensus kuwa mikataba iwekwe wazi. na hii ni consistent na EITI Standard. Aidha kulifikiwa consensus kuwa iwapo kutakutwa non compliance ya MDAs, sharia ya TEITA itatumika retrospectively. Ninaijua vizuri sheria hii tangu maandalizi yake (2012) hadi kupitishwa Dodoma (2015 - nilishiriki).
 
Kuna kitu kimmoja kikubwa kinakosekana.
Dr.Hajui how to deal with international codinated corrupt syndicate.
Hana experince wala hana exposal ya mafia world,yeye anafikiri the world is just fair.
Pole Dr.Jipambanue kwanza ujue underwold.
 
Mkuu,

Weka chanzo cha taarifa yako ili na akina siye tupate maarifa na tuwaumbue "wezi" hawa.

Kaka ...
Kalaghabaho na uchadema wenu usio na uzalendo wenye hisa wako highly interested kujua kama management ya accacia iliiibia tu serikali ya Tanzania au waliwapiga na kuwaibia na wao. Bei za hisa za accacia zimeshushuka kwenye masoko ya hisa Ya kimataifa wanahisa wanataka maelezo ya kueleweka Kama management ya accacia iliibia tu serikali au nao walilizwa ripoti Ya tume za uchunguzi za serikali ya magufuli wanazichukulia very serious. mleta mada alichoandika na matamko ya akina lisu na chadema ni upuuzi mbele Ya wanahisa wa Accacia ni aibu kwa mtu kujiita msomi na kuandika vitu vya kipuuzi kama alivyoandika mleta maada. Hoja kama za tundu lisu na chadema kwa wenye hisa wanaziona ujinga mtupu. Heri wangenyamaza kimya. Issue hii ya mchanga wanahisa wanaichukulia very serious kuhakiki kuwa je na wao hawajaibiwa na management? Mtu wa kuwahakikishia hili ni raisi na tume zake sio mleta mada wala mpiga yowe koko la kisheria tundu lisu au chadema
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.
Kweli kabisa, naona pia kaichambuwa kidogo sana, hasa upande wetu tunaoibiwa, ebu tusubiri wengine waje nao, ila hapa ACACIA wamepatikana, JPM kawakamata vizuri mno, wakubali kosa tuhesabiane vya kuhesabiana, wawe wa kweli sio uababaishaji, wajuwa walitegemea mambo yatakuwa kama walipokuwa wa kina chenge na warema, kumbe bana mambo yamebadilika! Wako hoi..
 
Makosa ya kitaasisi magumu sana kurekebisha kwa sababu yanakuwa yanalindwa na sheria. Hatuna wa kumlaumu kwenye suala hili la madini. Serikali na Bunge vyote vinahusika.
Kinachoniumiza mimi ni pale ninapoona kitaasisi kidogo kama TMAA kinakaliwa kooni; Waziri Muhongo anasulubiwa kama vile kutolewa sadaka tu.
Tuunde Tume ya ukweli na maridhiano juu ya hujuma za kiuchumi na kijamii nchi hii. Tutayajua mengi tu na kuyarekebisha.
 
Sheria ni kitu ngumu sana kuilewa na hasa wananchi wa,kawaida.. wanaongozwa na hisia na ushabiki. Angalau mwenye ufahamu au anayetaka ufahamu anaweza kuelimika, inapokuja swala la mikataba, kuna mengi na wanasheria wetu wana jukumu kubwa kuelimisha.
 
Kwa maelezo hayo tumeisha kwama kitambo. Mtu wa kutunusuru hawezi kuwa yule yule aliyetuingiza unless awe radhi kuaibika.
Itafutwe namna bora ya kufukia kichwa cha mbuni kwenye mchanga. We are in a fix!
 
Cha ajabu. Wengine wanampunga mtaalam hata sheria hawajui, toeni hoja na watu wazichambue
 
Agent of imperialist at work. Ahadi mojawapo Ya mwana Tanu ilikuwa ikisema nitajiellimisha kwa kadri Ya uwezo wangu kwa faida Ya watanzania walio wengi .mleta maada kajielimisha sana kwa faida ya imperialists. Very sad.Yeye na tundu lisu wamejielimisha sana kwa faida ya imperialists
Inaonekana akili zako ziko chini huna hata uwezo kufikiria mbali huna Pumbav!!!!!! Mkubwa!!!!!
 
Hili swala ni sawa na mbu anakungata kwenye korodani ukipiga kwa nguvu unaumia ww na ukimwacha unaumia ww
Cha kufanya hapa ni kutafuta namna ya kumuuwa kwa utulivu tuache ushabiki tuungane as Tanzanian tumalize hili swala salama na kwafaida kwa sisi na vizazi vijavyo

Chinekeee
 
Amenifungua ubongo, just why tangu mabishano haya yaanze, sija comment chochote. Mwanzo niliona Kama Raisi amefanya vizuri, lakini kadri Siku zinavyokwenda naaza kukata tamaa. Tuendako nathani kuna kiza kinene.
Rais wetu angekua hawachukii wapinzani tungekuwa tunapambana na adui mmoja kwa silaha sahihi bila kupoteza muda.
Tundu Lisu alionya kwa maneno makali na kikakamavu.
President alipaswa ku absorb political segment ili nationalism segment ituletee ushindi.

Lakini ile mentality ya kuona yeye ndio yeye inatukwamisha kipuuzi kabisa.

Magufuli ni tatizo kwa nchi yetu, ukijumlisha ccyem yao linakuwa Janga!!!!!
 
Back
Top Bottom