Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Usiwasahau walee wahusika walio saini hiyo Mikataba!!.

Dr. [emoji310] Ametoa facts [emoji115] [emoji115] [emoji115] . Muhimu kuzingatia.
Well written!
 
Bahati mbaya wewe hukujielemisha hata kwa faida yako binafsi. Na baada ya TANU kuwa hijacked, the rest ni historia.
 
Narudia kusema tena. Rais asione nongwa kuwaita kina Lissu na wenzake kujadili mbinu na njia ambazo zitakuwa na athari ndogo katika kuwabana hawa jamaa wa mchanga.
Akitumia hasira na maamuzi yasiyozingatia sheria ataiumiza nchi vibaya. Akae nao wabobezi Wa sheria ila siyo masaju, chenge
na mwakyembe watampoteza.
 
Nadhani labda tumesahau kuna kamati nyingine itakayoshughulika kuangalia madhara ya kiuchumi yaliyotokea na pia changamoto za kisheria zilizopo.
 
hoja yako ni ya kweli kujipanga ni muhimu lakini kumbuka moja ya kombora hatari tulilonalo ni Acacia kudanganya kuhusu uzito wa makontena,9 kwa yaliyopitiwa yapo yaliyozidi uzito kwa tani wala sio kilo. Huu nao ni wizi wala haihitaji tume huru ni kumuita yeye tukapima atasema tumeongeza mchanga wa baharini?
Ni kujipanga tu mpaka hapo tunaongoza moja bila.
 
Uzalendo uchwara
 
sasa we msoshalist njoo na hoja zako za kututoa hapa tulipo.
 
Kuitetea ccm kwa mambo wanayoyafanya lazima utakuwa unatembea na dozi toka mirembe mfukoni.
 
Kwa uelewa wangu,naona Dokta angalau ametoa mwanga.Kwa mujibu wa utangulizi wake anasema yeye hataki kuegemea upande wowote ,kwa maana ya kutoa uamuzi wa aliyeshinda au kushindwa.Ukisoma kwa utulivu yeye amejaribu kutuonyesha pande zote mbili za shilingi.Sehemu ambapo kuna makandokando na mahali ambapo kama nchi tuna ahueni na tunaweza kusimamia kujihami.Hii ni vita ni lazima tuipigane tulinde mali ya nchi yetu.Kujikwaa si kuanguka.Hebu vichwa hivi vyenye uelewa wa sheria za madini ,za nchi na za kimataifa vikutanishwe viunge uzi mmoja vitoe ushauri.Huu si wakati wa kutoa silaha zote ndio maana wanaojua wamenyamaza wanasubiri wakati muafaka.Naomba tuendelee kuelimishana na mwisho wa siku",kitabu" kitasomeka kilaini na vita tutaishinda.Jiulize kama hii hela yote ingekuwa hazina ,maendeleo yangekuwaje.Kilio cha maji maji maji maji maji....umeme ..... kingeisha mara moja.
 
Endelea unadhani Iraq na libya walipenda ,ukikataa kutoa huwa wanatumia nguvu hao mabepari, watatungo uongo kuwa mnahifadhi magaidi kibiti huko wanashambulia kibiti madini wanavuna geita
 
Safi sana well said
 
Thanks Dr kwa ufafanuzi huo Ubarikiwe sana
 
Amenifungua ubongo, just why tangu mabishano haya yaanze, sija comment chochote. Mwanzo niliona Kama Raisi amefanya vizuri, lakini kadri Siku zinavyokwenda naaza kukata tamaa. Tuendako nathani kuna kiza kinene.
Usikate tamaa Major,huwezi amin ukichagua side sasa hivi utakua unabetia mawazo yako,acha kubeti kwenye hii issue,hata kesi iwe vipi mawakili wanakuwepo pande mbili na hapo ndipo panabeba maana ya neno "usikubali kubeti" tuache wanaojua sheria waumane tusijipe pressure Major trust me kesi ni kesi tu,atakayekuwa na wakili makini atashinda,we stay tune ITAFAHAMIKA
 

Na wewe toa elimu yako
 
Uchunguzi wa upande mmoja hauwezi kukubalika katika mahakama za kimataifa na hili ndio kosa kubwa tulilolifanya.

Kingine cha kushangaza ni kwanini serikali haitaki kukubali hoja ya ACASIA ya kuunda Tume Huru kuchunguza jambo hili?
Naomba unijibu kulingana na nilivyo uliza,,,SWALI,.

1.Ukihisi unaibiwa,utamwambia unaemhisi aje mthibitishe kwa pamoja kabla ya wewe kuwa na uhakika kuwa umeibiwa!!!?

2.Naomba unithibitishie hii kauli yako,, "Serikali haitaki" ili nielewe kwa nini unashangaa

Kuelimishana ni vizuri ila kueleweshana ni vizuri zaidi,nna imani utanielimisha nnapokosea na nitaelewa nisipopaelewa
 
Binadam sisi ni watu wa ajabu sana. Kwa mfano JPM asingezuia hayo makontena, haya tunayoyaongea tungejuaje. Tungeelewaje undani wa hizi asasi za kimataifa tulipojifunga? JPM did the best ever, nani mwingne angeweza kufanya hayo? Kama umemuelewa mtoa mada kuna kitu kakieleza kinaitwa state capture, kuna ma tycoon na watu wazito waliokuwa na influence kwenye kuridhia hizo sheria kandamizi ila JPM hakujali hlo amejali nchi kwanza. Tusimlaumu JPM, ametufunilia ni jinsi gani tulikuwa tunaibiwa.. Maana kila mwenye akili timam anaona kuwa mikataba hyo na ya kilaghai na kinyonyaji. Tuchambue tuwezavyo ila tusimtafute mchawi.

[HASHTAG]#tutalivuka[/HASHTAG] [HASHTAG]#daraja[/HASHTAG] [HASHTAG]#tukilifikia[/HASHTAG].
 
Hivi karibuni kumetokea varanganti la aina yake kuhusu taarifa ya kamati ya makinikia. Kumejitokeza kuvutana kati ya Setikali na wawekezaji na pia baadhi ya Wananchi amegawanyika pia na inavyoonekana kila siku zinavyokwenda mbele ndivyo mzozo unazidi. Natoa mapendekezo kwa Serikali na wawekezaji kusafirisha hayo makinika mpaka yanapochambuliwa, yasimamiwe na pande zote mbili wakati wa kuchambuliwa na ukweli upatikane na hicho ndicho kiwe kigezo cha wawekezaji kulipa kodi kwa kila makinika yatakayokuwa yanapelekwa huko kabla hatujanunua mashine yetu.
N.B. Mod tafadharini msiuunganishe uzi huu na nyuzi nyingi kupindukia zilizomo humu. Napenda serikali iupitie ushauri huu ili kumaliza mzozo huu kistaarabu.
 
Haya mwenye mbwa kamteua mtetezi wa wahuni kuwa AG..ngoja tuone mbwa mzalendo ataendelea kubweka au!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…