Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

YEHODAYA Rafiki huyu aliyeteuliwa leo AG (nadhani ni huyu aliyeandika article hii) nimesoma hapa umemuita majina yote ya dharau, muhuni, msaliti, mkoloni. Leo naomba maoni yako! Please come and come all Lumumba!
 
@
Sio kwa faida ya imperialist mkuu bali ameelezea vipengele vya namna mikataba yetu ilivyo ngumu kuwakaba hawa wazungu ambao wao wenyewe ndio wana influence utungwaji wa hizo sheria.

Kiufupi hawa majamaa wanakaba potepote, ndio washika vibendera na marefa wa huu mchezo wa wa uwekezaji katika sekta ya madini.
Jiulize tutapenyea wapi sisi ngozi nyeusi? yaani ni mwendo wa "ukimumunya nchale, ukimeza nchale, ukitema nchale" sarareee Watanganyika mwafwaa!
Kisima leo huyu atatwambia nini kuhusu huyu aliyeteuliwa aliyemuita argent wa imperialism! Leo ni mzalendo?
 
Jinga kabisa wewe! Weka akiba ya maneno kiazi wewe!

Jana uliniita kibaraka wa mwingereza! Kumbe ndo ujinga wako unauonyesha badala ya kuuficha.
Baada ya kukuita kibaraka wa mwingereza Leo hujaandika neno lolote LA kiingereza umebadilika Hongera wewe ambaye ulikuwa kibaraka wa mwingereza aliyekuwa akijivunia lugha koloni ya mwingereza ambaye umebadilika sasa hivi unaandika kiswahili kilichonyooka .Ukibaki hivi ulivyo sikuiti kibaraka wa mwingereza tena.
 
YEHODAYA Rafiki huyu aliyeteuliwa leo AG (nadhani ni huyu aliyeandika article hii) nimesoma hapa umemuita majina yote ya dharau, muhuni, msaliti, mkoloni. Leo naomba maoni yako! Please come and come all Lumumba!
. Reasoning capacity yake inakuwa moderated na matamko ya Makufuli
Sina wasiwasi atamsifu nakusema mtu sahihi wa kupambana na Lissu bungeni
 
Hili ni andiko la Dr Adelardus Kilangi,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha,mwanasheria kitaaluma aliyebobea kwenye sheria za madini,na mwenyekiti wa bodi ya Petrol Tanzania!

............................................
Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.
Naona Adelardus amekoi na kupaste yale ya Lissu, au naweza kusema hawa magwiji wa sheria wamezungumza jambo moja, tulichopaswa kufanya ni kuwabembeleza na ndio maana mbwe mbwr zote zimeishia kwenye kapuni.

Pamoja na ma international laws yote hayo bado wanaccm walipiga mumo kwa mumo ili na wao wapate. Hahahahahhaaa
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria
Duuu hata Adelardus hujamwelewa? Au ni hutyo tu quotes twa kingereza tumekupiteza. Alichosema Lissu hakiko tofauti kabisa na haya.

Tena magufuli akijua huyu jamaa aliwahi kuandika haya anaweza kutengua uteuzi wake? Yaani Adelardus anasema tunaweza kushtakiwa? Hili ni jambo Magufuli hapendi kulisikia japo limeshamla na mpaka sasa holaaaaaaa
 
Hahaha YEHODAYA atafukuzwa ccm hivi karibuni, mkuu wake anatambua wasomi wenye PhD yeye anawaita wasomi koko.
YEHODAYA sasa utaanza kushabikia TLP au ADC?! Na unavyopenda kusifia sijui utaandika nini na hao hawana sifa hahaha
 
Duuh, kwa aina ya ufafanuzi huu...kazi ipo. hivi second year wa LLB anashindwa kuandika hivyo? maskini Tanzania...
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria
Siku nyingine uwe unaweka akiba ya maneno!
Angalia namna ambavyo leo umeaibika!
Hatahivyo,nadhani huwa huna haya,Si ndiyo?
 
Baada ya kukuita kibaraka wa mwingereza Leo hujaandika neno lolote LA kiingereza umebadilika Hongera wewe ambaye ulikuwa kibaraka wa mwingereza aliyekuwa akijivunia lugha koloni ya mwingereza ambaye umebadilika sasa hivi unaandika kiswahili kilichonyooka .Ukibaki hivi ulivyo sikuiti kibaraka wa mwingereza tena.
Umesoma kipengele # 22? Hiyo hoja hakuitoa Lissu?vilevile mkamuita msaliti na akaponea kuuwawa pengine kwasababu hiyo ya kusema ni msaliti kwa Taifa?

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.
 
Kama limempa cheo, wapambe wake walitaka kumuuwa mtu risasi kwa maneno kama hayo tu.

Sioni tofauti kubwa kati ya aliyosema huyu AG mpya na aliyosema Lissu.
They are the same, Exactly the same! Akiyaona haya aliyemteua atamtumbua mara moja kuwa kumbe unatawaliwa na mawazo ya Lisu, ... Yehodaya unasemaje?

Sent from my HM NOTE 1LTEW using JamiiForums mobile app
 
Theu are the same, Exactly the same! Akiyaona haya aliyemteua atamtumbua mara moja kuwa kumbe unatawaliwa na mawazo ya Lisu, ... Yehodaya unasemaje?

Sent from my HM NOTE 1LTEW using JamiiForums mobile app
Kwahiyo kama siyo siasa za kijinga za hii nchi, Lissu ndo angetakiwa kuwa AG! Assuming huyu amemteua baada ya kuona haya aliyoyasema!

Personally, sidhani kama hajayaona.

Kipanya alikuwa sahihi kwenye ile katuni yake ya mkuu akijipiga risasi ya mguu!
 
hapakuwa na sababu ya kumpiga Risasi. Lisu will always be a HERO! UZAO ULIOBARIKIWA
Bahati mbaya katuni sikuiona. Niwekee tafadhali kama umeitunza
 
Umesoma kipengele # 22? Hiyo hoja hakuitoa Lissu vilevile mkamuita msaliti na akaponea kuuwawa pengine kwasababu hiyo ya kusema ni msaliti kwa Taifa?

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.
Na Lisu alisema tatizo kubwa ni mikataba tuliyosaini na sheria za kimataifa .. MIGA, ICSDI??? (rekebisha)... yote alitasema Lisu, utadhani huyu Dk. amekopi kwa LISU
 
Back
Top Bottom