Mwanasheria mkuu amepotoka

Mwanasheria mkuu amepotoka

kapotolo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2010
Posts
3,727
Reaction score
2,217
Kwa kweli hata mimi sikumuelewa, ameongea kwa dharau sana, kwamba eti katiba ni kitu kidogo sana na eti watu wanaongea kama bata hawaleti hoja.
Viongozi wetu need to be serious and should think twice before making any comment, they annoy u know, boring.
Namuunga mkono mhariri huyu Mwanasheria mkuu "Amepotoka! Katiba mpya haiepukiki; na maji yakimwagika hayazoleki"
Tahariri Tz daima..Mwanasheria mkuu amepotoka
Habari leo Werema: katiba mpya ya nini?HabariLeo | Werema: Katiba mpya ya nini?
 
Aisee huyu mzee niliwahi kufanya nae kazi kweli anadharau sana...!

Ni mtu wa amri, ukali na sio friendly kabisa kabisa. He is typical Mkurya na ana tabia ya kujivuna sana kwa kuona wengine hawaweza kazi kabisa...! Lets wait and see him, this is just the beginning of his weird answers...!
 
Ila kwa kweli mzee mbabe katika hoja zake! nafasi ile haihitaji mtu mwenye mentality ya kijeshi au mtu supressive. Angeacha watu watoe hoja zao na yeye atoe mwongozo wa namna nzuri ya kukipata tunachokihitaji bila kubeza hoja za wengine au kuminya mjadala na yeye kuelekeza mwelekeo kungali mapema hivi.
 
Waacheni hao kwani wanaingia taratiiiibu na wakifika 18 watapata wanachokitafuta
 
Kwa hiyo Kawaita Pinda, Agustino Ramadhani, Mkapa, Slaa, Mnyika, Warioba n.k kuwa ni Mabata kwanini kikwete asimfukuze kazi?
 
Kwa hiyo Kawaita Pinda, Agustino Ramadhani, Mkapa, Slaa, Mnyika, Warioba n.k kuwa ni Mabata kwanini kikwete asimfukuze kazi?
Chaguo lake.............. Ushawahi sikia katika historia ya TZ mtu akafukuza chaguo lake...............??? Kwa vile tushazowea kulitwa.......TWAROPOKA TUUUUUU
 
duh,kumbe kuna kenge wengi eh?
yani na usomi wake wote haoni mapungufu ya katiba au kwa kuwa inampa ahueni yeye?
au ndio msimamo wa jk
 
Huyu bwana sina uelewa naye. Sidhani wanaosema katiba mpya wanataka iliyopo ifutwe iandikwe mpya bali kinachotakiwa ni kuingalia upya kwa umakini, yale mabaya, mikanganyo na mabo yaliyo[itwa na wakati yaondolewe yaingizwe mazuri yanayoendana na wakati wa sasa. Hata ungefanyaje bado kwenye katiba ya sasa kuna mazzuri
 
Aisee huyu mzee niliwahi kufanya nae kazi kweli anadharau sana...!

Ni mtu wa amri, ukali na sio friendly kabisa kabisa. He is typical Mkurya na ana tabia ya kujivuna sana kwa kuona wengine hawaweza kazi kabisa...! Lets wait and see him, this is just the beginning of his weird answers...!

Mkuu hicho ndicho kinachoitafuna tz, majirani zetu wamepandikiza watu wao ambao wako tz kwa ajili ya kuua kila kitu-Reli, Umeme, bandari Airports ili washamiri wao tu-chunguzeni mtapata majibu ya haya nayoyasema!
 
Sidhani kama mwanasheria mkuu wa serikali Mkurya WEREMA anauelewa mzuri saana wa sheria kupita watanzania wengine. Mimi ninafikiri watu wasimjadili saana huyu jamaa, kwani lengo lake ni kuwatoa watu katika kujadili masuala ya msingi ya katiba na badala yake waTZ waanze poteza muda wao kwa kumjadili WEREMA. Mi nafiri WaTZ kwa ujumla wao ndio wenye uamuzi wa nini wanataka kufanya katika katiba yao. Iwe kuibadilisha kwa kuweka viraka kama ilivyofanyika huko nyuma au kwa kufanya OVERHAUL ya katiba yote. WEREMA atambue kuwa kile wananchi tunachokitaka ndio kitafanyika. Ni jukumu la serikali ya CCM kulielewa hili, kama wao ndio wanamtumia WEREMA kutoa yale wanayoyafikiria basi wajue kuwa THIS TIME NO WAY BACK ama wanafacilitate movement towards new Constitution or wananchi wenyewe tutaongoza msafara huu!!!
 
Imani yangu kwa wateule wa Rais ni haba haswa linapokuja suala linalohusu wananchi nao kukosa ulaji zaidi..
 
Mkuu hicho ndicho kinachoitafuna tz, majirani zetu wamepandikiza watu wao ambao wako tz kwa ajili ya kuua kila kitu-Reli, Umeme, bandari Airports ili washamiri wao tu-chunguzeni mtapata majibu ya haya nayoyasema!
Uko sahihi kabisa ndugu yangu!...hasa hasa kutoka kaskazini magharibi mwa nchi yetu....
 
haya machaguo mengine ya JK ni too much pumba.mbaya zaidi werema hajui kua hajui
 
Kwa kweli hata mimi sikumuelewa, ameongea kwa dharau sana, kwamba eti katiba ni kitu kidogo sana na eti watu wanaongea kama bata hawaleti hoja.
Viongozi wetu need to be serious and should think twice before making any comment, they annoy u know, boring.
Namuunga mkono mhariri huyu Mwanasheria mkuu "Amepotoka! Katiba mpya haiepukiki; na maji yakimwagika hayazoleki"
Tahariri Tz daima..Mwanasheria mkuu amepotoka
Habari leo Werema: katiba mpya ya nini?HabariLeo | Werema: Katiba mpya ya nini?

Huu ulevi wa madaraka sijui utakoma lini? Huyu mzee naye ni kama akina Mramba na kauli zake kwenye rada na ndege ya Rais!

Anaposema hakuna Katiba mpya huku akisisitiza wanaotaka katiba mpya si watanzania ni kikundi cha watu; Je yeye hayo ya kukataa katiba mpya ndiyo mawazo ya watanzania au na yeye anawakilisha kikundi cha watu?

Tunaitaji viongozi wanaoelewa kwamba ukiwa kiongozi siyo kwamba mtizamo wako ndio mtizamo wa taifa zima na vilevile siyo lazima uwe mtizamo ulifaalo taifa!

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
ameweka historia ya kuwa mpuuuzi, ameunga tera kwa wenzake tunaowajua kuwa hawana lolote si bora angekaa kimya tu?
 
Ukali wa kizuzu namna hiii bila kusoma alama za nyakati ndizo zitakazo mponza rais. Viongozi ambao wanataka kujikomba na kutekeleza mambo yao kwa frequencies za rais hata kama dhamira zao ninajua ukweli ndio wameifikisha Tanzania hapa tulipo. Presidential appointees wengi wameingia katika mtego wa kuweka professional zao chini na kufanya kazi kwa remote ya JK kutokana na NJAA zao. WEREMA bado ana njaaa ya kufa mtu. Hivi unategemea watu kama hawa wakiagizwa wawapige shaba wapinzani wote wa JK watasita? Hawa nai wasaliti wa wananchi na nchi.
 
Back
Top Bottom