Mwanasheria Mkuu: Jopo la Wanasheria lapambana kuokoa ndege ya Tanzania na mchakato wa Kimahakama upo katika hatua nzuri

Mwanasheria Mkuu: Jopo la Wanasheria lapambana kuokoa ndege ya Tanzania na mchakato wa Kimahakama upo katika hatua nzuri

Wapinzani wamenuna

Dege lipo mbioni kutua
Ulishawahi kuona mama wa jirani siku akipika chakula kizuri huwa anakuwa na maneno ya shombo na juu kwa majirani zake? japo huwa si kawaida yake kula chakula kizuri kila siku
 
Hapo ndio kwanini sala za watu wengi hazijibiwi. Unakuta mtu ana deni hataki kulipa halafu anamkimbilia Mungu eti amsaidie asilipe deni!

Wewe ni nani kujiweka kwenye nafasi ya kujua.. nini na nini kinajibiwa na Mola!!!!
 
Hapo ndio kwanini sala za watu wengi hazijibiwi. Unakuta mtu ana deni hataki kulipa halafu anamkimbilia Mungu eti amsaidie asilipe deni!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wakulima wa Afrika Kusini wana akili sana, huku kwetu mkulima anadai muda wa Rais kutawala uongezwe
Afadhali hayo anadai ukituletea maji baba hata ukitawala milele sisi hatuna neno. Harlequin kuwa kupata maji safi na salama ni haki yake.
 
Wewe ni nani kujiweka kwenye nafasi ya kujua.. nini na nini kinajibiwa na Mola!!!!
Mola amesema kupitia maandiko yake.... Msidhulumu, mtende haki, msikuchue visivyo vyenu etc labda wewe husomi Biblia au Quran. Ni dhambi kubwa kutaka kumdhulumu huyo mkulima jasho lake...
 
nimekumbuka stori moja, jamaa alishikwa na trafiki akadungwa faini, akalimbikiza wee, mwisho wa siku aliamua kuliendeshea kwenye viunga vya ndani kwake, yani anazunguka nyumba yake ili kupasha betri moto.
 
Benki inapochukua hati ya nyumba na kutaka kuipiga mnada huwa wanataka nyumba au pesa?
WaTz uelewa wetu uko wapi?
Kwa nini anakimbilia kukamata ndege wakati tunaambiwa hii nchi ni tajiri sana
 
SERIKALI imesema mchakato wa kimahakama wa kuachiwa kwa ndege mpya ya Tanzania, aina ya Bombardier Q400 iliyokamatwa nchini Canada hivi karibuni, uko katika hatua nzuri.

Mkulima, Hermanus Steyn aliikamata ndege hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita nchini Canada. Mzungu huyo aliwahi kuikamata ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 nchini Afrika Kusini mwezi Agosti mwaka huu.

Tanzania ilishinda kesi hiyo dhidi ya Steyn, baada ya serikali kutuma jopo la wanasheria wake Afrika Kusini. Lakini mkulima huyo ameibukia tena Canada na kuizuia ndege ya Bombardier Q400, ambayo ilikuwa tayari kuja nchini.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi alilieleza gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Uingereza, kuwa jopo la wataalamu wa Tanzania linaloongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Clement Mashamba liko nchini Canada, kuhakikisha ndege hiyo inaachiwa.

Alisema Wakili Mkuu wa Serikali na jopo lake, wanafanya kazi kubwa na hatua iliyofikiwa ili ndege hiyo iachiwe ni nzuri. Profesa Kilangi alisema kwa kuwa Steyn alipata amri ya kimahakama ya kuikamata ndege hiyo, Serikali ya Tanzania nayo imelazimika kufuata mchakato wa kimahakama ili amri hiyo itenguliwe na ndege iachiwe.

Kwa kuwa tukio la ndege za Tanzania kukamatwa nchini Canada, limejirudia mara ya pili baada ya tukio kama hilo kutokea mwaka 2017, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alimweleza Rais John Magufuli mjini Dodoma kuwa aliamua kumuita Balozi wa Canada nchini ili kueleza kwa nini kila ndege za Tanzania zinapotaka kutoka nchini mwake, zinakamatwa.

Profesa Kabudi alisema alifanya mazungumzo marefu na Balozi huyo wa Canada jijini Dodoma na kumweleza kinagaubaga, bila kupepesa macho na bila tashwishwi kuwa Tanzania haifurahishwi na tabia na vitendo hivyo vya kila ndege ya Tanzania inapotakiwa kuondoka Canada kurudi hapa nchini, inakamatwa.

“Nimemwambia siyo tu kwamba tunasikitika, lakini pia tumekasirika, kwa maana hiyo tunafikiri Mheshimiwa Rais kukushauri kama Canada inaendelea kuruhusu vitu kama hivi, siyo wao peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kwenda kununua ndege Canada, zipo nchi nyingine zinatengeneza ndege,” alisema.

Source: Habari Leo

My take;
Yule mzushi aliyeleta mada kuwa mkulima kashinda, sasa ameumbuka!
Hivi tunadaiwa kweli au hatudaiwi? Kama tunadaiwa, hii kazi ya kukwepa madeni kijanjajanja mpaka lini? Kama hatudaiwi kwa nini tusimshtaki huyu aitwaye Mkulima ili akome kutufuatafuata?
 
Hivi walokole wenzangu mko wapi tumpige mkulima upofu tena tumfanye alegee asombwe na upepo wa kisulisuli, tumechoka!
 
Back
Top Bottom