Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu, ameshindwa kumshauri 'kisheria/kikatiba' Rais Samia S Hassan

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu, ameshindwa kumshauri 'kisheria/kikatiba' Rais Samia S Hassan

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Kwanza, wakati Mama Samia anatangaza kifo cha Hayati JPM, alitangaza siku 14 za maombolezo ilihali kwenye katiba zinatajwa siku 21. Baadae Katibu Mwenezi CCM ndg Polepole akatangaza siku 21 kwa niaba ya chama 'MKANGANYIKO'. Wananchi walihoji kwanini Makam alitangaza siku 14 badala ya 21 'Mwanasheria' hakuliona hili.

Pili, mara tu baada ya kuapa na kutoa hotuba fupi, taarifa iliyotolewa ni kwamba Rais anaenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Baadae TLS wakatoa mwongozo wa kikatiba na kisheria kuhusu Baraza hilo kuwa kwasasa 'halipo'. Mwanasheria Mkuu na wanasheria wengine wa serikali mlikuwa wapi? Mbona hamjasema chochote? Washauri wa Rais mnamsaidiaje Rais?

Pia soma

Wakati mwingine ndiyo maana tunaamini taarifa za mitandaoni kuliko za serikali
 
Huyo ndio mtu wa kwanza Rais Samia anatakiwa kumuapisha, kama ataamua kuendelea na huyo wa mwanzo, au kama atachagua mtu mwingine.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ndio anatakiwa kuwa mtendaji wa kwanza wa serikali kula kiapo kabla ya wengine.
 
Isingekua ajali aliyopata Tundu lisu ile Dodoma, sasa hivi tungekua tunamchangia pesa kama asante mana mwezetu alitufanya tujue mengi kuhusu sheria. Prof. mzima alikosea kiasi hicho au mama alikaidi?
 
Kwanza, wakati Mama Samia anatangaza kifo cha Hayati JPM, alitangaza siku 14 za maombolezo ilihali kwenye katiba zinatajwa siku 21. Baadae Katibu Mwenezi CCM ndg Polepole akatangaza siku 21 kwa niaba ya chama 'MKANGANYIKO'. Wananchi walihoji kwanini Makam alitangaza siku 14 badala ya 21 'Mwanasheria' hakuliona hili.

Pili, mara tu baada ya kuapa na kutoa hotuba fupi, taarifa iliyotolewa ni kwamba Rais anaenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Baadae TLS wakatoa mwongozo wa kikatiba na kisheria kuhusu Baraza hilo kuwa kwasasa 'halipo'. Mwanasheria Mkuu na wanasheria wengine wa serikali mlikuwa wapi? Mbona hamjasema chochote? Washauri wa Rais mnamsaidiaje Rais?

Pia soma

Wakati mwingine ndiyo maana tunaamini taarifa za mitandaoni kuliko za serikali
Hatufai kabisa ni bomu tu
 
Rais ndio kanuni ya Katiba

Katiba haimwongozi rais ila rais anaingoza katiba

Katiba ni kitu ila Rais ni Nafsi
 
Kiukweli huyo mwamba apigwe chini , Jiwe alikuwa hafati katiba na Sheria inawezekana hata jamaa naye aliona hakuna haja ya kupitia pitia katiba [emoji39][emoji2]
Alikiwa amesahau notice za shule mpeni muda.
 
Walushazoea kuvunja sheria za nchi, ilishakuwa kawaida kwa utawala wa jiwe kukanyaga sheria.

Pili, mazingira ya kutangaza kifo hayakuwa rafiki kufanya mashauriano na Mwanasheria. Tangazo lilirekodiwa Tanga likatumwa TBC.

Mfumo na wenye Chama walikuwa hawataki kutangaza kifo, mtifuano ulikuwa unaendelea ndani kwa ndani kuhakikisha Mama Samia haapishwi kuwa Rais. Mama ni km aliwafanyia surprise.

Lilikuwa tangazo la kibabe.
 
Back
Top Bottom