Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kwanza, wakati Mama Samia anatangaza kifo cha Hayati JPM, alitangaza siku 14 za maombolezo ilihali kwenye katiba zinatajwa siku 21. Baadae Katibu Mwenezi CCM ndg Polepole akatangaza siku 21 kwa niaba ya chama 'MKANGANYIKO'. Wananchi walihoji kwanini Makam alitangaza siku 14 badala ya 21 'Mwanasheria' hakuliona hili.
Pili, mara tu baada ya kuapa na kutoa hotuba fupi, taarifa iliyotolewa ni kwamba Rais anaenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.
Baadae TLS wakatoa mwongozo wa kikatiba na kisheria kuhusu Baraza hilo kuwa kwasasa 'halipo'. Mwanasheria Mkuu na wanasheria wengine wa serikali mlikuwa wapi? Mbona hamjasema chochote? Washauri wa Rais mnamsaidiaje Rais?
Pia soma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Kilangi, jiuzulu kwa yanayotokea Bungeni na kunyamaza
Kazi muhimu ya Mwanasheria mkuu wa serikali ni kuishauri na kuisimamia serikali ili isiende kufanya mambo yanayokiuka Sheria na Katiba ya nchi. Hata kitendo cha kuhakikisha naye anakuwa sehemu ya Bunge ni kuona ndani ya jengo hilo tukufu sheria na katiba zinafuatwa bila kunajisiwa. Sasa hivi...www.jamiiforums.com
Wakati mwingine ndiyo maana tunaamini taarifa za mitandaoni kuliko za serikali
Fuatilia vizuri, viongozi wengi wa serikali huwa hawajui sheria wala katiba kwa upana wake,na wenye wajibu wa kisheria hufanya kuendana na mdundo wa kiongozi. wakati wa Magufuli ilikuwa ni rahisi sana kuongoza maana alikuwa hafuati sheria, bali alikuwa anatumia njia aliyooita nia njema ikiongozwa na uzalendo, hivyo mwanasheria Mkuu wa serikali, majaji, mahakimu na wengine walikuwa wanatekeleza sheria sio kama zilivyo, bali alivyokuwa anataka Magufuli. Sasa inaonekana bado mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu na wengineo bado wako kwenye hangover ya utawala wa Magufuli.