Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Jaji Mkuu wajitokeze Kujibu au kufafanua Hoja za Tundu Lissu. Hawa wengine wanajichanganya tu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Jaji Mkuu wajitokeze Kujibu au kufafanua Hoja za Tundu Lissu. Hawa wengine wanajichanganya tu

Mpaka sasa watu wanaoaminika kwa hoja na weledi ndani ya Chama cha Mapinduzi Ndugu Comrade Kinana Makamu mwenyekiti wa Chama Taifa na Ndugu Ali Happy ambaye mpaka sasa sijui cheo chake wamejitokeza kujaribu kujibu Hoja za Tundu Lissu.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wakati wa wiki mbili zilizopita Mh Wakili Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti Taifa Chadema alimwaga sumu ktk Mikoa takribani sita, sumu hiyo isiyoua bali inayolenga kuwapa Mwangaza Watanzania wote kuhusu Mstakabali wa Nchi yao na uongozi.

Hata hivyo inaonekana Damage aliyosababisha Tundu Lissu kwa chama Tawala is beyong Repair.

Baada ya Magwiji hao wa kisiasa Kinana na Ali Hapi kujitokeza kujibu na kufafanua wamejikuta wanajichanganya tu wao wenyewe na kuwachanganya wasikilizaji wao.

Mkanganyiko huo si vema tukauruhusu kuendelea maana unawaweka Wananchi Njia Panda au waendelee kuamini yale waliyofundishwa na Mh Tundu Lissu.

Niumbe kwa Heshima na Tadhima watu wenye ueledi kwa level sawa na ya Lissu wajitokeze ktk sehemu ya kuitumikia Taifa wafafanue na kunyoosha mabonde mabonde yaliyoachwa.

Mh Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu ni watu tunaoamini wana weza kazi hii kwa kiwango kikubwa na kufuta sintofahamu inayoendelea.

Waheshimiwa wasomi jitokezeni muokoa Jahazi.

Nawatakia kazi njema watumishi woote Nchini, tukutane 2025

Mambo yanayobishaniwa ni ya Kisiasa.... awaachie Wanansiasa.

Issue ambayo ilikuwa inawahusu, issue ya Bandari, Mwanasheria Mkuu akuizungumzia. Wataongea kama watapewa maelekezo.
 
Nyerere ukamfufue kaburini? tunataka solution ya huu muungano fake ambao ni wanzazibar pekee ndiyo wana haki

Lissu hakusema Mzanzibar asifanye maamuzi Bara.

Lissu amesema Mzanzibar kuziacha salama bandari na ardhi za Zanzibar huku anauza na kugawa bandari na ardhi za Bara ni ushahidi kwamba Tanganyika inadhulumiwa na Rais Mzanzibari asiye na uchungu na Tanganyika, na kwamba Muungano huu unabaka haki, rasilimali na maslahi ya Tanganyika.
Basi tulivunje hili LiMuungano tumrudishie Nyerere
 
Mambo yanayobishaniwa ni ya Kisiasa.... awaachie Wanansiasa.

Issue ambayo ilikuwa inawahusu, issue ya Bandari, Mwanasheria Mkuu akuizungumzia. Wataongea kama watapewa maelekezo.
Hao niliowataja ni nafasi zinazotokana na siasa na wanateuliwa kisiasa na siasa ndio zinazotunga hizo sheria na kanuniz za mahakama wanazosimamia wao

Tafuta sababu nyingine
 
Back
Top Bottom