Mwanasheria wa Yanga ashangazwa na mambo yanayoendelea soka la Bongo

Mwanasheria wa Yanga ashangazwa na mambo yanayoendelea soka la Bongo

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Tangu nimeingia kwenye mpira wa Tanzania, kitu ambacho nimekua sifurahishwi nacho ni kwamba Yanga ikiwa na jambo flani ikaenda kwenye taasisi yeyote hapa nchini, taasisi hiyo itapeleka jambo ambalo mnataka kufanya upande wa pili eti isionekane inapendelea upande mmoja.

Nina mifano hai, Yanga ilipeleka business concepts kwa taasisi kubwa 3 hapa nchini za kibiashara, zilivokubaliwa taasisi zile zikabeba concepts kama zilivyo na kuzipeleka upande wa pili ili wasionekane wanaipendelea Yanga, mwisho wa siku upande wa pili ukashindwa kutekeleza hizo projects.

Hii mentality ya tutaonekana tunapendelea timu mmoja imezidi kukua na kuduwaza watu.

Jamani eeh, dunia ya sasahivi watu ufaidika na matunda ya akili zao na kamwe watu wenye fikra tofauti hawawezi kuwa sawa, hii ndio maana halisi ya elimu.

Watani pelekeni proposal yenu wizarani, Serikali ya Mama @samia_suluhu_hassan ilishasema kila ombi au wazo lenye tija kwake litapita na ndicho Yanga tumefanya.

Wizara ya michezo na BASATA endeleeni kuupiga kazi, kama watu wameamua kulala kutotumia fursa za mama nyie pigeni kazi wakiamka watakuja.

Hongereni sana Idara ya Mashabiki na Wanachama ya Yanga kwa kuendelea kuwapambania mashabiki wetu.

Tukutane kwa Mabida, Kwao ni kama kwetu!

#daimambelenyumamwiko
 
• Sema umeandika hii thread, huku upo upande wa yanga.. Right ungeandika kama shabiki wa maendeleo ya mpira hapa Tanzania nina imani ungeeleweka vizuri 🤒🤒.

• Vipi lakini, mambo yanasemaje hapo mtaani 🤔🤔??
 
FB_IMG_1682646137959 (3).jpg
 
Back
Top Bottom