Mwanasheria wetu unakielewa ulichokiongea kuhusu Mange ama unataka kumfurahisha aliyekuteua?

Mwanasheria wetu unakielewa ulichokiongea kuhusu Mange ama unataka kumfurahisha aliyekuteua?

Kijana wa Ifoza

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2025
Posts
1,180
Reaction score
2,302
Nilimskiliza Mwanasheria wetu wa Serikali akiongea kuhusu Mange Kimambi kufanya jinai kwa kuhamasisha Maandamano, na akaendelea kwa kusema anafanya jitihada zozote hata za Kidiplomasia Mange arudishwe kujibu mashitaka. Ni aibu sana kwa mwanasheria msomi kuongea PUMBA kama hizi. Ninapata wasiwasi kama kweli huyu ni wakili Msomi kweli ama kama yule kibaka alieshinda kesi nyingi bila kusomea sheria.

Kwanza kwa kifupi Mange Kimambi hajafanya kosa lolote kwa sheria za Tanzania wala za Marekani na yeye (mwansheria) analijua hilo. Japo mimi siyo mwanasheria kama yeye ama Peter Kibatala ndugu yangu wa ukaya, lakini najua kabisa Katiba yetu na ya Marekani zinaturuhusu kufanya maandamano ya amani.

Nitaanza na kipengele cha Katiba ya Tanzania kinachoruhusu Maandamano.. Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema kila mtu ana uhuru wa kukusanyika kwa uhuru na amani. Haki hii pia inalindwa na vyombo vya kimataifa ambavyo Tanzania ni mwanachama, kama vile Kifungu cha 11 cha Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu. Japo haki hiyo hua inakwamishwa na sheria za kizamani hasa ile ya mwaka 1969 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 iitwayo Police Force and Auxiliary Services Act ambayo inawataka waandamanaji watoe report Polisi masaa 48 kabla ya siku ya maandamano.

Mange Kimambi pia akiwa Mkazi wa Marekani analindwa na sheria ya Marekani iitwayo
The First Amendment Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ni marekebisho yanayoruhusu maandamano ya amani nchini Marekani.
Inahakikisha haki kadhaa ambazo kwa pamoja hulinda uwezo wa kuandamana, zikiwemo
Haki ya uhuru wa kujieleza.
Haki ya watu kukusanyika kwa amani.
Haki ya kuomba serikali ili kutatua malalamiko.
Ulinzi huu unahakikisha kwamba watu binafsi wanaweza kukusanyika katika vikundi ili kutoa maoni yao na kuomba serikali kushughulikia matatizo yao, ingawa haki hii haihusu maandamano ya vurugu.


Nani wa kulaumiwa kukitokea vurugu na fujo kwenye Maandamano?

Tafiti zinaonyesha kwamba vurugu hutokeo Pale ambapo mamlaka ya serikali ni ya chini, wananchi hawafikirii mawakala wa serikali kuwa nyenzo muhimu kwa kutatua matatizo, na inapowezekana, wataamua kuepuka mwingiliano na mashirika ya serikali, kama polisi.

Utafiti pia unapendekeza kwamba nguvu ya serikali ya kulazimisha hufanya vurugu za maandamano kutokea zaidi, haswa wakati uhusiano kati ya serikali na jamii ni dhaifu. Katika mazingira haya, waandamanaji wanaona polisi waliojihami vikali kama watendaji haramu na wenye jeuri. Zaidi ya hayo, utafiti wa Brandon Ives na Jacob Lewis unaonyesha kwamba matukio ya ukandamizaji husababisha waandamanaji kufikiria upya gharama za vurugu. Maandamano yenye jeuri huwa na hatari kubwa zaidi—ya kuumia, kukamatwa, au hata kifo—kuliko maandamano yasiyo na vurugu. Hata hivyo, ikiwa waandamanaji wanatarajia jibu la ukandamizaji hata wakati wanahusika katika hatua zisizo za vurugu, basi gharama ya jamaa ya vurugu itapunguzwa. Katika hali kama hizi, waandamanaji wanaweza kuchagua vurugu kwa urahisi zaidi.

Baada ya ghasia za miaka ya 1960 nchini Marekani, mapendekezo ya Tume ya Kerner kwa serikali ya Marekani yalisisitiza umuhimu wa kuleta serikali karibu na raia na kuongeza ushiriki wa wananchi katika taasisi za serikali kama mkakati wa kuepuka maandamano ya vurugu ya baadaye. Badala ya kutuma jeshi, Marekani inapaswa kurekebisha uhusiano kati ya serikali na jamii—kama tume yake yenyewe ya machafuko ya kiraia ilipopendekezwa.

Kwa kuzingatia hizo tafiti ni dhahiri lawama za vurugu haziwezi kutupwa kwa wale waliohamasisha Maandamano bali serikali ilaumiwe kwa kutumia vibaya vyombo vya dola kudhibiti uhalifu wa baadhi ya waliungana kwenye maandamano kwa lengo la kufanya uhalifu.

Hitimisho

Ndugu yetu Mwanasheria Mkuu wa serikali nakuomba tu usituaibishe hata kupeleka hiyo extradition order utachekwa na itatupwa kapuni.






 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    6.4 KB · Views: 34
Wameshajua boss wao ni kumsifia tu

Kwanini asifanye hivyo ili apate mkate wake wa kila siku
 
Washamjua samuya mpenda sifa & kilazaa basi ni kumsifia kwa chochote kitu afurah kikubwa watoto wao waende choo!.

Wengine wamempa taarifa eti maandamano yalifanywa na vijana kutoka nje ya Tz hahhahaaa naye kama kawaida kaingia mzima mzima bila tafakuri!.
 
Washamjua samuya mpenda sifa & kilazaa basi ni kumsifia kwa chochote kitu afurah kikubwa watoto wao waende choo!.

Wengine wamempa taarifa eti maandamano yalifanywa na vijana kutoka nje ya Tz hahhahaaa naye kama kawaida kaingia mzima mzima bila tafakuri!.
Hivi wale waliofunguliwa mashitaka ni vijana kutoka nchi gani? Nilikua sifahamu kama Lema, Heche ni raia wa nje. Tanzania nchi yangu kutoka kuongozwa na Dr wa Kweli Dr Julius Kambarage Nyerere mpaka kuongozwa na typist Form Four failure
 
Back
Top Bottom