Mwanasiasa huyu alizaliwa na kipaji cha uigiza kwenye siasa aliingia kutafuta maisha tu

Mwanasiasa huyu alizaliwa na kipaji cha uigiza kwenye siasa aliingia kutafuta maisha tu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mnajua watanzania wengi mpaka leo kuna kitu hawajakigundua kuhusu bwana mkubwa na ndio maana anafanikiwa kuwa-manipulate kwa kiasi kikubwa tangu aingie ofisini.

Msilolijua ni kuwa bwana mkubwa ana kipaji cha hali ya juu sana cha uigizaji na ni kipaji cha kuzaliwa kiasi kwamba kama tangu ujana wake angeingia kwenye fani ya uigizaji angeweza kufanikiwa sana na angekuwa na jina kubwa katika fani ya uigizaji na wakati huu angekuwa anakula tu mafao ya uigizaji.

kwakuwa kaingia kwenye siasa na ana kipaji hiki cha kuzaliwa,sasa analazimika kukitumia katika siasa kwa madhumuni ya kisiasa na kamwe hawezi kuacha na wala msitarajie ataacha.

Kipaji hiki cha mheshimiwa kiko wazi kila anapopata wasaa wa kuongea na wananchi ambapo huweza kuigiza ana uchungu, hasira, yuko serious,n.k na hata sura yake ukiingalia inakufanya uamini kabisa kuwa kile anachokitamka ndicho anachokimanisha kumbe siyo.

kwa mfano,anaweza kuongea kwa uchungu kuhusu jambo fulani kiasi kwamba wanaomuangalia na wao wakaumia wanapomsikiliza ila rohoni akawa yuko tofauti kabisa lengo likiwa ni kuwahadaa wanaomsikiliza na kumtazama ili waamini anamanisha akisemacho.

Anaweza kuongea mpaka ukamhurumia kuwa anaguswa sana na matatizo ya watu kumbe mwenzenu anaigiza tu na kwasababu ana kipaji cha kuigiza basi anafanikiwa kuwachota watu akili.

Ushahidi mwingine wa wazi kuwa uigizaji ni kipaji chake cha kuzaliwa ni matukio ya kutengeneza anayoandaliwa bila shaka kwa maagizo yake na jinsi anavyoyamudu akiwa jukwaani.

Mtu ambae hana obi ya uigizaji haweze ku-entertain matukio ya aina hii tena ya mara kwa mara isipokuwa tu kwa mtu ambae uigizaji ni jambo analolipenda na ana-enjoy kulifanya ikiwa ni kipaji chake cha kuzaliwa.

Jambo lingine watu wanalopaswa kujiuliza ni pale anapoongea akionekana kuwa na uchungu na hasira juu ya lile analoliongea lakini ghafla anabadili mada na kuanza kucheka kwa raha kama hakuwa yeye kitu ambacho si cha kawaida na si rahisi kwasababu kwa kawaida hasira hushuka kidogokidogo na si kutoweka ghafla tena ndani ya dakika chache tu.

Ni imani yangu amezaliwa na kipaji cha uigizaji na kama angekuwa amezaliwa katika nchi za wenzetu ambazo vipaji vya watoto huendelezwa tangu angali watoto wadogo,basi bila shaka angekuwa muigizaji mzuri na angeonyesha kipaji kikubwa katika fani ya uigizaji.

Waliosoma nae,kama wamo humu, tunawaomba watueleze kama shuleni, kwa maana ya msinigi na sekondari, alikuwa hashiriki katika michezo ya kuigiza.

Mifano ya maagizo yake iko mingi na kwakweli inamsaidia sana kuwa-fool wadanganyika na wengi itawachukua muda kugundua janya yake hii.

Poleni sana wabongo.
 
Ni mmoja tu ana degree ya sanaa usihamishe Elimu na vipaji vya watu kuwapa wengine
 
Back
Top Bottom