TANZIA Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Njelu Kasaka amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu

TANZIA Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Njelu Kasaka amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu

RIP Mzee Njelu Kasaka, pamoja na kustaafu hakuacha kutoa nasaha na uzoefu wake popote pale anapoulizwa maoni yake


March 21, 2020
Chunya, Mbeya

TANROAD, DC na Mzee Njelu Kasaka wazungumza

Daraja la mto Lupa mafuriko, mbunge wa zamani wa Chunya, Mzee Njelu Kasaka amesema hali hiyo ya maji kujaa haitaacha mpaka mwezi September 2020 na hivyo changamoto ya usafiri bado ipo



Source : MbeyaYetuOnlineTV
 
Sory mkuu alikuwa nani ndani ya nchi hii. Sisi vijana wa juzi /jana wengine hatumjui
Huyu mzee alianzisha kundi la wabunge 55 la kudai serikali ya Tanganyika wakati malecela akiwa waziri mkuu kitu kilichomuudhi Sana Nyerere na ndiyo sababu malecela kukataliwa kugombea urais.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
...mwalimu kuona hivyo ilibidi atoke butiama mbio kwenda kuokoa jahazi na alifanikiwa kweli kuwanyamazisha yule mzee..
Ni kweli bila mwl.Nyrere hoja yao ilikuwa ipite kwa kishindo...kwenye hiyo hoja alikuwepo pia Mzee Malecela
 
Duu! Huyu mgeni kwangu kusema ukweli.
Kama siyo Nyerere basi leo tungekuwa na serikali ya Tanganyika.
Hivyo vichwa vya G55 vilipanga hoja zilizompoteza kabisa mzee wetu mpendwa Julius Kambarage Nyerere ambaye aliishiwa kabisa hoja za kuvikabili vichwa hivyo ikabidi asiye mbunge au kiongozi kwa wakati huo aombe kuingia bungeni ambako aliishia kutishia kwamba kama wataendelea kushikilia hoja hiyo basi yeye atarudisha kadi namba moja na kujitoa CCM.
 
Ukikipitia kitabu chake utaupenda uwezo wake wa kujenga hoja na lile vugu vugu la G55 unaona jinsi gani mzee huyu alikuwa hazina kubwa.... mwaka 1995 na nia yake ya kuutaka urais huku sera ya utanganyika haikuwahi kutoka kinywani mwake

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
ni mbunge wa zamani wa jimbo la lupa, chunya
mzaliwa wa mtanila, mkimbu amekufa na 87 miaka,
pumzika kwa amani babu mjomba, if i was
in lupa, i would have come and pay my last respect
 
Mzee wa G40 liliopitisha bungeni kurudia serikali ya Tanganyika .Njelu Kasaka,Kinyondo,Jenerali Ulimwengu walikuwa wabunge viwango.
Kama sio mbinu za Baba Ambiliki kutengua azimio hilo kwa mlango wa nyuma tungekuwa Tanganyika. RIP Njelu Kasaka.
 
Back
Top Bottom