Mwanasiasa yeyote, Hakikisha unajua hesabu ya Matendo na maneno yako kabla hujazungumza

Mwanasiasa yeyote, Hakikisha unajua hesabu ya Matendo na maneno yako kabla hujazungumza

Smartkahn

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2020
Posts
1,028
Reaction score
1,790
Tunatarajia kushuhudia mwanasiasa hasa yule mashuhuri(public figure), kuzungumza hoja zilizofanyiwa utafiti na zikathibitishwa kwa uchambuzi wa kina na scope pana.

Weledi katika hutuba unahitajika sana, kamwe usije ukajitolea tu maneno kichwani mwako utaharibu mambo.

Hayohayo maneno unayotamka tu ilimradi, yanaweza kuja kukufunga huko mbeleni ukawa au ukakiweka chombo katika wakati mgumu.

Kuongea ni kipaji na kuhutubia ni professional, hasa hutuba ikiwa inahusisha professional ya mamlaka/kitengo fulani.

Ndio maana katika sheria unashauriwa usizungumze chochote pasipo mwanasheria wako!

Kufanya mambo kiholela kuna gharama zake, nadokeza kama kuna jambo linahitaji utaalamu basi lishughulikiwe kitaalamu pasipo kijali mazingira au upo na audience wa namna gani.

Yaani kama kuna maswala ya kisheria basi iacheni sheria ifanye kazi yake, utawala wa sheria kila chombo kitimize wajibu wake pasipo kuingiliwa...ili Jamii istawi.

Mfano polisi wamezalisha matatizo mengi nchini kwa kukiuka misingi yao na kuingilia kazi ya mahakama.

Hiki chombo cha police hapa nchini ni corrupt kwa kivyovyote vile, kimekua tatizo! majukumu yake na wanachokifanya ni kinyume chake. Mwenendo wao umeshafika limit ni lazima kitu kifanyike kuhusu chombo hiki. (wanapoteza raia na Mali zao), kama kikisipo tazamwa upya basi tusije tukawalaumu, mabeberu kwa mipango yao ovu dhidi yetu.

Kwasababu hata wanaobakwa au wanaoibiwa na majambazi mara nyingi wao ndio wanakuwaga sababu. Wewe unajua uko vizuri una mali safi kwanini usiisitiri vizuri,
huyo mwizi wazo la kuiba atalitoa wapi.

Kwa lugha nyingine hawa vijana wetu Gen z wameshawishiwa na kuhamasishwa kwa facts na sababu zenye mashiko(sio kuhadithiwa tu bali wanaziishi), na sababu zenyewe sio kwamba zipo nje ya uwezo wa mamlaka kuzikabili la hasha bali ni incopitence yakutokua;

1. Proactive enough, instead watendaji wanakua reactive/firefighting mentality(zimamoto) tatizo likitokea si kiongozi wala Wananchi wote wanashangaa na kulalamika.

2. Weledi madalakani, kufanya mambo kiholela/kimazoea.

3. Uadirifu/nidhamu ya kazi/wajibu kutokutambua umuhimu na uzito wa nafasi kiongozi aliyonayo kwa jamii yake... Kuwachukulia poa wananchi/vikaragosi.
 
Ndio tunapoteza kidogo kidogo hadi hapa tulipofika tushatoka kwenye misingi ya nchi hii, Ambayo ndio uthabiti wetu, mbaya zaidi hakuna anaejari tena.
Tuoubaliane tu tunabahati mbaya sana kwa sasa toka 2015 hatujapata mwanasiasa anayeweza kuongea ukasema yes rais ameongea ndani na nie ya nchi wanaelewa..
 
Back
Top Bottom