Mwanasimba mwenzangu isikupite hii

Mwanasimba mwenzangu isikupite hii

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
KUNA MTU MCHAFU KULIKO KASIM DEWJ SIMBA?
KWA KUWA UMETUCHOKOZA WACHA TUSEME.

Kasim Dewj unapotembe kwenye media usisahau kusema na ubadhirifu wako kuiibia klabu ya Simba. Achana na dola feki ambayo ni kashfa isiyokuwa na ushahidi.

Ueleze uma kwamba ni wewe uliyeingina mikataba feki ya kuendeleza na kupangisha majengo ya Simba ya pale Msimbazi na fedha zote ukaingiza mfukoni mwako wakati ukiwa katibu mkuu wa Simba.

Ulitulaghai kwamba mkataba ni wa miaka 30 huku Simba ikiambulia shilingi milion 48 kwa mwaka. Ni kipindi hiki cha mwenyekiti muheshimiwa Mangungu ndio ilibidi wachimbe hiyo mikataba na kugundua ulidanganya na mkataba ulikuwa ni wa miaka kumi ila wewe ulisema 30 ili muda ulipoisha uchukue kodi uweke mfukoni na uilipe Simba fedha kiduchu.

Umefanya hivyo kwa miaka mitatu baada ya mkataba kumalizika mpaka pale Mangungu na watu wake walipokuja kubumburua dili.

Leo Simba inaingiza zaidi ya milion 500 kwa mwaka kwa kodi ya majengo yake.
Maana yake ni kwamba ulipanga kwa miaka 30 uwe unakusanya kodo ya zaidi ya milion 500 halafu ulipe Simba milion 48 na nyingine zote uweke mfukoni mwako. Wizi gani huu? Baada ya dili kubumburuka kwa wenye mkataba kuweka hadharani mkataba kukwepa kufukuzwa kwenye jengo na kupelekwa mahakamani leo ndio wanalipa zaidi ya milion 500 kwa mwaka. Na wanasema wazi ulificha mkataba kwa nia ya kuiba fedha za klabu.

Hili ni eneo mojawapo linalokufanya ujenge chuki na viongozi wa Simba.
Nani mchafu kuliko wewe Simba?

Ni wewe Kasim Dewj miaka nenda rudi umekuwa ukihujumu mapato ya jezi na kujipatia fedha nyingi kwa kuhujumu mapato ya klabu. Ni nani mwingine mtengeneza jezi feki za Simba kuliko wewe? Ukiijua biashara ya jezi vizuri kuliko mtu mwingine yeyote bado kwenye tenda ya jezi za Simba uliweka mezani milion 300 huku Fred Vunjabei akiweka mezani bilion 1.1 kwa mwaka.

Nani mjinga angekupa tenda? Unamjengea Babra chuki mpaka kwenye jambo lililo wazi na peupe kama hili? Ulitaka uendelee kuhujumu mapato ya klabu mpaka lini? Fedha zako zote umepata kupitia wizi wa kuihujumu Simba. Kwa nini isifike mahali angalau uwe na huruma kwa hii klabu?
Wizi gani huo?

NANI NI MCHAFU KULIKO KASIM DEWJ KWENYE SIMBA?
UNAPOTEMBEA KWENYE MEDIA TUNAOMBA UWE UNASEMA NA HUU UCHAFU WAKO.
( Jicho la tatu la KAGAME).
WANASIMBA WENZANGU TUUNGANE NA MH KIGWANGALA KUHOJI MAMBO
 
kwa nini huyo jamaa asifungashiwe virago
 
Eti kagame. Unamfahamu Kagame ama unamsikia tu?. Kagame gani mbwiga tu unalia lia?. Mikia wote kama mmelogwa mnalia lia
 
Uswahili ndio ninao uona, ligi ya tanzania sio bundersliga. nadhani tujipangeni msimu ujao tuache ujinga + uswahili.
 
Baada ya kassim kuondoka wamepita viongozi wengi akiwemo Dalali, Rage, Aveva, Nkwabi na sasa Mangungu. Kila mwaka Luna taarifa ya fedha ya klabu inasomwa, INA maana wakaguzi wore walishindwa kugundua? Labda ungemsema kuingia mkataba ambao walidanganya watajenga msingi was ghorofa Saba wakati sio kweli na jinsi alivyokuwa anawapiga Simba kwenye mauzo ya jezi.
 
Back
Top Bottom