Mwanasimba popote ulipo anza kushangilia kwani wameshauvagaa ' mtego ' wenyewe Morogoro

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama hujanunua tiketi yako ya Derby ya Jumapili nakuomba sana wahi sasa hivi kanunue kwani tayari Yanga SC wameingia ' mtegoni ' huko Morogoro na sasa wanagombana na kulaumiana kwani mbinu iliyotumia ni ya Kimafia zaidi na kama Yanga SC hatofungwa Jumapili Kichwa changu halali yenu wote.

Jana Yanga SC walionywa vizuri kabisa pale Morogoro kuwa waache kutufuata fuata wana Simba SC hasa kwa kutufanyia mambo yao ya ' Ushirikina ' hawakusikia na mmoja wa Komandoo wao ' Kiherehere ' Carlos Ze Don akawachuuza wenzake na kilichofanyika leo huko Morogoro naongezea kusema kwamba kama Yanga SC hatofungwa na Simba SC Jumapili tarehe 29 April 2018 kanitupeni Mto Ruaha au Rufiji niliwe na Mamba au Kiboko.

Simba SC tusilaumiwe kwa Kichapo cha Kishalubela / Hatari ambacho huenda kikasababisha Yanga SC kutokee ' Fujo ' ambayo tokea ianzishwe haijawahi kutokea kwani wametuchokoza Simba SC ambao tulitaka tu ' ustaarabu ' nao ila kwakuwa wametaka tufanyiane ' uhuni ' sasa wana Yanga SC jiandaeni kulia na wengi wenu ' mtazimia ' mno kwa Mchina hiyo Jumapili.

Na Simba SC tunatoa ' ONYO ' kali ole wenu Hospitali hizi mbili ( majina nayahifadhi ) za Morogoro na Dar es Salaam mtoe ' Maiti ' yoyote kuwapa Yanga SC ambao sasa wanahaha ' kuchomoa ' ili wakafanye yao maeneo ya Kiromo Bagamayo au katika Bahari ya Bagamoyo kwani Simba SC tumeweka ' Majasusi / Manjagu ' hatari hivyo kwa Hospitali yoyote ile itakayotoa ' Maiti ' kwa Yanga SC mtatutambua na tutawachomeeni kwa Baba Magu mapema tu.

Si mmetaka mechi hii ichezwe ' Kiuchawi ' zaidi sasa mtatutambua Simba SC ambao ' Uchawi ' Kwetu ndiyo Makao Makuu na huyo Commando wenu anayewaponzeni kila Derby ikija Carlos Ze Don Jumapili atafute Wodi ya kulazwa kwa ' Presha ' kwani nina uhakika kwa Kipigo Yanga SC itakachokipata naogopa yanaweza yakawa mengine Kwake.

Namalizia tu kwa kusema kama Wewe ni Mwanasimba uliyepo Dar au nje ya Dar nikimaanisha Mikoani na hata Wewe Mwanasimba uliyepo nje ya Tanzania au Ng'ambo tafadhali kajipatie upesi tiketi yako ili uone ' mauaji ' ya ' Shalubela ' hiyo Jumapili.

Tumeshawakamata kila idara Yanga SC na hasa idara ya ' Ulozi ' ambayo sasa inasimamiwa na Babu wa Kiluguru na Bibi wa Kipemba mwenye Ziwa Moja ambaye Siku zote hajawahi kutuangusha wana Simba SC na mpaka sasa Babu wa Morogoro na Bibi wa Kipemba wote wanacheka tu kwani ' shughuli ' wameshaimaliza na kama Yanga SC wanataka kuepuka Kipigo hicho na wasifungwe basi wanatakiwa kumtoa ' Kafara ' ( namaanisha Wafe kabisa ) Makamu Mwenyekiti wao Sanga au Katibu Mkuu wao Mkwasa au Mchezaji mmoja kati ya Tshishimbi na Chirwa ila kwa bahati mbaya wote hao walipotakiwa kutoa ' ushirikiano ' wao wa Kutukuka wa Kufa na Kufariki kwa ajili ya Yanga SC walikataa na kusema uhai ni muhimu kuliko Kaburi.

Nawasilisha.
 
hahaaaaaaaaa kicha chako ni halali yetu ?

Ndiyo Mkuu. Hivi Wewe hujiulizi kwanini GENTAMYCINE nina furaha hivi? Kwa kilichofanyika Morogoro usiku wa kuamkia leo ndani ya Kambi ya Yanga SC Mkuu nakuhakikishia tegemea Vita kubwa sana pale mitaa ya Twiga na Jangwani siku ya Jumapili jioni kwani kitakachowatokea Yanga SC hawajawahi kukipata tokea Klabu yao ianzishwe. Wameanza wenyewe Sisi tumemaliza tayari na unaambiwa Yanga SC wanahaha Morogoro na Dar es Salaam lakini kila wakienda kwa Babu / Mtaalam wao wanayemtegemea sana katika mechi za Simba SC anachowaambia tu ni kwamba ili wayapindue matokeo lazima Mtu mmoja kati ya Viongozi au Wachezaji atolewe ' Kafara ' la Kufa na wao Kufa au Kufariki kwa sasa hawataki.
 
GENTA huwa nakuaminia sana na ramli zako hukoseagi kuhusu ushindi wetu

Wahi upesi kajipatie Tiketi yako Jumapili ukale raha kwa ' Mchina ' uone Okwi, Bocco, Kichuya, Muzamiru, Mavugo na Nyoni watakavyoimaliza Yanga SC.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] watoe kafara
 
kwahio ni bet kabisa hio mechi uhakika wa kula upo
 
kwa mawazo haya, mpira wetu hauwezi kutoboa... Anyway sisi wana wa jangwani Mpira ni uwanjani, n'a Tuna kawaida y'a kueshimu matokeo ya uwanjani. Hayo y'a ulozi tunawaachia nyie kina Genta n'a Simba yenu.
 
kwa mawazo haya, mpira wetu hauwezi kutoboa... Anyway sisi wana wa jangwani Mpira ni uwanjani, n'a Tuna kawaida y'a kueshimu matokeo ya uwanjani. Hayo y'a ulozi tunawaachia nyie kina Genta n'a Simba yenu.
 
kwa mawazo haya, mpira wetu hauwezi kutoboa... Anyway sisi wana wa jangwani Mpira ni uwanjani, n'a Tuna kawaida y'a kueshimu matokeo ya uwanjani. Hayo y'a ulozi tunawaachia nyie kina Genta n'a Simba yenu.
 
kwa mawazo haya, mpira wetu hauwezi kutoboa... Anyway sisi wana wa jangwani Mpira ni uwanjani, n'a Tuna kawaida y'a kueshimu matokeo ya uwanjani. Hayo y'a ulozi tunawaachia nyie kina Genta n'a Simba yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…