Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,591
- 6,946
Mwanasoka raia wa Uturuki Aykut Demir alikataa kuvaa tisheti maalumu zilizoandikwa "No To War" katika mechi ya Jumapili iliyoikutanisha timu yake ya BB Erzurumspor dhidi ya vinara wa Turkish Second Division timu ya Ancaragucu
Aykut alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo, alisema "Maelfu ya watu wanakufa kila siku huko Mashariki ya kati, najisikia vibaya naungananao kwenye maumimivu watu wasiokuwa na hatia, wale ambao wanapuuza mauwaji yao wanafanya vitu hivi linapokuja swala la nchi za ulaya, sikutaka kuvaa hizo tisheti kwa sababu hazikutengenezwa kwa ajili nchi za kule".
Mimi ni Dalmine nasema hivi,
Mwanaume PUTTIN yuko sawa kabisa. Palestina, Syria na Nchi zingine za kiarabu watu wanauliwa kila leo pamoja na watoto wasiyokuwa na hatia lakini limeonekana jambo la kawaida kama vile wanaouliwa kule ni wanyama na siyo binadamu. Lakini imeguswa nchi ya ulaya kila mtu anapiga kelele. Siungi mkono mauwaji yanayotokea ukraine kama NIKWELI WANAUAWA, lakini nguvu zinazotumika sasa kupinga haya mauwaji yangetumika mashariki ya kati nadhani ingelikuwa vizuri zaidi.
Mungu awe pamoja nawe ndugu yetu Aykut.