Mwanasoka Raia wa Uturuki Aykut Demir alikataa kuvaa tisheti maalumu zilizoandikwa "No To War" Sababu?

Mwanasoka Raia wa Uturuki Aykut Demir alikataa kuvaa tisheti maalumu zilizoandikwa "No To War" Sababu?

Safi sana huyo mwamba. Huwa sina shaka na waturuki. Maelfu wanauwawa kwa vita za mchongo Afrika na Arabuni. Marekani ni adui wa dunia. Mimi hata nchi yao sijawahi kutamani kwenda kama wengi walivyo na ulimbukeni wa kutamani kwenda huko.

NB: Nimekomenti kama mtu huru sina mahaba na nchi yoyote ila nasimamia haki. Hata hao Urusi pengine wangekua super power wangetuchezeshea ngoma ileile kama wamarekani. Watu weupe hawaaminiki, maslahi mbele kwa gharama za uhai.
 
Jamaa wanapenda sana mambo ya dini wasiwasi umewajaa. Kutafuta amani kunaanzia kwao wenye vita wenyewe na dunia inawaunga mkono ila vita vingi vinavyopigwa kwenye nichi za kiarabu ni wao na makundi yao wanachangia amani isiwepo wao hawafundishwi kutafuta amani ila kulipiza kisasi kuuwa kwa kujitoa muhanga, mabomu na ukatili mwingi. Itawachukua miaka mingi kupata marafiki mana kweli hawaaminiki....
Vipi kama waisrael ndiyo wangerikuwa ndiyo wanauawa!
 
Mrusi na Marekani walikuwa anadondosha mabomu daily ktk majiji ya Raqqah,Allepo, Kobane, Tadmur,Mosul n.k ndani ya Iraq na syria lakini hakukuwa na matangazo kama haya ya Ukraine.

Na hizi propaganda zote za kimagharibi ni kwasababu tu anaepigana ni hasimu wao (Putin) ,laa sivyo angekuwa ni mmarekani n uingereza ndio wanashambulia basi media zao zote zingebariki
 
Maisha wanayoishi wa Ukraine hii wiki ndio maisha wanayoishi wa middle east na Africa kwa miaka mingi.

I'm pro-peace lakini kitu kinachonitia hasira Hawa wazungu kujiona hawastahili vita ni kweli hakuna aneyependa kufa ,lkn wao wanasema hayo mambo ya kuuana ni ya waafrica na waarabu....yaani sisi tukifa hakuna shida.

Kuna muda naona wauwane tu 💔
 
View attachment 2137541
Mwanasoka raia wa Uturuki Aykut Demir alikataa kuvaa tisheti maalumu zilizoandikwa "No To War" katika mechi ya Jumapili iliyoikutanisha timu yake ya BB Erzurumspor dhidi ya vinara wa Turkish Second Division timu ya Ancaragucu


Aykut alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo, alisema "Maelfu ya watu wanakufa kila siku huko Mashariki ya kati, najisikia vibaya naungananao kwenye maumimivu watu wasiokuwa na hatia, wale ambao wanapuuza mauwaji yao wanafanya vitu hivi linapokuja swala la nchi za ulaya, sikutaka kuvaa hizo tisheti kwa sababu hazikutengenezwa kwa ajili nchi za kule".

Mimi ni Dalmine nasema hivi,
Mwanaume PUTTIN yuko sawa kabisa. Palestina, Syria na Nchi zingine za kiarabu watu wanauliwa kila leo pamoja na watoto wasiyokuwa na hatia lakini limeonekana jambo la kawaida kama vile wanaouliwa kule ni wanyama na siyo binadamu. Lakini imeguswa nchi ya ulaya kila mtu anapiga kelele. Siungi mkono mauwaji yanayotokea ukraine kama NIKWELI WANAUAWA, lakini nguvu zinazotumika sasa kupinga haya mauwaji yangetumika mashariki ya kati nadhani ingelikuwa vizuri zaidi.

Mungu awe pamoja nawe ndugu yetu Aykut.
This is already World War III. Putin started it long ago & Ukraine is only the current front. He will escalate anyway, and it's even more likely if he succeeds in destroying Ukraine because you have again convinced him you won't stop him even though you could.
 
Back
Top Bottom