Mwanaume afariki akifanya tendo la ndoa, mwanamke asema "Alihema kwa kasi kisha akaanguka pu!"

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mwanaume mmoja amefariki dunia wakati akiwa faragha na mpenzi wake katika nyumba ya wageni kwenye ghorofa moja jijini Nairobi.

Taarifa za Polisi zinasema, Joseph Ngaruiya umri miaka 40, anadaiwa kupata shida ya kupumua akiwa na mpenzi wake katika vyumba vya Myra, Jumatatu, Februari 28, 2022.

Siku ya tukio hilo, Ngaruiya aliingia katika nyumba hiyo iliyoko kando ya Barabara ya Kindaruma kabla ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyejulikana kama JM kufika.

Dakika chache baadaye, mpenzi huyo, ambaye inasemekana ni mfanyakazi wa KRA, alitoka nje ya nyumba hiyo ghafla, huku akipiga mayowe, akisema mpenzi wake alikuwa ameanguka na kufariki dunia.

Polisi walitembelea eneo la tukio wakiwa na wahudumu wa afya ambao walithibitisha kuwa alikuwa amefariki na waliupeleka mwili wake katika makafani wakisubiri uchunguzi wa maiti.

Katika ombi lililowasilishwa kortini Jumatano, Machi 2, 2022, JM alipohojiwa, alikiri kwamba waliingia ndani ya nyumba hiyo saa kumi na mbili jioni na walipokuwa wakifanya mapenzi, Joseph alianza kuhema kwa sauti kabla ya kuanguka.

Mwanamke huyo aliwaambia Polisi kwamba alijaribu kumuuliza marehemu alikuwa na shida ipi lakini hakumjibu, jambo lililomfanya kutafuta msaada kutoka kwa usimamizi wa jengo hilo na wakati huduma za dharura zilipofika, tayari alikuwa amefariki dunia.

Afisa mpelelezi aliiambia mahakama kuwa timu ya maafisa wa polisi kutoka eneo la Kilimani walitembelea eneo la tukio na kukuta mwili wa Ngaruiya ukiwa umekaa huku ukiegemea ukutani.

Wakamatwa kwa kukutwa na nyara za serikali
Msako ulifanyika katika nyumba hiyo na dawa kadhaa za aina mbalimbali, vileo na vinywaji baridi vinavyoaminika kuwa vya marehemu vilipatikana.

Serikali ilimtaka Hakimu Zainab Abdul kuwapa siku 14 za kufanya uchunguzi wa maiti na kuvifanyia uchunguzi vitu vilivyokutwa ndani ya chumba hicho ili kubaini kilichosababisha kifo chake.

Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai DCI wanataka mpenzi huyo wa marehemu Joseph Ngaruiya, akamatwe na kuhukumiwa.

Source: Kenyanlyrics

00niagara1-superJumbo.jpg
 
View attachment 2138222
Mpenziwe ahukumiwe kwa kosa lipi?
 
Haya kama ulikuwa ni mchepuko sasa kimeumana
Watoto wake na mke wake sijui wamelichukuliaje hili suala

Baki njia kuu michepuko siyo dili
 
Amejojoa rohoo..

Muwe mnakula Kwanzaa na kushiba kabla ya mechi.. Sasa from kukojoa hewa to kukojoa roho mchezo? Njaa zitawaua nyang'au
 
Back
Top Bottom