Mwanaume ajitokeza na kudai ameporwa demu na Nuh Mziwanda!

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Posts
10,518
Reaction score
13,144
Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.

Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.
Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.

Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana. “Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.

“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali. “Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho. “Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.

 
Huyo Dada mpz wake mziwanda ni Mwanafunzi wa drs la saba aliyeachishwa Shule ya msingi Gilmani Rutihinda iliyopo Kata ya Kigogo wilaya ya kinondoni. deal limechezwa mtoto kaachishwa Shule.Na amesajiliwa kufanya Pepar ya mwezi September nashangaa hata hatua za kinidhamu hazija chukuliwa hii ndiyo Tanzania ya magufuri kwa kwenye Pesa wanatesa
 
Kumbe na Nuh ni mlamba lips tu kama aikana bobu junio.
 
Tetesi: ninasikia ndoa ya mkeka imepita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…