PROF NDUMILAKUWILI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2016
- 10,518
- 13,144
Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.
Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.
Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana. “Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.
“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali. “Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho. “Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.