POTOSHI Mwanaume aliyemwokoa mwanamke kutoka kwenye ajali ya gari sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono

POTOSHI Mwanaume aliyemwokoa mwanamke kutoka kwenye ajali ya gari sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu hii video inatembea sana mtandaoni kuwa Mwanaume aliyemwokoa mwanamke kutoka kwenye ajali ya gari sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono. Je, mtu anawezaje kumshitaki mtu aliyeokoa maisha yake na kuita unyanyasaji wa kingono wakati wa kumuokoa? hii ni ya kweli?



1768031824051.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni na kueleza tukio la mwanaume anayedaiwa aliyemwokoa mwanamke kutoka kwenye ajali ya gari na sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono ambapo katika video hiyo upande wa walalamika wanaeleza kuwa hata wakati wa dharula kunahitajika ridhaa ili kumgusa ama kumshika mtu wakati wa kumuokoa.

Video hiyo ilichapishwa katika mtandao wa Instagram kwenye ukurasa unaojulikana kama interestingfindz Desemba 18, 2025 ikiwa na watazamaji zaidi ya milioni 25, ikisambazwa zaidi ya mara laki 4 huku watu wengi wakikosoa kitendo cha mwanaume huyo kushtakiwa na kwamba aliyedaiwa kuwa mwanamke katika video hiyo hakustahili kusaidiwa na kuhamasisha wengine kutokusaidia wanaokumbwa na changamoto au dharula kama hiyo.

Je, ni upi uhalisia wa video?

Ufuatiliaji wa kina wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo inapotosha uhalisia kwani taarifa hiyo imetengenezwa kwa kuhusisha video isiyohusiana na taarifa hiyo kama ilivyoripotiwa.

Kwa kutumia Google reverse image search imebainika video hiyo ambayo ni ya kutengenezwa ilipangwa kwa ajili ya dhumuni la kutoa elimu kuhusu usalama barabarani ambapo tukio hilo liliongozwa na watumiaji wa TikTok kutoka Belarus, familia ya Gomylyaev.

Walichapisha video hiyo TikTok Novemba 30, 2022 ikiwa na ujumbe wa kuhamasisha umakini barabarani. Maandishi yaliyo juu na chini ya picha yanasema: “Usivunje sheria za barabarani!!!” na “Kaa makini na uwe mwangalifu barabarani!”

Kadhalika wanatahadharisha kuwa kwa kusema "Video hii imetengenezwa kwa madhumuni ya kielimu. Tukio linaloonyeshwa ni la kubuniwa na limerekodiwa na wataalamu. Usijaribu kulirudia."​

Kadhalika video hiyo inaonesha ilirekodiwa tarehe 26 Novemba, 2022.

pasy-1140x602-c-default-jpeg.3527835
Katika video hii, mwanamke anaeleza kuwa video hiyo ilitengenezwa kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaonya madereva, kwamba wakati wa majira ya baridi hali ya hewa si rafiki kwa mwendo wa kasi na uendeshaji hatarishi. Pia, kutokana na mwonekano kuwa duni mara nyingi, ni rahisi kutokea majanga. Hivyo basi, video hiyo yenye kile kinachoitwa “Guardian Angel” iliundwa ili kuvuta umakini juu ya ukiukwaji wa sheria za barabarani.
​
Back
Top Bottom