Mwanaume aliyeziacha familia kwenye maumivu

Mwanaume aliyeziacha familia kwenye maumivu

Hypersonic

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2012
Posts
829
Reaction score
1,564
Wakuu habari zenu,

Iko hivi uko kwa Biden bana kuna jamaa aliyefahamika kwa jina la Richard Hoagland, ambaye alimuoa mwanamke aliyetambulika kwa jina Linda Iseler na walibahatika kupata watoto wawili wa kiume.

Kwa kipindi chote cha maisha mambo yalikuwa poa kabisa na mahaba niue. Mnamo waka 1993 bwana Richard alitoweka nyumbani na gari yake kukutwa imetelekezwa airport.

Polisi walianza kumtuhumu mke kuwa anajua nini kilichotokea kwa mmewe. Maskini wakati mama anapitia yote kwa kipindi cha miaka 23, mshikaji alikuwa na maisha mengine hapo hapo USA AKITUMIA utambulisho wa marehemu baada ya kuokota cheti cha kifo mtu aliyejulikana kwa majina ya Terry Symansky aliyeariki 1991 akaamua kutumia jina la marehemu na kama haitoshi akapanga kwenye nyumba ya babake marehemu na kwa kuwa baba wa marehemu alikuwa mzee bwana Richard akatumia nafasi hiyo kutaka kujua ni kwa namna gani Terry alikufa na hii ilimsaidia kuendesha maisha yake ya ulaghai na hatimaye akafunga ndoa na mke mwingine mpaka anakamatwa alikuwa tayari ana watoto wengine wawili.

Wakati anakuja kukamatwa ndio mke wa pili anagundua alikuwa ameolewa na babu janja.

Nisikuchoshe hii story ni kama filamu nimekuwekea link hapo chini pitia mwenyewe uone duniani kulivona maajabu.

After 23 Years, Wife Learns Truth About Missing Husband
 
Back
Top Bottom